Fahamu kwa nini mchezaji Said Mwamba aliitwa “ Kizota

Kuna game moja dhidi ya Simba pale taifa,Kizota aliteswa mbaya na jamaa mmoja Deo Njohore,dogo deo kipindi hicho full ball controll,akili,kujiamini,mwisho wa game yanga alipoteza kwa goli 1,Kuhusu kizota alikuwa anajua,vitu vyote alivyotakiwa navyo mshambuji alikuwa navyo. lakini mwishoni hapa alipoteza dira,mitungi sana.....daa alikufa akiwa masikini kama wachezaji wengi wa Tanzania...alale anapostahili.
 
Dah umenikumbusha mbali sana,huyu jamaa alikuwa jembe,maana ni wachezaji wachache sana waliojaliwa kuwa washambuliaji wazuri na pia mabeki waukweli kabisa,jamaa kwa Viwiko au Vipepsi alikuwa ni noma mpaka ikafika kipindi wachezaji wa Team pinzani hawaruki nae hewani maana hautarudi chini salama. R.I.P jembe maana nikikumbuka siku ile jioni unafariki pale Tazara Vetinary kwenye ile Shell ya Oil Com ulipokuwa unatoka Uwanja wa Taifa kucheki Game ya Taifa Stars,mpaka leo napata huzuni kubwa sana maana ulikanywaga na lile Lory pale Shell katika mazingira tatanishi sana mpaka watu wakahisi labda ndio kafara za mwenye Shell maana ndio kwanza ilikuwa imefunguliwa.
 
1. Malota Soma huyu sijui alikua anaitwa (Ball juggler?) 2. Khamis Thobias (Gagarino) 3. Zamoyoni Mogela (Golden Boy) 4. Sanifu Lazaro (Tingisha) Hawa nao unaweza kutujuza majina yao waliyapataje? Shukran mkuu LIKUD na wengine mtakaochangia.

1. Malota Soma huyu sijui alikua anaitwa (Ball juggler?) Fundi huyu kutoka Morogoro! Huyu alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kuuchezea mpira kwa mbwembwe yeye mwenyewe na huku wachezaji wa timu pinzani wakiwa hawana cha kumfanya wakati wote wa mbwembwe zake, labda wamchezee rafu, kwa kifupi alikuwa na vitu mchanganyiko wa ZIDANE na GAUCHO (Juggle ni ule mchezo wa kurusha vitu vi3 juu afu unavichezea bila hata ki1 kudondoka chini, kuna mtangazaji wa RTD ndiye alimpachika hili jina MALOTA SOMA)!

2. Khamis Thobias
(Gagarino) Huyu nae ni alikuwa fundi kutoka Morogoro - RIP! Gagarino lilitokana na jina la ku-copy katika majina ya wachezaji wa Brazil

3. Zamoyoni Mogela (Golden Boy) Mwingine nae kutoka Morogoro, mkazi wa kinondoni mkwajuni kwa sasa! huyu alikuwa mfungaji mzuri sana enzi zakee! alitwaa ufungaji bora maranyingi sana, ktk soka mfungaji bora imezoeleka kupewa VIATU, huwa vinaitwa GOLDEN BOOTS, hapa ndio jamaa wakamuita GOLDEN BOY, ni kama alishazoea aina hii ya tuzo!

4. Sanifu Lazaro (Tingisha) Huyu nae alikuwa mfungaji hodari sana kwa YANGA na timu ya taifa! Sanifu aliitwa TINGISHA wakimaanisha wakati wwt wa mchezo alikuwa na guarantee ya kutingisha nyavu!
 
Mbona nilisikia jina lake linatokana na manaburi yaliopo kizota Dodoma makaburi hayo yanasemekana ni mengi sana na yamekaribiana sana sasa kipindi hucho naye Kizota alikuwa anapiga chenga za hapa na pale za karibu kama makaburi ya kizito.

Hivyo nakumbuka nikiwa darasa la tatu nikiwa kwenye alaki ya ccm kutimiza miaka 10 mjini dodoma kipindi hicho na miaka 10 ya kuzaliwa nikisomacshulevya msingi kiwanja cha ndege.
 
