Helicobacter pylori
JF-Expert Member
- Feb 15, 2013
- 424
- 283
Sisi kama Wafugaji Wanyama ndio tegemeo letu kubwa katika kuinua hali zetu za kiuchumi, Vile vile Wanyama ni viumbe wenye Matumizi Mengi kwa binadamu kuanzia Chakula mpaka Urembo.
Kwa namna tunavyochangamana nao, mahusiano ya karibu na wanyama hawa wanahitaji huduma na Uangalizi wa Afya zao ili Nasi Tuwe salama.
Uangalizi wa Karibu wa Madaktari kwenye kundi la wanyama wako ama Mnyama wako utakuweka salama pamoja na Familia yako na jamii nzima.
Wanyama wanahitaji hali nzuri ya kuishi kuanzia Mazingira, Mahusiano, Chakula, kinga na Matibabu hizo ni Haki zao za Msingi kabisa ili waweze kukupatia kile ulichataka kutoka kwao, Hii ni Kwa Mujibu wa Sheria ya wanyama namba 19 ya mwaka 2008 (Animal welfare Act 2008).
Unapoamua kua na Mnyama awe kwa ajili ya uzalishaji ama matumizi mengine na Humpatii mahitaji yake ya muhimu tambua unajiweka katika Hatari ya Maradhi, Hasara na Kupoteza Muda.
Tuangalie baadhi ya magonjwa na Maambukizi ya Minyoo kutoka kwa Wanyama kwenda kwa binadamu na kinyume chake.
Zoonosis
Haya ni Magonjwa yanayoambukizwa toka kwa wanyama kwenye kwa binadamu na kinyume chake.
Tutaangalia kwa Upande wa wadudu Nyemelezi (Parasites)
Parasites (Endo + Ecto)
Endoparasite (Inside the body normally in GIT) mara Nyingi wanaishi ndani ya mwili wa Mnyama hasa Tumboni. Mfano Minyoo
Ectoparasite (Outside the body normally on skin, hair) Mara zote wapo kwenye Nywele, Juu ya Ngozi ama Ndani ya Ngozi Mfano Fungus (Kuvu), Kupe, Utitiri, Kiroboto nk.
Tuanze kuangalia Endoparisite (Minyoo) na tutaangalia baadhi ya wale tu walio Muhimu kwa wanyama na Binadamu kwa muktadha wa Nchi yetu (Tanzania).
Minyoo toka kwa Wanyama inaweza kumpata mwanadamu/Mtu kwa njia mbali mbali! Kunywa maji, kula chakula, matunda, mboga mboga, Nyama/Maziwa mabichi ambayo hajaiva vyema (Partially cooked), kula kinyesi cha wanyama ama binadamu mwenye maambukizi.
Ntazungumzia kwa makundi ya wanyama Hasa wale wenye Ukaribu sana na Binadamu.
NG’OMBE & NGURUWE
Tegu (Tape worm)
Hii ni aina ya minyoo yenye pingili pingili (Tape worm). Wenye umuhimu kwa binadamu na wanyama ni (Taenia saginata) kwa Ng’ombe na (Taenia solium) Kwa Nguruwe wanaosababisha Hitalafu kwenye ubongo (Neural cysticercosis)
Mzunguko wa Maisha ya Mnyoo wa Ng’ombe (T.saginata) na Nguruwe(T.solium).
Binadamu hupata maambukizi kwa kula Cyst wanaokuepo kwenye Nyama( Mbichi au Ambayo haijapikwa vyema) ama Mayai yanayotolewa kwenye choo.
(Cyst ni mfuko mdogo wenye maji ndani yake na Mayai hai. Mfuko huu hukinga yai/mbegu kuharibika dhidi ya mazingira mabaya kwa yai/mbegu.) kawaida Cyst wanakiwango cha juu joto la kuwaua (BP)
Muonekano wa cyst baada ya kutolewa kwenye kichwa cha Mtoto wa miaka 12.
Mtu hupata maradhi kwa kula CYST hasa kwenye Nyama ambayo haijapikwa vyema. Naomba ieleweke kwamba Wanyama wengine wakiathirika na Cyst tunasema ni Cysticercosis ila binadamu ni Taeniosis na itakua NeuroCysticercosis ikiwa atakula cyst wa T. solium kutoka kwa Nguruwe. Kumbuka sio kwamba lazima ule nyama ili upate Taeniosis au Neurocysticercosis ila hata Matunda, Maji, Mboga mboga zenye kua na mayai/pingili za Minyoo hao.
