Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,307
- 25,932
Ndugu zangu watanzania, baadhi yetu hawana uelewa wa kutosha wa Bunge Maalum la Katiba litakalojadili na kupitisha Rasimu ya pili ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nikiwa kama mtanzania, msomi wa sheria, nimeona ni bora kudokeza kwa ufupi kuhusu Bunge hili Maalum la Katiba (Constituent Assembly). Nitakuwa, nikisaidiana na mtanzania yeyote mwenye uelewa na jambo hili, ninajibu maswali yatakayojitokeza.
Nafanya hivi nikiamini kuwa ni wakati muafaka kusambaza uelewa juu ya jambo hili kwakuwa nchi yetu inakaribia hatua hiyo muhimu ya kuwa na Bunge Maalum la Katiba katika kuelekea kupata Katiba mpya ya nchi yetu. Napendelea kuleta hoja zangu katika mtindo wa maswali na majibu.
1. Sheria gani inalisimamia Bunge Maalum la Katiba?
Ni Sheria ya Mapitio ya Katiba (Sheria Nambari 8) ya mwaka 2011 ikisomwa pamoja na Marekebisho yake yaliyofanywa kupitia Sheria Nambari 2 ya mwaka 2012.
2. Akina nani watakuwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba?
Kulingana na kifungu cha 22 kifungu kidogo cha (1) aya (a), (b) na (c) cha Sheria Nambari 8 ya 2011, Wajumbe wa Bunge la Katiba watakuwa: Kwanza, Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pili, Wajumbe wote wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.Tatu, wajumbe 166 watakaopatikana kutoka katika Taasisi zisizo za kiserikali, Jumuiya za kidini, vyama vyote vya siasa vilivyosajiliwa, Taasisi za elimu ya juu, shirikisho la wafanyakazi,shirikisho la wakulima,shirikisho la wafugaji, shirikisho la watu wenye mahitaji maalum, na kikundi chochote cha wananchi kinachojulikana kwa jina lolote ambacho kina malengo yanayofanana.
3. Nani anateua/atateua Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba?
Jibu lipo chini ya kifungu cha 22 kifungu kidogo cha (3) cha Sheria Nambari 8. Ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Rais atachapisha majina ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba katika Gazeti la Serikali. Hatahivyo, uteuzi husika, ifahamike mapema na kwa umakini hapa, utawahusu wajumbe 166 tu ambao si Wabunge wala Wawakilishi. Hii ni kwakuwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar wataingia Bunge Maalum la Katiba kama walivyo.
4. Bunge Maalum la Katiba litaoongozwa na Nani?
Bunge Maalum la Katiba litaoongozwa na Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti ambao watachaguliwa kutoka Wajumbe wa Bunge hilo na Wajumbe wenyewe kwa kura za siri. Kama Mwenyekiti atatokea upande mmoja wa Muungano,Makamu wake atatokea upande wa pili. Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, kabla ya kushika ofisi zao, watakula kiapo kitakachoongozwa na Katibu wa Bunge hilo. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 23 cha Sheria Nambari 8 tajwa hapo juu.
Pia, Bunge Maalum la Katiba litakuwa na Katibu na Katibu Msaidizi. Hawa watakuwa ni Katibu wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa sasa pamoja na Katibu wa Baraza la Wawakilishi wa sasa. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 24 cha Sheria tajwa hapo juu.Lakini, kama Mwenyekiti anatokea upande mmoja wa Muungano, Katibu atakuwa ni kutoka upande mwingine. Mfano, Mwenyekiti akitoka Zanzibar, Katibu atakuwa ni Katibu wa sasa wa Bunge la Jamhuri. Katibu na Msaidizi wake wataapa mbele ya Rais kabla ya kuanza kazi zao. Hii pia inatamkwa na kifungu cha 24.
5. Mamlaka ya Bunge Maalum la Katiba yatakuwa/ni yapi?
Mamlaka ya Bunge Maalum la Katiba yanapatikana chini ya kifungu cha 25 cha Sheria Nambari 8 ya 2011. Yatakuwa ni kuunda Ibara za Katiba mpya, kuboresha na kuweka ibara-mvuko za Katiba Mpya kadiri Bunge husika litakavyoona inapasa. Haya yatazingatia Rasimu ya Katiba itakayowasilishwa na Mwenyekiti wa Tume ya Katiba na Kupitishwa na Bunge hilo Maalum la Katiba.
Hapa, Bunge la Katiba litajadili, kurekebisha na kuboresha Rasimu ya Katiba na kuipitisha.
Tuanzie hapa kwa leo.....karibuni