Fahamu kuhusu matumizi ya OverDrive (OD) kwenye gari automatic

Ni nzuri zaidi wakati una overtake gari na bahati mbaya kuna gari inakuja mbele yako,ili uweze kuwahi kabla hamjakutana uso kwa uso unatakiwa kutumia O/D,lakini ni vizuri gari yako iwe katika speed kuanzia 80kph na kuendelea.
O/D huwa mda wote kwa gari zilizo nying inakuwa ON ila kui turn OFF ndio optional na yenyewe hutumika zaid unapo kuwa mwendo kasi zaid ya 80kmh hufanya gari kuwa na mwendo na gari kuwa nyepesi lakin stable isiyo kuwa na kelele nyingi pia huruhusu gar kuingage automatic kwenye gia nyepesi kwa haraka hata ukiwa katika mwendo wa wastani. Kifupi ni hivyo.
 
Ni nzuri zaidi wakati una overtake gari na bahati mbaya kuna gari inakuja mbele yako,ili uweze kuwahi kabla hamjakutana uso kwa uso unatakiwa kutumia O/D,lakini ni vizuri gari yako iwe katika speed kuanzia 80kph na kuendelea.

Salama zaidi nikupinguza mwendo nakurudi yuma ya huyo uliyetaka kumpita maana huwezi jua huyo anayekuja mbele yako nayeye yuko kwenye mwendo gani
 
Kwa jinsi ninavyoelewa O/D ni gia ya juu kabisa kwenye automatic cars.

Kwamfano gari nyingi automatic kutoka Japan zinakuwa na gia 4 ikiwemo O/D,

hivyo basi kama O/D itakuwa imezimwa gari lako litakuwa linalazimika kutumia gia 3 tu badala ya 4 ( hii ni kwa magari mengi yanayotoka Japan).

Kwa mantiki hii inashauriwa O/D yako iwe on mda wote ili kuiwezesha kutumia gia zote.

O/D hutumika ku overtake na kwenye mipando hapa unatakiwa kuizima ili gari iweze kushuka Gia
 
OD ni ka gia cha ziada neno over drive maana yake hapo output shaft inazunguka mara nyingi kuliko injini .......OD inapaswa kuwa on ndo mana ukitoa kuna ki taa kitaandika OD off yani inakukumbusha uweke sababu utakuwa unatembelea gia kubwa mfano kwa toyota cami gia ya nne ndo yenye ratio 0.696:1 ndo overdrive so ukitoa overdrive utaishia gia ya tatu tu japo kuwa na yenyew inaweza kukufikisha spid 170+ lakin injin itakuwa inafanya kazi kubwa sana rpm itakuwa juu


vuta picha kwenye ile baskel yako ya gia iwe kuna sehem ukigusa mnyororo hauwezi fika kwenye gia ya mwisho afu uwe mteremkoni huwez kwenda spid mpaka uwe unachochea sana ila ukiweka gia ya mwisho kwa spid ile ile utakuwa unachochea taratibu na bila kuchoka sana vivo hivo kwa gari
 
Naombeni msaada kwenye hili, O/D (over drive)inafanyaje kazi kwenye gari?
Hiyo ninavyo jua mm hutumika sana ktk overtake na mlima mkali kazi yake ni inafanya gear zichelewe kubadilika mfano o/d ikiwa off gear zinabadilika pale mshale wa speed unavyo fika ktk no 2 na ikiwa on o/d gear znabadilika mshale ukifika ktk no 5 na gari inakuwa na power nadhani umenipata
 
Johnkelly kubadilika kwenye no 2 au popote ni kulingana na ulivykanyaga ukikanyaga kidogo car computer au ECU inajua unataka kwenda mdomdo hvo inakupa gia mara kwa mara na ukikanyaga kwa nguvu inaeza shusha gia moja ikijua unaoverteki
 
Dah!!!
 
