Fahamu jinsi ya kuandaa Bajeti ya Mradi (Project Budget)

Fahamu jinsi ya kuandaa Bajeti ya Mradi (Project Budget)

The Consult

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2017
Posts
220
Reaction score
252
1.jpg

Mafanikio katika mradi (wakati mwingine) huangaliwa ni kwa kiasi gani shughuli za mradi (project activities) zimetekelezwa ndani ya bajeti iliyopangwa. Utekelezaji wa mradi ndani ya bajeti hutokea tu, pindi bajeti husika inapoandaliwa kikamilifu na kuzingatia vipengele vyote muhimu.

Bajeti ya mradi (Project budget) ni makisio (estimates) ya gharama zote za shughuli za mradi; hii hujumuisha gharama za malighafi (material procurements), gharama za uendeshaji (on going operations cost), gharama za usafiri na mafunzo (training and travel costs) n.k. Bajeti ya mradi humsaidia mfadhili (Donor) kujua ni kwa namna gani fedha zitatumika pia humsaidia kupima faida na gharama ya mradi husika (Cost/Benefit Analysis)

Uandaaji wa bajeti ya mradi hutegemea taarifa zifuatazo ambazo ni;
  • Makisio ya gharama ya shughuli (Activity cost estimate)
  • Kalenda ya mradi (Project schedule)
  • "Basis" ya makisio

Mnyambuliko wa shughuli (Work Breakdown Structure) ni hatua muhimu na ya msingi katika kuandaa bajeti ya mradi wako. Mnyambuliko wa shughuli pia utakuwezesha kujua shughuli ipi ianze na ipi ifuatie.
Kwa mfano ; Shughuli ya kufanya hafla ya chakula cha Usiku/To provide banquet (Hii inasimama kama shughuli mojawapo katika shughuli za mradi X)

Katika kutekeleza shughuli hii itakubidi uivunje vunje (Breaking it down) ili kupata shughuli ndogo ndogo ambazo utaweza kuzifanya kiurahisi kama ifuatavyo;

Shughuli ya kufanya hafla ya chakula cha Usiku (Shughuli kuu)
  1. Upangaji na usimamiaji (Hapa itajumuisha uandaaji wa bajeti, uratibu wa shughuli n.k)
  2. Chakula (Hapa itajumuisha kuandaa list ya vyakula/menu, list ya manunuzi, mapishi n.k)
  3. Ukumbi na vifaa (Hapa itajumuisha utafutaji wa ukumbi,upangaji wa viti na meza,mapambo n.k)
  4. Uandaaji wa wageni (Hapa itajumuisha utengenezaji wa list ya wageni, kutambua mahitaji maalum ya wageni n.k)
  5. Kuandaa wafanyakazi (Hapa itajumuisha kuandaa wapishi, wahudumu, wapokeaji, wafanya usafi n.k)
  6. Kumuandaa m(wa)zungumzaji (Hapa itajumuisha ualiko, kuandaa usafiri, uandaaji wa mada n.k)
Hivyo katika uandaaji wa bajeti ya mradi wako; unapaswa kufahamu gharama za kila kipengele katika shughuli hizi ndogo ndogo, kisha utajumlisha gharama za vipengele vyote, hapo utakuwa umepata gaharama nzima ya shughuli ya kufanya hafla ya chakula cha usiku, kisha utaingia katika shughuli zinazofuata mpaka mwisho. Jumla ya gharama ya shuguli zote ndio itakuwa gharama ya mradi wako.

Vitu vya kuzingatia wakati wa uandaaji wa bajeti;
  • Hakikisha unashirikisha timu ya mradi katika kupata makisio ya mahitaji ya mradi, usiifanye kazi hii peke yako.
  • Kila taasisi ina utaratibu na muongozo katika kuandaa bajeti ya mradi; hivyo pindi uandaapo bajeti yako ni vyema ukazingatia taratibu na muongozo wa taasisi yako.
  • Zingatia thamani ya pesa (Net Present Value &Future Value)

The Consult ; +255 719 518 367
Dar es Salaam
Tanzania


Calls for Proposals


 
Asante sana boss. Ila ni jinsi gani tunaweza kupata donors kwa mradi husika..??
Mkuu
Kuna njia nyingi ambazo hutumika kutafuta donation ya mradi wako, miongoni mwazo ni;
  • Ku-respond call for proposals iliyotolewa na mfadhili, ukijiridhisha kwamba uko na sifa (eligibility) ya kupewa fedha, basi unaweza omba.
  • Kupeleka andiko lako (Project proposal) kwa wafadhili mbalimbali, hata kama hawajatoa call for proposals, ila hakikisha malengo ya huo mradi wako yanagusa INTERESTS za mfadhili husika, pia hakikisha unaifahamu vyema sera yake ya uchangiaji katika maendeleo kwa kipindi husika (Kumbuka, sera hubadilika mwaka hadi mwaka).
MUHIMU: Jitahidi kuwa unazingatia cost sharing, kwa maana ya kwamba; unapompelekea mfadhili andiko lako, jitahidi kuonyesha kwamba nawe umeweka mchango wako (Hii itaonyesha kwa kiasi gani uko committed katika mradi wako), japo kuna wafadhili wengine hutoa ufadhili kwa asilimia 100.
,
Karibu kwa huduma
 
mkuu, umeweka maneno vizuri sana. Ubarikiwe.
Tushushie na mbinu za kugundua kama mradiw ako utamalizika kwa ghalama iliyopangwa mapema. Ikiwepo Earned Value Management. Mkuu tatizo kubwa la miradi yetu ni Kumalizika kwa Gharama iliyo nje ya iliyokubalika wakati mradi unaanza.
 
mkuu, umeweka maneno vizuri sana. Ubarikiwe.
Tushushie na mbinu za kugundua kama mradiw ako utamalizika kwa ghalama iliyopangwa mapema. Ikiwepo Earned Value Management. Mkuu tatizo kubwa la miradi yetu ni Kumalizika kwa Gharama iliyo nje ya iliyokubalika wakati mradi unaanza.
Shukrani kwa pongezi Mkuu.
Nitazingatia takwa lako.
Karibu Sana
 
Asante...umenifanya nikumbuke darasani.... hizo mambo zilikuwa tamu sana na nilikuwa nawahi kipindi...
 
Back
Top Bottom