Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 378
- 766
Amewahi kuonyesha kazi zake katika Wiki ya Mitindo ya Mavazi ya Kiume huko Cape Town, Afrika Kusini, Wiki ya Mitindo ya Estelle Mantel nchini Zambia, Wiki ya Mitindo ya Msumbiji, Music on the Catwalk huko New York (USA), Bongo Style huko Ubelgiji (Ulaya), pamoja na Jambo Fashion Affair na Wiki za Mitindo za Swahili nchini Tanzania.
Martin ana tuzo tatu hadi sasa. Mwanamitindo Mwenye Kipaji (2008) tuzo iliyotolewa na Smilling Faces na Mwanamitindo Bora (2010). Mbunifu Bora wa Mavazi ya Kiume (2012) tuzo zilizotolewa na Swahili Fashion Week.
Katika kazi yake ya ubunifu, Martin amewahi kuwabunia mavazi watu maarufu ndani na nje ya nchi. Miongoni mwa watu hao ni pamoja na Uti Nwachukwu mshindi wa Big Brother 5, Monalisa Ekijede mbunifu wa mapambo ya kike kutoka Nigeria, Mwanamitindo Millan Magase, Nassib Abdul (Diamond) na Msanii Hemed Suleiman.
Baadhi ya Mitindo iliyobuniwa na Martin Kadinda:
2011- Alianza kwa kuzindua ubunifu wa makoti ya Blazer yenye kifungo kimoja 'Blazer Single Button'
2018- Kadinda alizindua (designs) za viatu vya kiume vilivyofahamika kama "The Originals"
2020- Katika tamasha la Swahili Fashion Week 2020, alionyesha design ya mavazi ya "Vanguard collection"
2022- Alizindua "Escapade collection" na ilikuwa ni mkusanyiko wa nguo za kitalii zenye ubunifu wa kisasa