Ipo hivi, unapoendesha gari yako, kama upo speed chini ya 60km/h, then usihangaike kuweka overdrive, na utajua overdrive ipo off kama pale kwenye dashboard itaonyesha kataa kale kalikoandikwa OD/OFF.
Ila ukiwa upo barabara mnyooko na hakuna foleni wala traffic wa speed limit, then ichochee gari mshale wa speed ukishafika mitaa ya 60km/h pale then bonyeza kale kabatani ka Overdrive na kale kataa katazima pale kwenye dashboard then utasikilizia utamu namna gari itakuwa nyepesi kama ndege.....
Pia mfano unasafiri na unataka kuovertake labda lorry au bus..... Then hakikisha usalama kuwa unaona mbele kupo clear hakuna gari inayokuja then achia pedal kidogo kuwe na nafasi kati yako na gari unayotaka kuiovertake then kanyaga uichochee gari hadi ifike speed ya 60km /hr kisha papo hapo bonyeza Overdrive kuiwasha then endelea kuchochea ili gari izidi kuchapa lami kwa kasi. Na unaweza kutambaa nayo hadi pale utapoona unataka kutembea speed ndogo then unaitoa......