Fahamu kuhusu matumizi ya OverDrive (OD) kwenye gari automatic


MKUU upo kinyume kisheria ya gari wakati inatumika dashboard inatakiwa isiwe na taa hata moja sasa kaangalie vizuri wakati unaendesha ukiona taa ya O/D inawaka angalia Gari itakuwa haimalizi gear lakini ikizima utaona gari ni nyepesi sana chunguza upya mkuu
 
Magari mengi taa ya OD inapaswa kuwaka Kama Ikimaanisha Over drive iko Off, Na iwe Imezima ikamaanisha OverDrive iko On.

Sasa nimegundua wengi wakiona taa inawaka huminya Button ili izime Kumbe ndio wameweka kwnye OD.
MKUU haupo sawa hata kidogo Kwa faida nitakueleza ukipenda ila Kwa hasara endelea kudanganya wana JF ila mi nimeshuka Kwenye gari yako safiri salama
 

Umeeleza vizuri kama unajua lakini umehitimisha Kwa kuonyesha hujui sawali la kujiuliza ni kwamba Gari ya manual ikiwa Kwenye namba tano wakati una overtaking halafu ukaona nguvu za ile gari unalo ovatek zimelingana na ya Gari yako ili uweze kuipita ni lazima utoe 5 uingize gia mamba 4 na hapo utasikia Gari inavuta na kuvuma ila mwendo utaizidi ile unayoiovatek sasa swali kama Gari ni automatic utaifanyaje? Na ikiwa rotation haipandi tena na gari ipo gear namba 5? Ukipata jibu na kuelewa nini nimeuliza utakuwa umekuwa dereva mzuri wa gari zote
 

Rudi kidogo shule MKUU
 
Ukiendesha hakikisha kwenye dashboard hakuna taa yoyote inawaka zaidi ya zile za gearliver tu.

Safi MKUU ww ni Dereva mzuri nashangaa watu wanavyodanganyana hapo inaonekana kabisa wamejifunzia magari ya mjomba
 
Ha ha ha! Hili somo la over drive linaonekana ni gumu sana! Ingekuwa mtihani, wengi mngepata division five!

Hata hiyo division five yenyewe ni wangekuwa wamepewa maana duh!! Wananiuzi kitu mtu hajui lakini anakielezea mpaka shida
 

MKUU umesema kweli kabisa sasa najiuliza hivi hawa wapouoshaji wamesomea wapi na leseni walipataje kweli kama ndiyo hivi naona ndiyo maana kila siku serikali inabaki kusema madereva wote ni wazembe
 
mm kwa hili nakussuport saana . na ndio watu wanabisha .
huwezi zima taa /OD ON ,while gari iko kwnye speed ndogo . .. utawaiweka ON pale tu ambapo Uko kwenye speed saana na ushamaliza Gear Zote kubwa .

Udereva wako na mtoa Uzi pamoja na unaemsuport ni chini ya wastani saana natamani ungekuwa karibu nikupe maelezo ya vitendo ila basi itabidi mwisho kila mtuu atoe namba zake ili mpigiwe kuelimishwa juu ya O/D maana mnatutia madereva aibu sana
 
Ukiendesha hakikisha kwenye dashboard hakuna taa yoyote inawaka zaidi ya zile za gearliver tu.

Sasa mnatuchanganya, huyu anasema off taa nyekundu ikiwaka na mwingine off taa nyekundu ikizima. Sijui yupi sahihi
 
Nilichohundua hapa wote mko sahihi ila ni jinsi ya kueleza tu. Ni kweli kwa kawaida unatakiwa kuendesha gari OD ikiwa ON ina maanisha kwenye dashboard haitaonekana ila ukiweka off ndiyo itaonekana kwa mandishi mekundu. Cha kuzingatia unapoendesha gari hakikisha taa zinazowaka ni za gear tu ukuona nyingine imewaka ujue hauko sahihi.
 

Wewe uko sawa. Wengine wanapotosha au hawajui
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…