Huu ni uzi wa tatu nausoma humu kuhusu hiyo OD lakini sipati kitu maana naona nachanganywa tu
Hilo somo liendelee tu mkuu maana pamoja na kwamba gari la automatic ni rahisi kuendesha kuna mambo kama hiyo O/D wengi hawaielewi na mbaya zaidi hata mafundi wetu pia kwenye hizi garage zetu kutokana na miaka yote kuwa exposed na gari manualNafikiri hii ni mara ya kumi tunatoa hili some!
Acha kabisa, kote nimeelewa ila hapa kwenye over drive ndo nachanganyikiwa kabisaHili somo la over drive litaeleweka lini?
Mzee tafuta mkalimani. Kulalamika kwamba huelewi hata ufafanuzi wa kitaalam unapotolewa na bado unalalama inaonyesha una elimu ya kiwango cha juu katika Nyanja ya malalamiko. Kama mtu kwenye njaa Amepewa maji, hakutosheka, kapewa chai hakutosheka, kapewa uji bado, kapewa chakula anadai kanywa chai Mara tano hakushiba, je akila nyama na ugali ndio atashiba?Hii ni mara ya tano nasoma kuhusu hii OD na bado hata sijaelewa, naona kuchanganyikiwa tu. Kama kiswahili sijaelewa kingereza itakuaje sasa?
Magari mengi taa ya OD inapaswa kuwaka Kama Ikimaanisha Over drive iko Off
Na iwe Imezima ikamaanisha OverDrive iko On.
Sasa nimegundua wengi wakiona taa inawaka huminya Button ili izime Kumbe ndio wameweka kwnye OD.
Masaiboi umeelewa, ikiwa gali ina zaidi ya mwendo kasi wa 120km kwa Saa, ukitoa overdrive Yaani Ikiwekwa off ingini inalazimishwa kurudi gia ya nyuma yake yaani, lower gears, mfano toka nne itarudi tatu, kwa four speed.Kwa tafsiri rahisi ni kwamba OD ikiwa off gari litakuwa kwny low gear ambayo ni kama 1,2,3 ambayo sio nzuri kama unaendesha zaidi ya 30ml/hr.
OD ikiwa on gari linakuwa na gear zote i.e 1-5 au 1-6 kutegemea muundo, hapo unaweza kwenda speed yyte unayotaka bila hofu ya engine kutumia mafuta mengi.
Taa kuwa on/off inategemea na muundo wa gari na sio gari zote zinafanana.
Ni OD kuwa on mara zote unapoendesha ili hata ukiwa mwendo wa kasi usipate usumbufu wa kubadili kila saa.
Hayo ni maoni yangu
ngoja nicheki mzee ...
ExactlyHebu tulia na usome kwa makini.
Katika hali ya kawaida OD IS ON na gari inatakiwa iendeshwe hivyo(isipokuwa kwenye situation fulani)ndio maana hakuna warning light.
OD ni nini? OD inasaidia gearbox Ku over ride engine maana yake ni kuwa gari Ina engage next gear bila rpm kufika maximum na hii inasaidia kuokoa mafuta. Mfano unaweza kuendesha gari 50kph na ikafika hadi gear namba tano.
Ukizima OD yaani OD OFF umeondoa uuwezo wa gearbox Ku over ride engine kwahio gear haita engage next one mpaka maximum rpm na hoi inakupa more power hence consume more fuel. Ukiweka OD OFF unaweza kupush gear namba mbili tu hadi 60kph wakati OD ON gari st 60kph inakuwa gear namba tano na rpm Kama 1500 hivi.
Kifupi unatakiwa uendeshe gari ikiwa OD ON tu na endesha gari OD OFF kwa waksati maalum mfano Ku overtake au kupanda mlima mkali au drag race.
Exactly
Usahihi ni huu:
Siku zote OD inatakiwa kuwa ON ili kusave fuel consuption.
Hivyo OD ikiwa ON hakuna taa itakayowaka.
Lakini OD ikiwa OFF taa itawaka kukuonyesha au kuku alert kwamba unatumia mafuta mengi.
Taa huwa zinawaka kwa vitu visivyo vya kawaida.
Unaweka OD OFF kwa mazingira maalumu km vile milima mikali, mashimo nk
Ngoja niwachambulie kuhusu taa kuwaka na overdrive yenyewe:
Kuhusu taa:
Taaa yoyote inapowaka wakati engine iko on, humaanisha kuwa kuna hitilafu inabidi irekebishwe. Unapoweka switch on kwenye dashboard, taa mbali mbali huwaka na unapowasha gari, taa zote huzima. Mathalani taa ya airbag ikiwaka au ya betri ikiwaka au ya oili ikiwaka, au ya over drive ikiwaka, inaonesha kuwa eneo hilo linashida na inabidi ufanye kitu ili taa hiyo ijizime.
Kuhusu over drive:
Tuchukue mfumo wa gari ya manual ili kuelezea maana ya over drive. Gari za zamani za manual zilikuaw na gear mwisho nne, lakini kutokana na kukua kwa teknolojia, wakagundua mtoto wa gearbox ambaye uki mu engage, gari inahama kutoka kutumia gearbox ya kawaida kwenye gear namba nne, na kuanza kutumia mtoto wa gear box ambaye kwenye gari ya manula itakuwa gear namba tano hadi sita kwa baadhi ya magari lakini kwenye gari ya automatic unapotumia mtoto wa gearbox ina maana unatumia gear ya over drive!
Kwa hiyo ili engine izunguke kidogo kwenye speed kubwa na ili uweze kuokoa mafuta, kwa gari ya manual utatumia gear namba tano, na kwe gari ya auto utatumia over drive. Kwa hiyo unapozima gear ya over drive, inamaana unaacha kutumia mtoto wa gearbox na hivyo gari itatumia gear kubwa kubwa, na hilo husababisha engine kuzunguka sana na mafuta kwenda kwa wingi. Kwa kifupi unapoendesha gari, taa ya over drive inabidi iwe imezimika wakati wote isipokuwa kwa vipindi maalum ambapo gari itahitaji nguvu ya ziada kama vile kuovertake au kupandisha milima.
Over Drive OD if you turn it on the light will go off.... Kama upo katika mazingira ya kawaida sio highway, hakuna milima, you don't overtake, unaendesha kawaida inatakiwa kuwa taa inawaka ikiwa ina masha kuwa OD off
Taa kuwaka mara nyingi uhashiria kuna taadhari lakini kwa OD ni tofauti. Opposite
nimegundua hili somo nilikubwa watu bado hatujaelewa vizuri .. bado kuna mkanganyiko wa mambo .
Kwa ufahamu wangu OD ikiwa off yaani taa kwenye dashboard inawaka fuel consumption inakuwa low na speed inafika hadi 130 km/h na fuel rotation haipandi kuzidi 3 lakini OD ikiwa ON yaani taa imezima fuel consumption lazima itakuwa kubwa sbb umeweka extra power na hapo speed ni hadi unamaliza dashboard na rotation inafika 5.
USHAURI: usiendeshe gari OD ikiwa ON kwa maeneo ya mjini sbb ni wastage of fuel na kama upo long safar weka OD ON kama una overtake tu na si vinginevyo.