Fahamu kuhusu baleghe.

Joined
Aug 11, 2017
Posts
61
Reaction score
78
Kifahamu kipindi cha baleghe
kwa wavulana na wasichana.

Ubalehe ni jumla ya mabadiliko ya mwili na ya roho yanayomfanya mtoto kuwa kijana halafu mtu mzima.


Ufafanuzi.

Ingawa kila mtu ni mwanamume au
mwanamke tangu atungwe (kadiri alivyo na kromosomu Y au la), kabla ya kubalehe tofauti hazionekani sana,isipokuwa katika viungo vya uzazi.

muda unafika wa watoto
kuanza kukomaa kijinsia: ndipo tofauti zinapojitokeza wazi.Kutoka utotoni kuingia utu uzima kuna mabadiliko ya haraka katika viungo, hisia na roho. Kama ilivyo kwa viumbe hai wote, ustawi huo
unaweza ukawahi au kuchelewa, lakini kwa kawaida unatokea kati ya
umri wa miaka 12 na 16.

Wasichana wanawahi kuliko wavulana ,lakini mabadiliko ni yaleyale, nayo yanafanyika hatua kwa hatua.Katika hayo, mengine yanamfurahisha kijana, lakini mengine hayampendezi, anayonea
aibu hata kuyafadhaikia hasa
asipoyaelewa. Bila ya shaka anahitaji msaada wa walezi aweze kukabili hayo yote bila ya kuvurugika kiasi cha kupotoka.

Kwanza mvulana anajikuta akirefuka haraka na kupata misuli mikubwa;

kifua kinapanuka. Papo hapo sauti yake inaanza kupasuka na kuwa nzito, ndevu zinaweza zikaota, na vilevile vinywele sehemu za siri,
kwapani na pengine kifuani.
Hali ya ngozi inakuwa ikikwaruzakwaruza hasa usoni , na chunusi hujitokeza.
Katika hatua ya mbele mabadiliko yanahusu zaidi viungo vya uzazi vinavyokua na kuanza kazi ambayo
kwa kawaida kwa mvulana itaendelea moja kwa moja, kwa msichana itakoma kati ya miaka 40 na 50.

Msichana vilevile anabadilika ili kujiandaa kuwa mama . Mwili unastawisha maziwa, ukubwa na uzuri wa umbo ,
vinywele sehemu za siri na kwapani,mabadiliko ya rangi ya uso. Hatimaye “anavunja ungo”, yaani anaanza
kutokwa na damu katika tumbo la uzazi.Kwa kawaida itatokea mara moja kwa mwezi , lakini itaweza
ikawahi au kuchelewa kutokana na hali yake ya mwili na ya nafsi (shughuli nyingi, mahangaiko ,
uhamisho n.k.).

Sababu ya damu kutoka ni kwamba,kijiyai kilichokomaa na kutoka nje ya kifuko cha vijiyai kisipopata mbegu ya
mwanamume baada ya siku moja kinaharibika harakaharaka; hapo ngozi nyembamba ya tumbo la uzazi ,iliyotanuka kwa damu ili kupokea na kulisha mimba, inachanikachanika na kutoa damu.mbegu ikikifikia kijiyai, mimba inapatikana na kujishikiza kwenye kuta za tumbo la uzazi ili iendelee kukua; hapo damu haitoki na mama anaweza kujihisi mja mzito.

Mabadiliko ya mwili yanaendana na mengine ya nafsi yanayofanya tabia
iwe tofauti na ile ya awali.

Hisia zinabadilika kadiri mwili unavyozidi kutengeneza chachu ( homoni) zinazomfanya kijana aelekee namna ya baba au mama
.Mvulana anajikuta akivutiwa na uzuri wa wasichana, na kupenda kuwajua zaidi, kuongea nao n.k.Anapenda kuwagombeza na kuwaonea ili aonyeshe uwezo na nguvu alivyonavyo. Katika hatua hiyo anakuwa mvivu na mzito katika kutembea na mara nyingi hajali unadhifu.

msichana anazidi kupenda sifa na kujiremba. Akili pia inapevuka na kumfanya
kijana apende kuwa na maoni maalumu kuhusu mambo mbalimbali, hata kubishana na wengine. Pia
apende mabadiliko, ujuzi mpya n.k. Ndiyo sababu kijana si mwepesi kupokea mashauri na maoni ya
wakubwa, asije akajisikia tena mtoto huku akipenda kutambulika amekuwa
mtu mzima .Kwa ajili hiyo anatamani kufanya yale wanayoyafanya wakubwa. kushirikiana na rika lake na hata kujiunga na makundi
ya wanaomzidi katika shughuli zao (genge , timu n.k.) ingawa pengine hazifai (uhuni , bangi n.k.).Hatimaye kuna mabadiliko upande
wa roho: kati ya mawazo mengine, kijana anajitafutia msimamo mpya kuhusu maswali makuu ya maisha:
anataka kuwa na falsafa na dini yake.

Shida ni kwamba usahihi wa majibu unategemea sana uadilifu wa maisha:kijana akifuata anasa, akili inapofuka na imani inapotea.

Mabadiliko ya viungo vya uzazi Uume wa mvulana unakua,lakini kwa kiasi tofauti kati ya mtu na mtu.

