Fahamu mambo 10 usiyoyafahamu kuhusu Lee Seung gi aliyeigiza Vagabond

Fahamu mambo 10 usiyoyafahamu kuhusu Lee Seung gi aliyeigiza Vagabond

Tea Party

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2019
Posts
658
Reaction score
1,133
Wakuu habarini za muda huu. Uzi sio mrefu sana.

Kwa heshima na taadhima naomba leo ni mlete kwenu kijana huyu kutokea South Korea aliyezaliwa mwaka 1987 huko Seoul.
Mambo mengi kama maisha yake ya utotoni hayafahamiki sana, lakini jina lake halisi ni LEE SEUNG GI.

Kama umeangalia series kama KING 2 HEARTS, GU FAMILY BOOK, KOREAN ODYSSEY MOUSE na kubwa kuliko VAGABOND utakuwa ushawahi kumuona kijana huyu kwenye screen yako.

Wakuu, leo naomba niweke hapa mambo kumi ambayo inawezekana huyafahamu kuhusiana na kijana huyu ambaye wadada wengi wakimuona husikia raha sana.

10. Wakorea wamempa jina la utani la TRIPPLE THREAT! Kwa kuwa yeye ni muigizaji, mwanamuziki pia ni mtangazaji mzuri tu wa vipindi vya TV huko Korea. Lee alikuwa ni mtangazaji wa kipindi cha STRONG HEARTS kuanzia mwaka 2009 mpaka 2012 na kuonesha kuwa Lee amebobea kwenye utangazaji pia kipindi hicho cha TV hicho kilishawahi kushinda tuzo ya kipindi bora cha kwenye tuzo za SBS Entertainment Awards.

9.Lee pia ni msomi. Yuko vizuri kitaaluma maana ana digrii ya INTERNATIONAL TRADE & COMMERCE aliyopata pale DONGGUK UNIVERSITY. Lee hakuridhika na kwenye chuo hicho hicho cha DONGGUK alipata Masters'ya MARKETING, TRADE THEORY, FINANCE & CULTURAL CONTENTS.

In summary Lee msimuone vile mdogomdogo ana Masters, vipi wewe unayo masters?

8. Lee ana cheti na ubobezi katika masuala ya ushauri kwa watoto yaani CHILD COUNSELING na alipata certificate hiyo baada ya kushiriki kwenye documentary au kipindi cha LITTLE FOREST ambapo mastaa hukaa na watoto na kuwalea kwenye mazingira ya kawaida kwa muda flani na alipofanya vizuri ndipo akagaiwa cheti hicho na mamlaka husika.

Sasa hapo sijui ndo tuseme ni babysitter mzuri? Anyway tuendelee.

7. Lee pia sio wa kumchukulia poa maana ameingia kwenye tasnia ya burudani akiwa na miaka 17 tu. Sasa hivi ana miaka 34 hivyo anaifahamu tasnia ya burudani nje ndani.

Alianza kwa kuimba imba na akatoa album yake ya kwanza iliyoitwa DREAM OF A MOTH ambapo humo ndani kulikuwa na wimbo wa "BECAUSE YOU ARE MY GIRL" wimbo ambao ulimtangaza vema Lee kwenye tasnia. Tokea hapo safari yake ikaanza.

Vipi wewe ulivyokuwa na miaka 17 ulikua unafanya nini?

6. Mwaka 2011 Lee alikuwa ndio msanii ambaye watazamaji walimpenda sana akionekana kwenye Tangazo. Tafiti hiyo ilifanywa na Korea Broadcast Advertising comission (KOBACO) ilihusisha watu zaidi ya elfu moja ambapo Lee aliongoza kwa kuwa na 12.5% ya audience waliosema kuwa Lee anapendezea sana akiwa kwenye matangazo hasa ya TV

5. Lee anajua lugha tatu. Kikorea, Kiingereza na Kijapan. Pia anajulikana sana huko Japan kwa kazi zake za muziki.
4.Alivyokuwa High school Lee alikuwa ni mjanja na mwenye akili sana kuanzia kwenye taaluma mpaka kwenye michezo na sanaa. Alikuwa mcheza soka mzuri akiwa shule.

3. Alipokuwa anashiriki VAGABOND Lee alifanya STUNTS ZAKE MWENYEWE kwa asilimia 90%. Director wa series alitumia Double Stunts mara chache sana huku Stunts nyingi kama ile ya kuruka kutoka ghorofani hadi kwenye gari (kama umeangalia Vagabond utaelewa) alifanya mwenyewe.

2. Lee ana mahusiano mazuri tu na PSY ambaye aliimba Gangnam Style. Kuna wimbo mmoja wa Lee alishawahi kutungiwa na Psy pia hata kabla ya kuingia jeshini alishirikiana na Psy kutunga wimbo wa kuwaaga mashabiki zake.

1. Lee alishawahi kuwa kwenye mahusiano na mwanadada Yoo Nah mwaka 2014 kisha wakaachan mwaka 2015. Kulingana na maelezo ya mawakala wao, SM ENTERTAINMENT ya Yoo Nah na HOOK ENTERTAINMENT ya Lee mwaka 2015 waliachana rasmi kwa sababu kila mtu alikuwa bize sana hivyo hawakuweza kuwa pamoja.

Uzi Tayari.
Screenshot_20210510-164234.jpg
B3RRqf.jpg
image_readtop_2021_204340_16147377274559687.jpg
download-2-3.jpg


Screenshot_20210510-164133.jpg
 
Tuache utani ile VAGABOND ni series na nusu japo sijui iliishaje labda kama ina muendelezo
 
ukitoa historical drama huyu jamaa ndo alifanya nikaanza kufuatilia drama za kimjini mjini za wakorea hasa ile series ya My girl friend is gumiho.
 
Back
Top Bottom