Platinum Consultancy
Member
- Jul 3, 2016
- 19
- 13
Habari za majukumu wapendwa.
Ni matumaini yetu kwamba mko vizuri katika hali zote, tunashukuru kwa hilo.
Leo tungelipenda ku-share nanyi juu ya mkakati au mikakati ya kibiashara (Business strategy)
MKAKATI WA KIBIASHARA (BUSINESS STRATEGY)
Asili ya kufikiri kimkakati katika biashara (strategic thinking) ilanzia au ilichimbukia katika medani za kivita.
Neno MKAKATI huweza kutafsiriwa kama:
Sun Tzu katika kitabu chake alikuja na mbinu ijulikanayo "First Mover Advantage", kwa maana ya kwamba mshindani anapochukua uamuzi wa kutangulia katika uwanja wa vita (battle field) kabla ya adui yake, basi hujiwekea uwezekano mkubwa wa kushinda vita.
Kimtazamo wa kibiashara tunasema kwamba mfanyabiashara anapoamua kuchukua maamuzi ya kuyafikia masoko hususani yale ambayo hayajafikiwa bado na washindani wake (untapped markets) anakuwa na uwezekano mkubwa wa kufanya vizuri dhidi ya washindani wake.
MBINU YA KIUSHINDANI KATIKA BIASHARA (COMPETITIVE STRATEGY)
Mbinu ya kiushindani katika biashara hujengwa katika msingi (premise) ya kwamba: katika biashara (industry) kuna washiriki (players) wa aina mbili. Kuna washiriki ambao hufanya vizuri katika biashara zao, na wapo ambao hufanya vibaya, hivyo basi lengo la mfanyabiashara makini ni kuhakikisha anawatawala (dominate) wote hawa wawili. Ili aweze kufanya hivi huyu mfanyabiashara hana budi kuhakikisha anakuwa na mikakati au mbinu thabiti na madhubuti za kiushindani (competitive strategy).
Kabla ya kuendelea na miongoni mwa mitizamo ya kimkakati katika ushindani, ni vyema kwanza tukawafahamu washiriki (players) katika biashara (industry), hawa hujumuisha:
Kuna mitazamo mbalimbali (views) juu ya mikakati ya kiushindani, mtazamo ulio maarufu ni huu ujulikanao kama "Kujinafasi" (positioning). Mtazamo huu huzingatia mambo yafuatayo ili kumuwezesha mfanyabiashara kuwa na mkakati thabiti wa kiushindani, ambayo ni:
Kwa huduma za:
E-mail platinumconsultancy74@gmail.com
BEI ZETU NI NAFUU SANA!!!!!!!!
NYOTE MNAKARIBISHWA

- Mpango changanuliwa (elaborated) wa kitendo fulani (action).
- Kitengo (branch) katika sayansi ya mapigano yenye kuhusika na maamrisho ya kijeshi (military command) na upangaji namna ya kupigana kiujumla.
Sun Tzu katika kitabu chake alikuja na mbinu ijulikanayo "First Mover Advantage", kwa maana ya kwamba mshindani anapochukua uamuzi wa kutangulia katika uwanja wa vita (battle field) kabla ya adui yake, basi hujiwekea uwezekano mkubwa wa kushinda vita.
Kimtazamo wa kibiashara tunasema kwamba mfanyabiashara anapoamua kuchukua maamuzi ya kuyafikia masoko hususani yale ambayo hayajafikiwa bado na washindani wake (untapped markets) anakuwa na uwezekano mkubwa wa kufanya vizuri dhidi ya washindani wake.
MBINU YA KIUSHINDANI KATIKA BIASHARA (COMPETITIVE STRATEGY)
Mbinu ya kiushindani katika biashara hujengwa katika msingi (premise) ya kwamba: katika biashara (industry) kuna washiriki (players) wa aina mbili. Kuna washiriki ambao hufanya vizuri katika biashara zao, na wapo ambao hufanya vibaya, hivyo basi lengo la mfanyabiashara makini ni kuhakikisha anawatawala (dominate) wote hawa wawili. Ili aweze kufanya hivi huyu mfanyabiashara hana budi kuhakikisha anakuwa na mikakati au mbinu thabiti na madhubuti za kiushindani (competitive strategy).
Kabla ya kuendelea na miongoni mwa mitizamo ya kimkakati katika ushindani, ni vyema kwanza tukawafahamu washiriki (players) katika biashara (industry), hawa hujumuisha:
- Watoa huduma/bidhaa (suppliers)
- Wanunuzi (buyers)
- Washindani (incumbent competitors)
- Bidhaa shabihishi (substitutes)
- Waingiaji wapya watarajiwa ( potential new entrants)
Kuna mitazamo mbalimbali (views) juu ya mikakati ya kiushindani, mtazamo ulio maarufu ni huu ujulikanao kama "Kujinafasi" (positioning). Mtazamo huu huzingatia mambo yafuatayo ili kumuwezesha mfanyabiashara kuwa na mkakati thabiti wa kiushindani, ambayo ni:
- Unafuu katika gharama (cost leadership), hapa mfanyabiashara huamua kuuza bidhaa au huduma zake kwa bei ya chini (low price) ukilinganisha na washindani wake.
- Utofauti (differentiation), hapa mfanyabiashara hujikita katika kutoa bidhaa au huduma zenye ubora wa hali ya juu (higher quality) ukilinganisha na washindani wake, japo kwa bei ya bidhaa au huduma hapa huwa juu kiasi.
- Uchaguzi (focus), hapa mfanyabiashara huamua kujikita katika eneo fulani tu kisoko katika kutoa bidhaa au huduma zake (market segment) mfano bidhaa/huduma kwa soko la wanawake tu, au watoto tu, wanafunzi tu n.k
Kwa huduma za:
- Kuandikiwa michanganuo ya miradi (project proposals)
- Kuandikiwa mipango ya kibiashara (business plans)
- Kuandikiwa mipango mikakati (strategic plans)
- Utoaji wa semina katika maeneo ya miradi, biashara kiujumla, usisite kututafuta kwa mawasiliano haya:
E-mail platinumconsultancy74@gmail.com
BEI ZETU NI NAFUU SANA!!!!!!!!
NYOTE MNAKARIBISHWA