Johnkelly kubadilika kwenye no 2 au popote ni kulingana na ulivykanyaga ukikanyaga kidogo car computer au ECU inajua unataka kwenda mdomdo hvo inakupa gia mara kwa mara na ukikanyaga kwa nguvu inaeza shusha gia moja ikijua unaoverteki
Hapa ukikanya kidogo haibadiliki n
 
Over Drive... Nachojua mimi ni kwamba kazi yake ni kuipa gari nguvu zaidi ya ile iliyokuwa awali mfano. Unaweza ukawa gia namba 5 ... Ukibonyeza over drive gia itabadilika na kuwa gia namba 4... Ili gari kuipa nguvu tena.... Na ndio maana mngurumo hubadilika... Kwa wale wenye magari yanayoonyesha namba za gia kwa dashboard watanielewa zaidi....
 
OD ni kwa ajili ya milima mikali Kazima D uiongezee na OD kama mlima mkali saaana unaweza ukatumia D 2 mchanga matope tumia L
D2 - ni kwa ajili ya gia kama 3 au 4.... Lengo la D2 ni kufanya gari iwe inacheza kati gia hizo na mara nyingi hutumika katika safari ndefu ..... Yaaani zile safari za kufunguka ambao gia namba 1 au 2 ni nadra kutumia.

L - lower gear mara nyingi hutumika kufunga au kulook gia namba 1. Hutumika katika kupanda vilima vikali na visumbufu au sehemu korofi ambapo gia hii huwa na nguvu kuliko gia nyinginezo pia hutumika katika kuchuka vilima vikali... Inadaidia brake pad zisipate joto haraka. Na kwa maana hiyo. Engine haiwezi kuchanga mwendo au kuongeza mwendo wakati gari linachuka. Mwendo wake unakuwa kama umefungwa au kubanwa.

Kama huamini Google kwa kina
 
Iko hivi.... Gari hizi automatic huwa zina gear /gia 4. Mara zote unapoendesha overdrive inakuwa on hivyo gari inabadili yenyewe gia toka moja hadi nne kadri unavyokanyaga. Sasa mtu akisema ameweka overdrive kwa lugha za mtaani kiuhalisia ni kwamba amezima /off overdrive. Hapo gari haitaweza kuhama gear kwenda hadi nne. Hivyo inakuwa na nguvu zaidi kama unavyojua ukipangua gia kutoka ya juu kurudi chini gari inaongezeka nguvu. Ndivyo inavyokuwa lakini haishauriwi kutembelea overdrive ikiwa off kwa mwendo mrefu kwa sababu za matumizi ya mafuta na performance ya gari kwa ujumla.
 
Kwa kiswahili chepesi ninavyoelewa over-drive ni gear no tano katika gari za automatic na inafanya Kazi kuanzia kwenye speed 65-80
Ukisema gia namba 5 unakosea nyingi ya hizi gari ni 1-4 tu kwa automatic. Sema unapokuwa kwa gia namba 4.... Ukibongeza kitufe ndani... Gia itabadilika na kuwa gia namba 3... Kusudi ni kuleta nguvu katika gari... Na ndio maana hata mngurumo unazidi...
 
Ni nzuri zaidi wakati una overtake gari na bahati mbaya kuna gari inakuja mbele yako,ili uweze kuwahi kabla hamjakutana uso kwa uso unatakiwa kutumia O/D,lakini ni vizuri gari yako iwe katika speed kuanzia 80kph na kuendelea.
acha kuwaingiza chaka watu...hapo hatubonyezi OD..kama unaovatake mliman ukitaka upite kwa kasi unaweka D2 hapo gari unaipa nguvu ya kupangua gia kwa kasi kurud mbili then iende 3..hapo kwa gari zingine zina botton ya power na eject huwa tunabonyeza hizo gari inakuwa kama ndege mliman...
overdrive kiutaratibu inatakiwa iwe on muda wote thats why ukizima OD dashboard inaku notice kwamba iko off...
 
uko chaka ndugu..tulia tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…