Fahamu kwa nini mchezaji Said Mwamba aliitwa “ Kizota

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
18,037
Reaction score
33,681






Said Mwamba a.k.a Kizota alikuwa ni mchezaji mahiri kwa klabu ya Dar Es salaam Young Africans na timu ya taifa ya Tanzania. Watu wengi hawafahamu kwa nini mchezaji huyu aliitwa ' Kizota '.

Kizota ni jina la ukumbi wa mikutano ya Chama Cha Mapinduzi uliopo mjini Dodoma.
Vikao na mikutano mingi inayo fanyika katika ukumbi wa Kizota huwa ina ongozwa na Mwenyekiti wa Chama.
Kama hiyo haitoshi, vikao hivyo vilikuwa vinaongozwa kwa mujibu wa falsafa ya " Zidumu Fikra Sahihi za Mwenyekiti wa Chama ".
Hivyo basi kila mara mwenye kiti wa chama alipokuwa alipokuwa akitoa hoja, katibu wa kikao alikuwa akiwauliza wanachama " KUNA SWALI HAKUNA SWALI" ., wananchi waliitikia " HAKUNA SWALI !"
Back To Said Mwamba Kizota.
Said Mwamba alisajiliwa na Yanga mwaka 1986. Mechi yake ya kwanza ilikuwa ni dhidi ya CDA ya Dodoma na ilichezwa katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Unaambiwa siku hiyo mpira ulimkubali kweli Kizota. Basi jamaa alikuwa kila akifanya tukio uwanjani, shabiki mmoja anawauliza wenzake " JAMANI KUNA MWENYE SWALI"..Watu nao walijibu " HAKUNA SWALI"
Kwa mfano, kuna ngoma moja, jamaa alichukua boli, akaweka gambani, akatuliza chini, akafanya mipango, adui akaja, akapigwa kanzu halafu ngoma ikaoshwa mbele.
Mashabiki wa upande mmoja wakawauliza wenzao " KUNA MWENYE S WALI " wenzao wakajibu ' HAKUNAAA"
BASI KUANZIA SIKU, HIYO SAID MWAMBA, AKAWA ANAITWA " KIZOTA !"
 
Kipindi hicho huku uswahili tunakokula miguu ya kuku, vichwa, utumbo, ngozi, vibawa na kitu cha mwisho ni "kizota" au "kikundu" hii ni sehemu ambayo kuku hutolea haja. Asikwambie mtu ktk vitu vyote hivyo nilichokipenda zaidi ni "kizota" aka kikundu!
 
Kipindi hicho huku uswahili tunakokula miguu ya kuku, vichwa, utumbo, ngozi, vibawa na kitu cha mwisho ni "kizota" au "kikundu" hii ni sehemu ambayo kuku hutolea haja. Asikwambie mtu ktk vitu vyote hivyo nilichokipenda zaidi ni "kizota" aka kikundu!
sisi temeke mikoroshini pale karibu na stereo bar kuna mzee mmoja alikuwa anaviuza ila tulikuwa tunaviita''vishitobe''
 
WE acha Kupiga watu FIX

KM HUJUI TU,WAKATI SAIDI MWAMBA KIZOTA ANAANZA KUCHIPUKIA NA KUCHEZA SOKA KWA MAFANIKIO

MPK ANA STAHAFU MPIRA HUO UKUMBI UNAO USEMA WW LILIKUA GHALA(bohari)

lilikua halina uhusiano wwte na chama cha mapinduzi.

Lilikua linamilikiwa na FAO,kuifadhia magunia ya mahindi.

Mwaka 2005 FAO wali wauzia chama cha mapinduzi mkoa wa dodoma, na ndipo CCM walipolichukua lile jengo na kuanza kulitumia.

Jengo ilo liko nje kidogo ya mji wa dodoma, karibu kabisa na Kiwanda cha taifa cha nyama TMC na Bohari ya Taifa ya Dawa MSD.

Eneo ilo linafahamika km Nkuhungu Magharibi linalopatikana ktk KATA ya KIZOTA.
(Kuna kata kubwa inayoitwa kizota)

so hakuna uhusiano wwote
wa Jina la saidi mwamba Kizota.
Kwa sbb wakati yy anacheza mpira, CCM walikua wanatumia ukumbi wa Chimwaga kufanyia Mikutano na Vikao vyao

kabla ya kulikabidhisha kwa Chuo kikuu cha Dodoma mwaka 2007
 
sawa balozi, ila kizota jamaa alikuwa mtu mwnye vtu adimu, kama vile faulo hambazo marefarii walikuwa hawazioni.
nakumbuka kuna game moja ilpigwa shamba la bibi kipindi hicho, nikiwa ball boy, kizota aliruka na mtu juu, kugombea mpira, kurudi yule mchezaji alikuwa anagaa gaa chini kwa maumivu.
refa hakuona, ila mm kwa vile kpnd hcho tulikuwa tunakaa karbu na uwanja, niliona nn alichomtenda jamaa.
kizota alikuwa mtu wa kazi!
 

1. Malota Soma huyu sijui alikua anaitwa (Ball juggler?)
2. Khamis Thobias (Gagarino)
3. Zamoyoni Mogela (Golden Boy)
4. Sanifu Lazaro (Tingisha)

Hawa nao unaweza kutujuza majina yao waliyapataje? Shukran mkuu LIKUD na wengine mtakaochangia.
 
Last edited by a moderator:
Steven Nemesi yupo? Keneth Mkapa? Edibil Jonath Lunyamila,Hussein Masha? Juma Pondamali? Sahau Kambi?
 
1. Malota Soma huyu sijui alikua anaitwa (Ball juggler?)
2. Khamis Thobias (Gagarino)
3. Zamoyoni Mogela (Golden Boy)
4. Sanifu Lazaro (Tingisha)

Hawa nao unaweza kutujuza majina yao waliyapataje? Shukran mkuu LIKUD na wengine mtakaochangia.

Umemsahau Abubakar Salum "Sure Boy" wa Yanga aliyesawazisha magoli mawili dhidi ya El Mereikh ya Sudan mpaka akazawadiwa....
 

Mkuu yuko sahihi, kulikuwa na mkutano wa Kizota mwaka 1987 ambapo Nyerere aliwachachafya wajumbe kama Said Mwamba alivyokuwa anawachachafya mabeki wa Simba n.k.; alikuwa anawapiga chenga na kuwasubiri kama wana jibu, rejea:

"These were prominent themes in his speech at the October 1987 party conference at Kizota" - Changing the Rules: The Politics of Liberalization and the Urban Informal ... - Aili Mari Tripp - Google Books
 

Nadhani Balozi wa Dodoma alipitiwa kidogo.
 
Last edited by a moderator:
Umekosea kidogo.......

Nyerere: Kuna Mwenye swali?

Wana CCM: Hakuna swali.

Nyerere: Kawawa funika kikombe...................

Usijali, nilikuwa nakuchemsha tu... Story yako juu ya Homeboy Mwamba ni ya kweli. RIP Said Mwamba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…