Fahamu jinsi ya kutumia LinkedIn kupata ajira

Fahamu jinsi ya kutumia LinkedIn kupata ajira

Nafaka

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
12,154
Reaction score
31,246
Habari ya humu ndani.

Mimi siyo HR wala mtaalam sana wa mambo ya HR ila ninataka kutoa mtazamo wangu kutokana na uzoefu wangu.

Katika mitandao bora kabisa ambayo inaweza kubadili maisha yako ni Linkedin hasa kwa wanaotafuta kazi au hata wenye kazi ambao wanatafuta kazi ya ziada au kazi bora zaidi.

Lakini shida ni kwamba watu wengi wanaitumia Linkedin kama vile wanavyotumia Facebook kitu ambacho siyo sawa kabisa.

Kwa mfano, mtu amejiunga Linkedin toka mwaka 2015, hajawahi kuupdate profile yake kwa kuongeza new skills na experience, hajawahi kushow case kazi zake n.k.

Mtu connects zake ni za marafiki zake ambao unakuta wengi nao wanatafuta kazi au wana kazi za kuunga unga, ameconnect pia na watu mashuhuri tu wakina Bilgates, Warren Buffet, Elon Musk n.k. Siyo vibaya kuconnect na marafiki zako lakini Linkedin siyo sehemu ya kupiga umbea na story na marafiki. Siyo vibaya kuwafollow wakina Bilgates, lakini mara nyingi huwezi kupata ajira kutoka kwao.

Jambo la msingi, ni kuconnect na maHr na makampuni, na watu ambao wako kwenye field/eneo ambalo linaendana na kazi unayotafuta. Yani uwe una circle ya watu ambao wanafanya kile unachokifanya na umeconnect na mahr.

Pia ni vizuri kufollow makampuni maana itakuwa ni rahisi kujua kama wametangaza kazi na kujua ni kitu gani kinachoendelea katika makampuni hayo.

Haya ninayozungumza ni kutokana na experience yangu ya muda mfupi toka nimetumia huu mtandao na response ninayoipata. Pia kama unaweza hata kutengeneza kivideo ukakiweka kwenye profile siyo mbaya.

Dunia imebadilika, juzi nimemuona HR flani katangaza kazi Linkedin anasema hataki watu watume documents za CV anataka mtu ajireodi kwa simu yake na usitumie professional videographer, we jirekodi jieleze elimu yako na experience yako halafu mtumie.

Kwa leo ni hayo tu.
 
Wabongo tuna mwamko mdogo sana kutumia Linkedln, Mtu akijiunga tu anatokomea moja kwa moja.

Wabongo wamejazana Insta na FB, na connection(kazi) itaendelea kwa kujuana tu.
 
Wabongo tuna mwamko mdogo sana kutumia Linkedln, Mtu akijiunga tu anatokomea moja kwa moja.

Wabongo wamejazana Insta na FB, na connection(kazi) itaendelea kwa kujuana tu.

Habari ndio hiyo. Some graduates hawana ubunifu(maujanja ujanja). Hawataki kujifunza kila siku kupitia kwenye mitandao + websites. Hawataki kuuliza watangulizi walitoboa vipi. Wakifika field kazi ni kujiselfie tuu,hawajui mule furksa zipo kibao

Wakiwa Chuo shughuli inakuwa ni ya uchakataji wa papuchi + conmection za porno. Hawataki kutengeneza strong connection pindi wakiwa vyuoni mule kuna kada ya watu tofauti tofauti. Tiktok kwa sana, Ig, Fb. Jamii forums kwa kupapasa, siku hizi twitter imeingiliwa.

Tazama uzi ulivyopwaya, baada ya kugraduate utasikia flani amepata ajira kwa kujuana. Shame upon them!
 
Watu mkipata mnajikuta kila kitu mnajua, halaf wengi wenu mlipata kipindi cha kitonga basi kutwa mnakuja kusakama young graduates, mf's toeni ushauri na ujuzi bila kucrush sisi upcoming madogo, nmeona jitu hapo juu linasemea fb, sijui ig wakat inawezekana kabisa kipindi yupo kwny michakato ya ajira hvyo vitu havikuepo.

Mmepata mazari mkakalia hvyo viti ofsin basi hatuwaambii kitu. Kila kitu mnajua nyinyi, na mtu akiwa hana ajira mbele ya watu kama nyinyi anajiona mkosaji sana. PUNGUZENI MANENO MAKAVU MBELE YA HUSTLERS, NAAMINI HATA NYINYI MNGEZALIWA DUNIA YETU MNGESUFFER VILE VILE.. MFS
 
Ushauri wako ni mzuri sana, lakini umeuleta kwa hasira.
Hasira kwa sababu tumeshindwa kwenda na teknolojia kama ilivyo, kwa mfano simu janja hizi zimeingia kwa fujo sokoni kwenye miaka ya 2011+ hivi.

Lakini kadri muda unavyosonga utandawazi unabadilisha tabia za vijana wetu haswa waliopo vyuoni na kuwa kitu kimoja.

Ok, kuna mdau analalamika hapo kuwa kuna watu wamepata ajira miaka ya Jk, nimuhakikishie kuwa kuna taasisi + mashirika ya Kiserikali ajira zinatoka nyingi sana na niseme jamani eeh haya mambo hayana mchawi wala nini bali skills gani alizo nazo mwajiriwa. Waajiri wanataka kuona ni namna gani utaweza kusukuma miradi yake au shughuli zake zikasonga? mbali na darasani.


Isitoshe hii mitandao haswa Ig imetubadilisha sana mifumo yetu tulivyozoea kuishi miaka ya nyuma, uvaaji, unyoaji sijui maviatu ya ajabu ajabu yaani kiufupi mionekano imekuwa mibovu sana, then kijana anakujia kuwa naomba kazi ofisini kwako sasa unawaza how?


Mdau alishauri vizuri sana,jamani eeh tutumia sana Linked In kuna vitu vya muhimu kule, na mimi naongezea kila hatua + sehemu tutengeneze connection tofauti tofauti pindi tukiwa vyuoni zitatusaidia kwa baadae. Nazungumza haya kwa sabbu nina experience.

KWA HIYO MIMI HASIRA YANGU sio kwamba nawagandamiza wasio na ajira,bali utumiaji mbovu wa mitandao ya kijamii + bila kutafuta furksa kupitia mitandao hiyo na hii ndio hoja yangu.

Yote kwa yote mtoaji ni Mungu + kila mtu ana mhimili wake..ni jambo la muda tuu Mungu anaweza kukuinua na Binadamu wakashangazwa,Imani ni kitu muhimu sana + kumtegemea yeye siku zote.

Pia ndipo Neno la BWANA lilimjia Yeremia na kumwambia “Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa”-Pia yeye ndiye ajuaye mwanzo na mwisho wetu[emoji120]

Muwe na amani ya Kristo
 
Kupitia LinkedIn Nimeshatumiwa ujumbe na ma operations managers wa makampuni mawili..wakitaka kunipa kazi.

Ila niliwaomba niwape the best people i trust kwenye zile kazi walizokua wanataka

Niliko am good.
 
Kupitia LinkedIn Nimeshatumiwa ujumbe na ma operations managers wa makampuni mawili..wakitaka kunipa kazi.

Ila niliwaomba niwape the best people i trust kwenye zile kazi walizokua wanataka

Niliko am good.
Ni sehemu nzuri ikitumika vizuri.
 
Kupitia LinkedIn Nimeshatumiwa ujumbe na ma operations managers wa makampuni mawili..wakitaka kunipa kazi.

Ila niliwaomba niwape the best people i trust kwenye zile kazi walizokua wanataka

Niliko am good.
Nipe uchawi wa kusukuma connection/followers wa Linkedln, nimehasto sana hadi sasa nina 800 tu wengi wao ni WaNiger na Mabeberu, wabongo wachache sijui tunakwama wapi..
 
Nipo linked tangu 2015,

Lakini mkuu usilaumu sana, mtu kajiunga linked atawajue hao ma-hr aweze kuwa follow?!

Anaweza kufollow makampuni husika na taaluma yake, lakini atawezaje kuwafahamu hao ma-hr na kuwafollow bila kuwajua?!

Hapa bado kuna changamoto sana, sipingi mfumo huu ni mzuri kweli, lakini kwa mazingira ya kwetu bado kazi nyingi zitaendelea kupatikana kwa connection tuache ubishi.
 
Back
Top Bottom