Fahamu Mkakati wa Kibiashara (Business Strategy)

Joined
Jul 3, 2016
Posts
19
Reaction score
13
Habari za majukumu wapendwa.
Ni matumaini yetu kwamba mko vizuri katika hali zote, tunashukuru kwa hilo.
Leo tungelipenda ku-share nanyi juu ya mkakati au mikakati ya kibiashara (Business strategy)

MKAKATI WA KIBIASHARA (BUSINESS STRATEGY)

Asili ya kufikiri kimkakati katika biashara (strategic thinking) ilanzia au ilichimbukia katika medani za kivita.
Neno MKAKATI huweza kutafsiriwa kama:
  1. Mpango changanuliwa (elaborated) wa kitendo fulani (action).
  2. Kitengo (branch) katika sayansi ya mapigano yenye kuhusika na maamrisho ya kijeshi (military command) na upangaji namna ya kupigana kiujumla.
Maandiko ya mwanzo kabisa yahusuyo MKAKATI yanatokana na Sun Tzu katika kazi yake iitwayo "The Art of War". Kitabu kilichoandikwa yapata zaidi ya miaka 2000 iliyopita.
Sun Tzu katika kitabu chake alikuja na mbinu ijulikanayo "First Mover Advantage", kwa maana ya kwamba mshindani anapochukua uamuzi wa kutangulia katika uwanja wa vita (battle field) kabla ya adui yake, basi hujiwekea uwezekano mkubwa wa kushinda vita.

Kimtazamo wa kibiashara tunasema kwamba mfanyabiashara anapoamua kuchukua maamuzi ya kuyafikia masoko hususani yale ambayo hayajafikiwa bado na washindani wake (untapped markets) anakuwa na uwezekano mkubwa wa kufanya vizuri dhidi ya washindani wake.

MBINU YA KIUSHINDANI KATIKA BIASHARA (COMPETITIVE STRATEGY)

Mbinu ya kiushindani katika biashara hujengwa katika msingi (premise) ya kwamba: katika biashara (industry) kuna washiriki (players) wa aina mbili. Kuna washiriki ambao hufanya vizuri katika biashara zao, na wapo ambao hufanya vibaya, hivyo basi lengo la mfanyabiashara makini ni kuhakikisha anawatawala (dominate) wote hawa wawili. Ili aweze kufanya hivi huyu mfanyabiashara hana budi kuhakikisha anakuwa na mikakati au mbinu thabiti na madhubuti za kiushindani (competitive strategy).

Kabla ya kuendelea na miongoni mwa mitizamo ya kimkakati katika ushindani, ni vyema kwanza tukawafahamu washiriki (players) katika biashara (industry), hawa hujumuisha:
  • Watoa huduma/bidhaa (suppliers)
  • Wanunuzi (buyers)
  • Washindani (incumbent competitors)
  • Bidhaa shabihishi (substitutes)
  • Waingiaji wapya watarajiwa ( potential new entrants)
Kila mshiriki hapa (player) ana athari yake katika biashara (industry), hivyo ni vyema wakati wa ufikiriaji wa makakati wa kiushindani kuwazingatia wote hawa (considering).

Kuna mitazamo mbalimbali (views) juu ya mikakati ya kiushindani, mtazamo ulio maarufu ni huu ujulikanao kama "Kujinafasi" (positioning). Mtazamo huu huzingatia mambo yafuatayo ili kumuwezesha mfanyabiashara kuwa na mkakati thabiti wa kiushindani, ambayo ni:
  • Unafuu katika gharama (cost leadership), hapa mfanyabiashara huamua kuuza bidhaa au huduma zake kwa bei ya chini (low price) ukilinganisha na washindani wake.
  • Utofauti (differentiation), hapa mfanyabiashara hujikita katika kutoa bidhaa au huduma zenye ubora wa hali ya juu (higher quality) ukilinganisha na washindani wake, japo kwa bei ya bidhaa au huduma hapa huwa juu kiasi.
  • Uchaguzi (focus), hapa mfanyabiashara huamua kujikita katika eneo fulani tu kisoko katika kutoa bidhaa au huduma zake (market segment) mfano bidhaa/huduma kwa soko la wanawake tu, au watoto tu, wanafunzi tu n.k
Ni matumaini yetu tulicho-share nanyi kimekuwa ni chenye kueleweka.

Kwa huduma za:
  • Kuandikiwa michanganuo ya miradi (project proposals)
  • Kuandikiwa mipango ya kibiashara (business plans)
  • Kuandikiwa mipango mikakati (strategic plans)
  • Utoaji wa semina katika maeneo ya miradi, biashara kiujumla, usisite kututafuta kwa mawasiliano haya:
0719 518367, 0657935110, 0783 695639
E-mail platinumconsultancy74@gmail.com

BEI ZETU NI NAFUU SANA!!!!!!!!

NYOTE MNAKARIBISHWA
 
Asante kwa kusambaza ujumbe pamoja nasi, vipi hii mikakati ni kwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo vipi kuhusu wanaoanza biashara ?
 
Just wondering marketing strategy for products that do not lend themselves to differentiation eggs potatoes beef ...... thinking .
 
Me natamani kufungua kikampuni cha labelling je mchanganuo wake ukoje na ni sh ngp bussiness plan yake kunipatiA
 
Asante kwa kusambaza ujumbe pamoja nasi, vipi hii mikakati ni kwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo vipi kuhusu wanaoanza biashara ?

Habari mdau,
Ahsante kwa swali lako

Kwa mtu anayeanza biashara mikakati yaweza kumfaa pia, ila itatokana na asili ya bidhaa/huduma (nature of the product) atakayotaka kuingiza sokoni.
Kimsingi kuna vipengele vinne vya kuzingatia/kufahamu:

  1. Waweza kuja na bidhaa mpya katika soko ambalo siku zote lipo (existing market), kwa mazingira haya wewe unayeanza biashara unapaswa uzingatie "utofauti" au differentiation kwa sababu soko lako tayari linafahamu mshindani wako na bidhaa zake, hivyo utofauti wa ubora dhidi ya mshindani wako ndio utakufanya ung'ae sokoni.
  2. Waweza kuja na bidhaa mpya katika soko jipya pia, hapa hutokuwa na haja ya kuwa na "utofauti" isipokuwa utapaswa kuitangaza biashara yako (your vision) na pia kueleza ni namna gani bidhaa zako zitaweza kutatua matatizo ya wateja wako.
  3. Waweza kuja na bidhaa mpya kwa kutaka kuligawa kwa mara nyingine tena soko (resegment), kimsingi hapa utapaswa kutumia mkakati wa "cost leadership" ambayo itapelekea bidhaa zako kuuzwa kwa bei ya chini kuliko mshindani wako.
  4. Waweza kuja na bidhaa mpya kwa kutaka kuligawa kwa mara nyingine tena soko (resegment), hapa mbali na unafuu wa bei, waweza ku-base katika ubora wa bidhaa zako dhidi ya mshindani wako
Tunatumai tumekujibu mpendwa.

Karibu Sana
 
Me natamani kufungua kikampuni cha labelling je mchanganuo wake ukoje na ni sh ngp bussiness plan yake kunipatiA

Habari mdau.
Tutafute kwa mawasiliano yetu hapo juu. Gharama zetu zina range kuanzia Tsh 150,000 mpka 300,000
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…