Tabia kama za kujisaidia porini, kutawaza na kutokunawa vyema na sabuni, kula matunda au mboga mboga bila kuosha vyema kwa maji yanayotiririka, kutokuchemsha maji ni tabia hatarishi kwa binadamu ila ni tabia Muhimu kwa Minyoo hawa.
Mayai yakiingia tumboni yananadilika na kua Cyst, ambao husafiri katika viungo tofauti na hatimaye kwenye Ubongo ambapo husababisha matatizo ya kiakili Kwa yule atakae pata kula mayai ya T. solium ((NeuroCysticercosis) dalili kama Kifafa, kusahau, kupooza, hii hutokana na Mgandamizo wa “Cyst” kwenye ubongo kadiri anavyokua) Pia Kichefuchefu, Choo kigumu, Kuharisha, Maumivu ya tumbo, kukosa hamu ya kula, kupungua uzito nk.
Minyoo wengine ni Trichnella na Cryptosporidium.
Picha ya Ubongo ikionyeshe namna “Cyst” walivyofurika kwenye ubongo (NeuroCysticercosis)
MBWA NA PAKA
Hawa ni wanyama tunawatumia kwa Shughuli Nyingi, kuanzia Ulinzi, Uokoaji, Uongozaji, Kimichezo, kushirikiana (Companion), viumbe pendwa(Pet) Nk, ukaribu huu na viumbe hawa ndio huongeza hatari ya kupata Maradhi hasa minyoo kutoka kwao.
Watoto ndio wapo kwenye hatari kubwa ya kupata Minyoo toka kwa viumbe hawa.
Binadamu anaweza pata Minyoo hii ama kwa kula mayai, Mbegu ama kunaswa katika ngozi na ubu (Lava).
Mbwa ama paka anapotoa choo kwenye mazingira mfano, ndani, bustanini ama bandani kwake anatoa pia na Mayai, Mbegu, ama ubu minyoo.
Ikitokea ushika kinyesi kwa bahati mbaya ama kukanyaga na hukunawa vyema , Utakula mayai na Yai litaenguliwa kua mnyoo Ama kugusana na Ubu(lava).
Mfano wa Minyoo hiyo
1. Toxocara canis
Hawa husababisha Ugonjwa unaoitwa Visceral Larva Migrant (VLM)) ambapo Ubu(Husafiri sehemu tofauti za mwili Macho,Ubongo, Maini, Mapafu ama Maini). Sio kila matatizo ya ini, figo, mapafu au moyo yanasababishwa na Presha, sukari, au magonjwa wakati mwengine ni Minyoo.
Mnyoo kwenye jicho (VLM)
2. Ancylostomum caninum
Husababisha Ugonjwa wa Cutenous Larva Migrants (CLM)) Yeye huzurura kwenye ngozi mpaka Jichoni lakini hadumu zaidi ya miezi 5-6 katika Mwili wa Binadamu.
Muonekano wa CLM.
3. Dipylidium caninum (Cucamber seed worm)
Mnyoo huyu ni aina ya tegu, ili akimilishe mzunguko wake wa maisha (life circle) anamuhitaji Kiroboto (Fleas). Anapokuwepo mbwa au Paka na viroboto basi Mnyoo huyu yupo kati yao.
Mzunguko wa maisha ya Dipylidium caninum.
Muonekano wa D.caninum kwenye choo (vijitu vyeupe hivyo).
Binadamu hupata maambukizi kwa kula mayai ama pingili hai za mnyoo huyu, pingili hizi zinauwezo wa kujongea.
Mbwa,paka au binadamu aliyeathirika na Minyoo hii, dalili kuu ni kuburuza matako sababu ya muwasho unaosababishwa na pingili za mnyoo, Pingili huonekana kwenye choo cha Mbwa, Paka au Binadamu zikiwa na rangi nyeupe na maumbo kama mbegu za matango, Mvurugano wa tumbo, kuharisha, puru kuwasha, Choo kigumu, uchovu usieleweka, maumivu ya tumbo, Kukosa hamu ya kula.
Kunauwezekano mkubwa ukasafisha eneo ambalo kuna choo cha mbwa au paka lakini mnyoo huyo ukawa umemuacha kwenye mazingira sababu kuu ni uwezo wa kujongea suluhu ni Kuogosha mbwa/Paka na dawa ili kuua viroboto na pia kutibu mbwa na paka dhidi ya minyoo.
Watoto wadogo wapo kwenye hatari zaidi kutokana na tabia yao kucheza chini na kula kula na pia wao ndio marafiki wakubwa (Ukaribu)
4. Toxocara gondii
Huyu sio Mnyoo bali ni protozoa wa paka ukoo mmoja na Cocsidiosis kwa wale wafugaji wa kuku wanamjua vyema huyu, Toxoplasma gondi husababisha ugonjwa unaitwa Toxoplasmosis, ambao huathiri wanyama wote Kuanzia Paka mwenyewe, Mbwa, Ngombe na Binadamu.
Mzunguko wa maisha ya Toxocara gondii.
Kwa upande wa binadamu Wazee, Wagonjwa, Watoto na Wajawazito wapo kwenye hatari kubwa ya kupata Maambukizi sababu ya kinga yao kua chini.
Paka na jamii yake ndio muhimu wakati wa kuzaliana (Definitive Host).
Jamii zingine zote za wanyama ni Muhimu tu kwa hatua ya Ukuaji (Intermediate Host).
Jamii zingine akiwepo binadamu hupata Maambukizi kwa kula “oocyst” ambayo ni kama mayai, kupitia matunda ambayo hayajaoshwa, Nyama isiyoiva vyema, kinyesi.
Wajawazito wakiathirika maambukizi hufika kwa mtoto na kusababisha madhara makubwa kwa mtoto aliyeko tumboni (Kuharibika mimba, kuzaa kabla ya wakati, kuharibu viungo vya mtoto mf. Ubongo, maini, macho nk) ingawa madhara yanaweza yasionekane wazi mtoto akizaliwa lakini yataonekana kipindi cha ukuaji hata utu uzima.
NAMNA YA KUDHIBITI MAAMBUKIZI YA MINYOO.
1. Hakikisha wanyama wako wapo Karibu na uangalizi wa daktari kuanzia Matibabu, Chanjo na Dawa za Minyoo.
2. Kuosha mboga mboga na Matunda vyema kabla ya kula.
3. Kunawa Vyema kwa maji na Sabuni baada ya kuhudumia wanyama, kucheza, kusafisha Malalo na mazingira ya wanyama.
4. Kuivisha Nyama vyema ili kuuwa Minyoo wanaokuwepo kwenye Nyama.
5. Chemsha Maji ya kunywa [emoji97]
6. Ni vyema kujenga utaratibu wa kutembelea Hospitali ama vituo vya Afya kwa ajili ya kuangalia Mwenendo wa Afya ya Mwili.
Minyoo Wengine
Filaria spp
Minyoo hawa wanaenezwa na mbu aina ya Anopheles na Culex.
Minyoo hii ndio Husababisha Ugonjwa wa Matende (Elephantiasis) na Mabusha (Testicular Hydroceal)
Mbu aina ya culex wanakua vyema katika ukanda wenye joto. Kwa hiyo ni lazima ung’atwe na Mbu ili upate Matende ama Mabusha.
Minyoo hawa wakiingia mwilini kwa kupitia ngozi wanaenda kuziba na kuharibu Mishipa ya lymph na Tezi zake, inayoperekea maji kujaa kwenye miguu, kende ama Matiti na Ngozi kua ngumu na kuonekana kama ya Tembo.
Matende (Elephantiasis)
Ugonjwa wa Mabusha hauna Umri wala rika, kuanzia watoto walioko tumboni mpaka wazee.
Maambukizi kwa watoto walioko tumboni dalili huanzia kuonekana tangu akiwa tumboni Mfano mfuko wa kende kujaa maji (mtoto anazaliwa na busha).
Licha ya athari za kujaa maji kwenye mfuko wa kende lakini Maambukizi yanaweza kutokea mfano Kifua kikuu cha kende (Testicular Tuberculoses).
Ugonjwa wa Mabusha (Testicular Hydrocele)
Kuharibu mazalia ya Mbu, Kutumia mafuta ya kupaka yenye kuua mbu, dawa za kupuliza na kutumia chandarua chenye dawa ni njia sahihi kabisa kudhibiti Mbu pamoja na Magonjwa wanayoeneza ikiwemo Malaria.
Kwa Maoni, Maboresho, Maswali na Nyongeza karibuni sana.
Imeandaliwa na
Sipy vetcentre - Mbuyuni Kinyerezi
0764667503