Fahamu kuhusu Munanka Road iliyopo huko Bunju

Fahamu kuhusu Munanka Road iliyopo huko Bunju

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
MUNANKA ROAD BUNJU
Nimeuona mtaa huo hapo chini wa Munanka Bunju.

Naingia Maktaba kumtafuta Bhoke Munanka.

Bhoke Munanka nimekutananae wakati natafiti maisha ya Ali Migeyo.

Katika kitabu cha Abdul Sykes kwa mara ya kwanza namtaja Bhoke Munanka kana hivyo hapo chini:

Katika majimbo ya ziwa katika miaka ya 1950 Tawi la TAA lililokuwa na nguvu lilikuwa tawi la Mwanza.

Viongozi wake, Saadan Abdu Kandoro, Mmanyema na mtunga mashairi, na Bhoke Munanka walikuwa wakitupiwa macho na serikali.

Kandoro na Munanka walikuwa wakijaribu kumuunga mkono Ali Migeyo ambaye peke yake alikuwa akijaribu kufungua matawi ya TAA sehemu za Bukoba.

Hii ilikuwa mwaka wa 1953.

Tawi la chama cha TAA la Tabora lilichukua changamoto hiyo kwa kupitia juhudi za Kandoro aliyeuona mgogoro wa ardhi ya Wameru kama jukumu lake binafsi.
Kandoro aliitisha mkutano wa matawi ya TAA ya Mwanza, Kigoma na Tabora kujadili suala hilo.

Mwanza iliwakilishwa na Bhoke Munanka, Mzee Mkama Mlaji na Mohamed Kihaka Kitenge; kutoka Kigoma mjumbe aliyekuja alikuwa Jumanne Mawimbi na Tabora iliwakilishwa na Sheikh Kinana, Kandoro na George Magembe kama rais wa TAA tawi la Tabora.

Mkutano wa Tabora uliahidi mshikamano wa pamoja na watu wa Meru katika mapambano dhidi ya walowezi.

Hii ilikuwa mwaka wa 1952/53 wakati wa Mgogoro wa Ardhi ya Wameru.

Mnamo tarehe 12 Novemba, Ally Sykes alimwandikia barua Kenneth Kaunda akimthibitishia kushiriki kwa TAGSA na TAA kwenye mkutano huo. Dennis Phombeah na Bhoke Munanka, katibu wa TAA Jimbo la Ziwa walikuwa ndio wawakilishi wa TAA.

Mnamo tarehe 1 Desemba, Alexander Tobias alimwandikia barua Kamishina wa Kazi, Bennet akimuombea ruhusa Ally Sykes ahudhurie mkutano huo wa Lusaka.
Munanka alinyimwa pasi ya kusafiria na serikali kwa hivyo hakuweza kusafiri.

Hii ilikuwa mwaka wa 1953.

Wajumbe walipiga makelele, wakagonga meza kwa hasira, wengine wakawa wanaburuza meza na viti kwa fujo kudhihirisha hamaki zao.

Jumanne Abdallah, aliyekuwa akifahamika kwa umaarufu wa kuwa Kadiani na Bhoke Munanka kutoka Jimbo la Ziwa walisimama na kumlani Sheikh Rashid Sembe wakimwita msaliti.

Baada ya kurejea kutoka Tabora, Sheikh Suleiman Takadir, Bibi Titi Mohamed, Elias Kassenge na Bhoke Munanka walifuatana na Nyerere kwenye ziara ya Jimbo la Mashariki kuwaeleza watu umuhimu na maana halisi ya uchaguzi uliokuwa mbele yao.

Nyerere aliwafafanulia watu kile ambacho Waafrika wangepoteza endapo TANU ingesusia uchaguzi. Lakini Sheikh Takadir alikuwa akishiriki katika mikutano ile kimwili tu; moyo na fikra zake havikuwa pale.

Alikuwa na wasiwasi jinsi matukio yalivyokuwa yakitokea katika TANU na namna siasa ilivyokuwa ikichukua mwelekeo mpya.

Sembe alishikilia msimamo wake kuwa TANU ni lazima iingie uchaguzi unaokuja ili ishinde uchaguzi na katika ushindi huo iwe na uwezo wa kufutilia mbali mfumo huo wa kuchukiza.

Nyerere alisimama na akamuunga mkono Sembe.

Hii ilikuwa kwenye Mkutano wa TANU wa mwaka wa 1958 Tabora kujadili Kura Tatu.

Baada ya kurejea kutoka Tabora, Sheikh Suleiman Takadir, Bibi Titi Mohamed, Elias Kassenge na Bhoke Munanka walifuatana na Nyerere kwenye ziara ya Jimbo la Mashariki kuwaeleza watu umuhimu na maana halisi ya uchaguzi uliokuwa mbele yao.

Nyerere aliwafafanulia watu kile ambacho Waafrika wangepoteza endapo TANU ingesusia uchaguzi.
Lakini Sheikh Takadir alikuwa akishiriki katika mikutano ile kimwili tu; moyo na fikra zake havikuwa pale.

Alikuwa na wasiwasi jinsi matukio yalivyokuwa yakitokea katika TANU na namna siasa ilivyokuwa ikichukua mwelekeo mpya.
Ilikuwa katika ya mazingira ya namna hii na uhusiano mzuri kati ya TANU na KANU ndiyo Nyerere alisafiri kwenda Nairobi kukutana na Tom Mboya.

Uamuzi ulitolewa kuunda umoja ili kuunganisha vyama vyote vya kupigania uhuru katika Afrika ya Mashariki - Pan-African Movement of East Africa (PAFMECA).

Chama hiki kiliundwa rasmi mjini Mwanza na wawakilishi wa vyama vya kizalendo kutoka Tanganyika, Zanzibar, Kenya, Uganda na Nyasaland mnamo tarehe 17 Septemba, 1958.

Tanganyika ilipewa heshima hiyo kwa sababu chama chake cha kizalendo, TANU kilikuwa ndicho chama kilichokuwa kikiendeshwa kwa ufanisi zaidi na chenye nguvu sana kuliko vyama vyote katika kanda ile.

TANU ilikuwa imeweza kujenga amani na umoja katika chama.
Mizozo ndani ya chama haikuwepo.

TANU kilikuwa chama cha siasa cha kupigiwa mfano katika Afrika.

Bhoke Munanka alichaguliwa rasmi kuongoza ofisi ya PAFMECA katika makao makuu ya TANU. Ilikuwa wakati wa mkutano wa PAFMECA uliofanyika Mwanza ndipo TANU Youth League ya Tabora iliamua kuwapa wakazi wa Tabora kitu ambacho kitadumu ndani ya fikra na kumbukumbu zao kwa miaka mingi.


 
Back
Top Bottom