Fahamu madhumuni ya kutangaza biashara

Fahamu madhumuni ya kutangaza biashara

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
20210119_143614_0000.png


Kutangaza biashara ni kitendo cha kuvuta umakini wa umma kwenye biashara kwa lengo la kuuza bidhaa au huduma kwa kutumia njia mbalimbali kama magazeti, mitandao ya kijamii na mbao za matangazo.

Madhumuni ya kutangaza biashara ni kama yafuatayo:-

Kukuza mauzo,
Dhumuni kuu la biashara ni kutengeneza faida, na jinsi mauzo yanavyopanda ndivyo faida zaidi hupatikana. Hii ni kwa sababu kanuni za biashara zinasema kuwa mauzo yakiongezeka gharama za uzalishaji hupungua.

Kutangaza bidhaa mpya, Bidhaa mpya inatakiwa kutengenezewa umaarufu ili iweze kupata soko. Kwahiyo kuitangaza ni njia muhimu ya kuitengenezea umaarufu.

Kutoa taarifa juu ya mabadiliko ya bidhaa, Matangazo yanaweza kutengenezwa katika njia ya kutoa taarifa kwa wateja juu mabadiliko ya bidhaa fulani. Kunaweza kuwa na namna mpya ya matumizi ya bidhaa ambayo ni muhimu kuitangaza.

Kumfanya mteja kuchukua hatua zaidi, Hatua kama kuulizia taarifa kama vile, mfano wa bidhaa, mahali zinapipatikana, namna ya kuagiza na namna ya kuzipata.

Kuwashawishi wateja wako kuwa bidhaa au huduma yako ni sahihi kwa mahitaji yao.
 
Upvote 3
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom