Fahamu kuhusu matumizi ya OverDrive (OD) kwenye gari automatic

Watu wengi wanapenda kuongelea magar waonekane wanayo ila hawajui kitu. Unapata complication kujua maana ya OD? Hivi asume unaendesha gar high then unaamua ku overtake gar ambalo pia lipo speed ila kwa mbali unaona kuna gari linakuja au huoni mbele vizur, ni lazima utataka ku overtake kwa haraka ili uwe salama zaidi. Hapo OD inakusaidiaje? Baada ya ku ingage nguvu ya gar inakuwaje RPM inasomaje? Labda aje mtu ajibu haya maswali

..Mpare wa milimani..
 
Bado hujafafanua....mm nijuavyo ni kuwa od ikiwa off unaendesha hadi speed ya mwisho...yaani kana ni gear tano unamaliza zote. ...ila ikiwa on mwisho gear 3....sasa sijajua madhara ni nini hasa...labda mleta mada afafanue

Umekosea. Kinyume ndio sahihi
 

very wrong
 

Mkuu umejitahidi kufafanua. Tatizo la wa tz wengi ni kwamba huwa tunashindwa kuelekeza hata kama materials tunazo kichwani. Kwa lugha raisin na Kifupi kwa mazingira ya kawaida ukiwa unaendesha gari yako,hakikisha taa ya OD Hawaiwaki. Washa taa ya OD tu(OD OFF) pale tu unapopanda mlima mkali au unapotaka ku overtake kwa kutumia muda mfupi zaidi.Kudos
 
mandella unapaswa uelewe, taa kwenye dashbodi hazipaswi kuwaka. Na ikiwaka yoyote, fanya jambo kutatua ili izime.

Kuhusu OD, RRONDO na Usedcountrynewpipo wameelezea vema sana. Wewe hujui hivyo sikiliza na tekeleza.

Kusema sijui ukiwa wenye jam nini nini huko ni stori zisizo a msingi. Fuata uliyoelekezwa uokoe mafuta na MB zako.

Usizime OD (taa itawaka kukutahadharisha unatesa injini) isipokua mazingira maalumu uliyotajiwa.
 
Last edited by a moderator:

ndugu ww mwenywe ni muulizaji halafu umeeanza kwa kukejeli watu ... gari kwan lazima liwe lako hata la kazini , la ndugu , rafiki ,jirani .. mtu unaweza ukapata chance ya kulitumia vitu ka hivyo no vya kujua .
Halafu kumbuka gari Si Maisha .Hivyo usione ambao hawana basi ndio maisha hawana .

Ww nawe unahitaji kujifunza , sasa ngoja unayoyataka kujibiwa utajobiwa , kejeli pembeni .
 
very wrong

Tatizo kubwa linaloleta mkanganyiko ni;
Lugha, Taa kuwaka pekee bila kuelewa ujumbe uliopo na aina ya magari.....

OD on - Taa inazima huoni kitu kwenye dashboard - mzunguko wa mafuta mkubwa , mwendo mkali, overaking ruksa kwa kuzingatia usalama unaweza weka hata D2. Gari inakuwa mzito na kubalance. SAFARI ZA MASAFA, MBEYA, ARUSHA IRINGA,

OD off kama kwenye picha taa inawaka- Badilisha maelezo yangu ya OD on [Opposite] mizunguko midogo midogo TEGETE, MWENGE, UBUNGO...kwa ujumla ya mjini ILA USIKIMBIZE GARI INAKUWA NYEPESI SANA

SIONGELEI MANNUAL VEHICLES

 
Kuna bwana mmoja anaitwa Mshana Jr; huyu jamaa mzoefu atupe uzoefu pia
 
Kwa ninavyoona od inatakiwa iwe on mda wote kutapunguza ulaji wa mafuta anaebisha afanye kwa vitendo aendeshe gari od ikiwa on na afike hadi speed 60 halafu azime od aone gari inavyokua kua nzito na kupungua mwendo

Mkuu nakubaliana na wewe 100%. Nimekuwa nikiokoa mafuta kwa kiasi kikubwa OD ikiwa ON kuliko ikiwa OFF. Gari inakuwa nyepesi tofauti na wakati OD inapozimwa.
 
Kuna watu wana vichwa vigumu sana. OD ikiwa ON maana yake taa haiwaki kwenye dashboard, gari inatumia gear 1-5/6, hivyo mwendo mkali mafuta kidogo.
OD ikiwa OFF taa itawaka kwenye dashboard itatumia gear kubwa 1-3 hivyo mwendo mdogo mafuta mengi.
Kitu gani kisichoeleweka hapa?
 
Maelezo yako ni mazuri sana mkuu lakini nadhani ungesema unaongelea gari gani kwani magari yote hayana tabia zonazo fanana kuhusu O/D.
 

Nimekukubali mkubwa. Naamini haya ndiyo matumizi sahihi ya hii kitu
 
Ni Shidaa kweli kwa waongoza magari, Yaani unakaa kwenye kiti cha dereva na kuliongoza gari na mnapata shida hivi, je mkipewa magari ya kuendesha mtaweza? Mmezoea kukanyaga break na mguu wa kushoto na mafuta mguu wa kulia?
 
Hapa naona ndugu zangu muwe mnatoa sana haya masomo kuhusu magari na driving kwa ujumla... Maana, ndio maana tunaua magari kabla ya muda wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…