tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,225
- 22,632

"Ushauri wangu kwa wanawake na wanaume ni kuacha nafasi kubwa katika maeneo nyeti. Hakikisha suruali na nguo ya ndani vinapata nafasi na wala usibanwe kwa namna yeyote," Kauli ya wataalamu.
Wana MMU, ni mwaka wa 5 sasa tangu niache rasmi kuvaa vazi la chupi. Zoezi hili nililianza taratibu lakini kadri siku zilipokwenda nikaona ni utaratibu wa kawaida.
Zamani nilikuwa nikivaa chupi mchana lakini wakati naenda kulala usiku, nilikuwa nikivua chupi na kuvaa bukta. Lengo langu kubwa lilikuwa kuziacha nyeti zangu ziwe free na kupata fresh air kwani mchana kutwa zilikuwa zikishinda zimebanwa na chupi!
Baadaye nilikuja kusoma makala moja ya Afya iliyodai kwamba kubana nyeti kwa chupi ni hatari kiafya kwa kuwa hupunguza uwezo wa kuperform kitandani--performance kwa maana quality and quantity of sperms produced (sperm count)--kitendo ambacho kinaweza kupelekea mtu kuwa mgumba.
USHAURI
Ushauri wangu kwa wadau wa MMU naomba muige mfano wangu huu kwani umenipa mafanikio makubwa sana. Baada ya kuacha kutinga kyupi perfomance yangu kitandani imeongezeka mara dufu. Hasa akina SHE nawashauri muige mfano huu kwani nyie ndio mnaovaa tamang'eo zinazobana sana hadi papuchi zenu kushindwa 'kupumua'.
Kwa taarifa zaidi, SOMA HAPA
Nawasilisha