Fahamu jinsi ambavyo mapacha hutokea

Dr PL

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2024
Posts
327
Reaction score
537

Picha kwa hisani ya Google

Mapacha hutokea pale ambapo yai linaporutubishwa hugawanyika mara mbili au zaidi kutoa mtoto zaidi ya mmoja au pale ambapo yai zaidi ya moja hurutubishwa na mbegu za kiume. Hali hii hutokea kwa viwango tofauti kulingana na jamii husika mfano kwa Waafrika ktk kila mimba 20 moja ni ya mapacha. Hata hivyo kutokana na maendeleo ya sayanasi na tekinolojia viwango hivi vimeongezeka ktk Karne hii.

AINA ZA MAPACHA:
Kuna aina mbili

(1). Mapacha Wanaofanana (identical twins): hutokana na yai moja lililorutubishwa na mbegu moja ya kiume kisha kugawanyika kutoa watoto wawili. Wakiwa tumboni hushirikiana vitu vingi pamoja. Mara nyingi watoto hao ni wa jinsia moja.

(2). Mapacha Wasiofanana: (non-identical/fraternal twins): hutokana na mayai tofauti ya kike kurutubishwa na mbegu tofauti ya kiume. Wakiwa tumboni kila mmoja hujitegemea, hawana ushirikiano wa moja kwa moja. Watoto hawa wanaweza kuwa wa jinsia moja au tofauti.

VISABABISHI (RISK FACTORS):
Si kila mwanamke anaweza kupata mapacha bali wale ambao wana sifa au vichocheo visababishayo hali hiyo kutokea. Hivi ni baadhi ya visababishi (risk factors) vya kupata mapacha:

(a). Kurithi: Historia ya kuwa na mapacha ktk familia upande wa mwanamke/mama: Mwanamke hurithi vinasaba (genes) ambazo huathiri moja kwa moja hali ya mayai yake (yaani uzalishaji na kugawanyika yanaporutubishwa).

(b). Kubeba mimba ktk umri mkubwa: tafiti zimeonesha wanawake wanaobeba mimba ktk umri mkubwa kati ya miaka 30 na 35 wanaweza kupata mapacha. Hata hivyo baada ya umri wa miaka 35 nafasi hiyo ya kupata mapacha pia hupungua.

(c). Asili (race): wanawake wenye asili ya Africa (weusi, black race) wana nafasi kubwa kupata mapacha ukilinganisha na wenye asili ya Ulaya na Asia. Mapacha wanaofanana ni wengi sana kwa wanawake wenye asili ya Africa (weusi).

(d). Kujifungua watoto wengi /uzao mwingi (high parity): wanawake wenye uzao kuanzia 5 na kuendelea wanakuwa na nafasi ya kupata mapacha kwenye mojwapo ya uzao.

(e). Matumizi ya dawa za uchavushaji ambazo huchochea mayai ya mwanamke kuzalishwa kwa wingi hivyo kuongeza nafasi ya yai zaidi ya moja kurutubishwa na hivyo kupata mapacha.

(f). Matumizi ya njia za kisasa za urutubishaji mayai. (In vitro fertilization, IVF): kutokana na maendeleo ya sayanasi na tekinolojia wenza wanaweza kutoa mayai na mbegu zao na kisha kurutubishwa kwenye maabara/kiliniki maalumu ili kupata mapacha. Hii ni njia mpya na hivyo ina gharama kubwa, sio wote wanamudu kulipia.

Kwa kuhitimisha: uzi huu nimeandika ili kutoa uelewa kwa jamii/wana ndoa kuhusu namna mapacha hupatikana ili kuondoa mkanganyiko au kulaumiana hasa pale wanapotamani kupata mapacha.
Karibuni sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…