Offshore Seamen
JF-Expert Member
- Mar 9, 2018
- 5,489
- 14,091
Sport Fishing ni Uvuvi wa Samaki katika bahari, Maji ya ziwa, bwawa au mto Kwa ajili ya kujifurahisha, burudani au Mashindano. Hii ni aina tofauti na Uvuvi wa Samaki wa biashara na kujikimu, huu ni rahisi Sana mtu anayevua anaweza akawa kwenye Boti ndogo au pembezoni mwa bahari/Ziwa/bwawa/mto.
Mvuvi hutumia zana za kawaida kama fimbo yenye mshipi(rod and reel), ndoano, chambo (baits), mkuki wa kuvulia au mtego mdogo wa uvuvi.
Pichani ni Rod and Reel(Hiyo fimbo na mashine ya kusogezea mshipi au Kamba ya ndoano, na artificial baits (chambo za plastic)
Sport Fishing unapofanya lazima uwe na kibali na kinatolewa na wizara ya Uvuvi pia Kuna Sheria zake na maeneo ambayo unaruhusiwa iwe baharini au ziwani.
Baadhi ya mataifa makubwa Duniani kila mwaka hufanya Mashindano ya uvuvi na Kuna chombo kinachosimamia na kutoa tuzo pia kutunza rekodi ambacho kinaitwa International Game Fish Association (IGFA). Hawa pia wanashirikiana na Serikali na Mamlaka mbalimbali Duniani kulinda na kutunza mazingira na viumbe wa majini.
Sport Fishing ni zaidi ya utalii na haina madhara kwa Samaki au mazingira ya Bahari au Ziwa. Mtu hata akimvua Samaki mdogo anaruhusiwa kumrudisha Tena na Sasa Kuna vifaa vya kisasa pia Sheria na kibali kinamkataza mtu kuondoka na baadhi ya Samaki kama wametunzwa Kwa kazi maalumu.
Kwa Sheria ya uvuvi ya Tanzania ya mwaka 2003, Sport Fishing naona imeongelewa kidogo sana kwenye page ya 22 kifungu (t) kwenye Mamlaka ya Director of Fisheries vitu anavyoweza kuzuia visifanyike kama vinahatarisha uvuvi.
Kama Sheria itaboreshwa itaruhusu utalii wa Sport Fishing kufanyika maeneo mengi na kutoa fursa kwa watu wengi.