Ni muhimu kila mmoja ajipokee alivyo hata katika kiungo hicho,bila ya kuhangaika wala kuona aibu kwa sababu, eti ni kidogo.
Kusimika kwa uume si jambo jipya kwa kuwa utotoni limeshatokea kawaida kutokana na kibofu kujaa
mkojo.Ila sasa linaweza kutokea kwa sababu mpya, yaani jinsia.

Muundo wa uume ni misuli yenye neva nyingi. Kukiwa na msisimko damu inajaa nafasi zilizomo na kusababisha uume utanuke na kusimama imara na wima.Kusimika kunajitokeza na kupotea haraka kutegemeana na hali
iliyopo.Hali hiyo inaweza kutokea bila ya mtu kutaka, kwa mfano usiku au pia mchana kati ya watu ikimfanya aone haya.
Upande wa maadili tusisababishe hali hiyo bila ya lengo jema,

kama vile kumtibu mgonjwa , kutoa ushauri nasaha au kujielimisha kuhusu jinsia .
Kwa hiyo tukwepe kwa kawaida yale yote yanayoweza kusisimua, kama vile mawazo, maneno, masomo,mitazamo na vitendo mbalimbali kuhusu jinsia. Mvulana anahitaji
kujifunza nidhamu ya namna hiyo.Mashauri mengine ni kutovaa kaptura wala suruali zinazobana,

Mapumbu yanaanza kutengeneza mbegu za kibinadamu kwa wingi
sana: hizo ni ndogondogo na zina umbo kama la viluwiluwi vya chura,yaani vina vichwa na mikia tu.Vichwa ndivyo vinavyoleta viini vya urithi wa baba. Mikia kazi yake ni
kusaidia tu kusukuma mbegu kwa kuogelea ndani ya tumbo la uzazi mpaka zikutane na kijiyai cha mama.
halafu inapotea ndani ya kijiyai.Mbegu zikiwa tayari zinahifadhiwa kwanza katika kifuko cha akiba,karibu na kibofu, zikisubiri msisimko
wa kijinsia ili zitoke kwa njia ya uume na kuanza mashindano ya kutafuta
kijiyai,zikisaidiwa na majimaji
ambayo yanaitwa shahawa na kutengenezwa ndani ya kifuko.Shahawa inafuata mshipa wa mkojo bila ya kuchanganyikana nao.
Shahawa inaweza ikatoka hata nje ya tumbo la uzazi la mke , lililo shabaha yake, kwa kuwa inalenga uzazi hasa.
Inaweza ikatokea k.mf. kutokana na ndoto za usiku, bila ya mtu kukusudia; huyo anaweza akazinduka mara au kutambua asubuhi tu
kilichotokea. Kwa vyovyote
asihangaike kwa kuwa hilo ni jambo la kawaida lililopangwa na Allaah ili
kumsaidia mwanamume asiye na mwenzi.Maana mbegu zake kadiri
zinavyoongezeka katika kifuko cha akiba zinataka kutoka, hivyo zinamuelekeza kwenye matendo ya kijinsia.
Basi, kwa ndoto hizo mbegu zinapungua bila ya dhambi, na vishawishi vinakosa ukali wake. Ni suala la kusubiri tu na kuwa na hakika kwamba havitadumu muda mrefu kwa nguvu ileile.

Upande wa wasichana pia, kuna siku zenye mvuto mkubwa wa kijinsia,
kuhusiana na mabadiliko ya kila mwezi yanayoendana na kijiyai kukomaa; inatosha kusubiri nao utapungua mapema.

Mvulana anapotokwa na shahawa kwa mara ya kwanza ni dalili ya kuwa
si mtoto tena, bali ana uwezo wa kuzaa : kwa hiyo awajibike kama mtu mzima kuhusu uwezo mpya
aliojaliwa. Hasa azingatie kuwa uwezo wake huo bado ni mbichi:ingawa unaweza kusababisha mimba, mimba hiyo itaendelea kwa shida au kufa kabisa.Ubichi wake ni mkubwa zaidi upande wa nafsi, kwa kuwa mvulana hajawa tayari kubeba mzigo wa familia mpya.Ndiyo sababu asichezee uwezo huo,bali ajiandae kuwa baba safi siku za mbele: ajipatie elimu au ufundi fulani, akomae kiutu na kutunza afya yake ya mwili na ya nafsi.Msichana afanye vilevile aweze kuwa mama bora; akijiingiza mapema katika masuala ya ngono,
anahatarisha heshima yake pamoja na afya, kwa kuambukizwa maradhi
yanayoweza yakasababisha utasa au kwa kuzaa kwa shida kabla ya wakati wa kufaa.

Nini ifanywe na mtu aliye katika ubalehe.

Kutojiingiza kwenye masuala ya ngono.

Kutoshirikiana na makundi maovu.
Kuepuka kukaa sehemu za giza na kutokwenda sehemu nyingine hatarishi.

Kuzingatia usafi wa mwili na
mavazi na hasa yale ya ndani Kupata elimu sahihi ya afya ya uzazi kutoka kwa wazazi au watu maalumu kama
ma daktari na wataalamu wengine wa masuala hayo. na kupewa maadili ya Dini.


Jiunge sasa na Chuo chetu kwa njia ya Whatsapp,Kwa Ada ya 2000/Kwa mwezi Upate Elimu ya Tiba Asili.

Wasiliana na Dr.Seifu.dodoma.
0620144253./0769116206.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…