Ikumbukwe pia Malota Soma (Ball Jugler) alikuwa ba staili ya ufungaji wa mabao alikuwa mahiri kufunga magoli kwa kichwa, kifua, tumbo ------ ------, kwa goti na nk. ndiyo maana alivuma sana enzi hizo.
 
Kaka kunywa Kilimanjaro mbili nitalipa
 
Kizota alikuwa noma sana..Alikuwa na kila kitu kama Pele vile
 
Kipindi hicho huku uswahili tunakokula miguu ya kuku, vichwa, utumbo, ngozi, vibawa na kitu cha mwisho ni "kizota" au "kikundu" hii ni sehemu ambayo kuku hutolea haja. Asikwambie mtu ktk vitu vyote hivyo nilichokipenda zaidi ni "kizota" aka kikundu!

Tanga twakiita “SUDI” !![emoji2][emoji2] kikund* chakuku mimi kilinishinda kula hadi sasa sikiwezi kabisa[emoji23][emoji23]
 
Msiba wa Kizota ulisikitisha watu wengi sana.Inasemekana alikuwa amelewa sana
 
Umenikumbusha mbali sana soka la zamani llilikuwa na watu wenye vipaji sana
 
Naikumbuka hiyo game..Nadhani Njohole alikuwa MTU wa Pili aliefanikiwa kumdhibiti Kizota ..Beki wa kwanza alikuwa Bakari Malima Jembe Ulaya wakati huo akichezea Pan na hiyo ndo ikawa sababu ya Dar Young Africans kumsign Malima
 
Miongoni mwa wachezaji ambao sitawasahau na alinichefua kwel ni mcjezaji anaitwa JUMA MHINA,

Hyu kwa wasiomfaham alikuwa golikipa wa wana tp lindanda, PAMBA YA MWANZA, Tim ambayo nliipenda sana,

Hii ilikuwa fainal ya kombe la jamhuri uwanja wa ccm kirumba-mwanza, mtangazaji ni dominich kirambo, radio ni RTD, MUDA saa 10 jion.. Mwaka 1989

Aseee juma mhina nasikia aliuza match hyo pamba ikapigwa 1 tena la penati, yaan alidaka mpira halafu akamfuata mchezaji wa malindi akamkanyaga kwa makusudi..

Asee hyo match sitaisaha, nakumbuka wachezaji wenzake, akina david mwakalebera, husen masha, JM(george masatu)
Abdalah bori, mao mkami, na wengine, timu ilikamilika..

Ila jamaa walikuwa wameloga balaa wakamnunua kipa, mhina baada ya machi akakimbilia kenya..


Leo nliposikia interview yake nikatamani kumuuliza unajisikiaje kuisaliti tim ya pamba? Leo hii pamba isingekuwa hapo, na baada ya match hyo pamba haijawahi kuwa na matokeo mazur...

Ila kwa vijana hawajui tu kuwa Tp lindanda, ndo tim yenye record ya kuifunga magori 19kwa ujumla, kwenye kombe la mabingwa afrika...

Leo pamba nikiiwaza tu namkumbuka hyo jamaa anaitwa mhina, kiukwel wanaomjua mwambien aliizamisha yanga...

N.b kama kunalichochanga wadau watarekibisha, bt story ipo hvyo.....
 
Pamba ya Mwanza walitisha sana enzi zao..Akina Abdallah Boli, Alphonce Modest, Nicco Bambaga, Fumo Felician, Kitwana Suleiman..Walikuwa shida wale jamaa nakimbuka miaka ya 95 tunapiga chandimu mwembeyanga wapinzani wetu wanajisifu " Tunagonga touch la mapamba "
 
Ila hyo jamaa aliniboa sana, nataman siku nikutane nae nimuulie kwa nn alifanya hvyo?
 
Tupe na story ya sande manala computer kuua mtu hapo jamhuri morogoro wahenga noma
 
Hii chai yake hata Mimi ilinipalia kuinywa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…