Ben Zen Tarot
JF-Expert Member
- Dec 13, 2014
- 4,298
- 7,612
Kampuni ya Toyota ilianzishwa na mtu anayeitwa toyoda na si Toyota kama wengi wanavyofikiria . mwanzo ilikuwa ikijulikana kwa jina la katakana . kampuni ya Toyota ni ya mtu na famila yake.
katika ukuaji wa biashara , katakana co.ltd , ilibadilishwa. Dhumuni kubwa lilikuwa kushindana katika soko la biashara ya magari nje ya nchi.
Kimaandishi kwa kijapani TOYODA , inatumia alfabeti 10 . TOYOTA inatumia alfabeti 8 . kwa mujibu wa wajapani namba 8 ni namba ya bahati , ikampendeza mr. toyoda kuita kampuni Toyota.
Katika logo ya TOYOTA kuna ubunifu , siri na maana kubwa . logo ya Toyota ambayo imechorwa kama zero na michoro ndani yake . kuna “T” iliyojificha , ikimaanisha herufi ya kwanza ya Toyota. Kuna maneno yote sita kwa alfabeti yaliyojificha yakimaanisha neno Toyota.
Maana halisi ya logo hiyo , iliyoanzishwa tangu mwaka 1990 katika muundo wa overlapping ellipses logo , inamaanisha muunganiko wa moyo wa mteja na moyo wa bidhaa za Toyota.
Majina mengi ya Toyota model , yalianzishwa na maana zake kwa sisi watu wa kiroho kila gari , muundaji alilinenea jambo na hayo lazima yataambatana na gari husika. Unaweza kuchagua kwa ubora na matumizi yako pia . kuna majina kama haya ya Toyota mfano.
TOYOTA RAV4 - ni kifupi cha maneno recreational active vehicles with 4wd . yaani ni magari ya mapumziko hasa Kama unaenda kupumzika sehemu za pembezoni mwa mji , zisizo na barabara bora ( outdoors recreation activities ). Waliziweka katika kundi la SUV cars ( sport utility vehicles).
TOYOTA HILUX – mkusanyiko wa maneno high na luxury. kiingereza
TOYOTA CARINA – ni mkusanyiko wa nyota kijapani.
TOYOTA HIACE – ikimaanisha TOYOACE na wakaweka HI (high) , ikiashiria kuwa imepita matoleo yote ya “ACE” ambayo yalikuwa magari kwa ajili ya kubeba wafanyakazi .
TOYOTA LAND CRUISER – neno la kijapani lilitolewa likimaanisha kwenda popote, neno la kizungu likauzika zaidi na kuita land cruiser.
TOYOTA SIENNA - jina hili lilitolewa kwa heshima ya mji wa sienna italia.
TOYOTA ALTEZA – Kwa maana ya neno la kiitaliano likimaanisha heshima na urefu wa kitu.
TOYOTA VEROSSA – limepewa kutokana na neno la kiitaliano VERO( ukweli), na ROSSO (nyekundu).
TOYOTA KLUGER – imetokana na neno la kijerumani , kisifa (adjectives) , ikimaanisha “KLUG” , ikimaanisha busara au nzuri. Kuna kuger l na v . l =liberty na v= victory .
TOYOTA VANGUARD –ni neno lililomaanisha kwa wajapani , wale waliombele katika maendeleo . neno la kiingereza likauzika zaidi … na hili ndilo gari nilipendalo sana.
TOYOTA COASTER – ni neno au jina la meli inayobeba mizigo kutoka bandari moja kwenda nyingine.
TOYOTA NOAH - limetokana na neno la kijapani sauti nyororo, ya kuburudisha.
TOYOTA HARRIER – ni ndege anayewinda kama tai au mwewe.
TOYOTA PASSO – hatua, steps.
TOYOTA IST - Ni kifupisho cha mwisho kutokana na maneno ya mwisho kama stylist , artist nk . ambao ni watu wenye shauku na kitu Fulani .
TOYOTA DYNA – ni magari ambayo yalibuniwa na wafanyakazi wenyewe wa Toyota , wakamaanisha neno , DYNAMIC kwa kiingereza.
Sent using Jamii Forums mobile app