Fahamu "Kakumba" mgodini

MC44

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2019
Posts
2,169
Reaction score
3,297
Baada ya kukaa maeneo ya machimbo kwa kipindi flani nimeona na nimefanya vitu vingi. Vingine nimeandika hapa:

Sitasahau biashara ya uchimbaji ilivyonifilisi

Na hii:
Jamaa walivyo dhamiria kuniua kisa machimbo ya dhahabu

Naomba leo nieleze KAKUMBA - dhahabu feki.

Kawaida mawe au fello yakitolewa chini huwekwa kwenye mifuko tayri kwa mnada.
Hapo wanunuzi huja na muuzaji kupanga bei.

Anakuja jamaa na vipande vya kofuli...imesagwa na kuwa unga ananyunyiza kwenye mfuko halafu unakuja kuchukua sampuli unapiga chabo unaona zile chenga za kofuli unajua ni dhahabu unaropoka bei kubwa unachokutana nacho ni siri yako.

Jamaa alichukua mzigo katengeneza hivyo kapeleka kwa mchina kuuza.
Jamaa kapiga chabo kapagawa. Kahesabu pesa ya kutosha.... pikipiki ziliwashwa mwendo wake hata gari za mwenye hazikamati.

Mchina anakuja kushtuka....jamaa wapo baa wanapiga vitu na Malaya pembeni.
Huwezi tena kuwapata

Na ule mzigo anakusanya tuu maudongo hayana chochote.

Karibuni kwenye dhahabu....
 
Hapo ni kwa sababu hao wanunuzi wanakua hawajui kitu kuhusu dhahabu. hiyo inayoitwa kupiga chabo ni jambo la kitaalam na kinachotazamwa ni aina ya ule mwamba wala si chenga au unga wa dhahabu kwa maana ya zile chembechembe za rangi ya shaba zinazoonekana.

Masaihost.com
Web designing and Web hosting solutions
 
Shaba na dhahabu hazifanani ni rahisi sana kutofautisha.
Ila dhahabu na na kofuli zinafanana.
Na hapa kwenye chabo hawaangalii ni mwamba gani. Wanaangalia wingi wa dhahabu tu.
Hiyo ya aina ya mwamba ni hatua nyingine kabisa
 
Nadhan hao wapiga chabo hawana uzoefu wa kutosha!! Kwa uelewa wangu ukitaka kupiga chabo inatakiwa usichukuwe fello, chukuwa jiwe Kama jiwe kwenye mfuko ulioshe , na usafishe sehemu ya kupondeapondea ! Na kuwa makini maana wengine huwa wanatembea na vimawe ambavyo vinaonesha dhahabu real, so akikuchanganyia wakati wa kupondapondaa umepigwaa tayarii [emoji2][emoji2]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yes sasa ukichukua kwenye fello si imekula?
Au wanaweka kichwani kwenye nywele ile unatikisa kisahani......anajikuna zinadondika.
Na hapo mpo wengi ukiona nyingi utaacha na kwenda kuzungumza bei ili wengine wasijue mzigo ni mzuri kumbe unapigwa
 
Na katika upigaji wa chabo huwa hatuchukuwi sempo ya jiwe moja tu, lazima mawe yawe tofauti ili ujilizishe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…