Fahamu namna bora ya kutengeneza Kachori

MadameX

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2009
Posts
7,792
Reaction score
3,856


Namna ya kuandaa kitafunwa hiki aina ya kachori
Mahitaji

  • Viazi 10
  • Chumvi kiasi
  • Masala
  • Unga wa dengu 1 cup
  • Ndimu 3[h=3]Mataarisho

Namna ya kuandaa/ Kupika
  1. Chemsha viazi na maganda yake.
  2. Vikisha wiva menya maganda na kata kila kiazi vipande viwili.
  3. Katika kibakuli koroga ndimu, chumvi na pilipili ya unga kisha pakaza katikati ya kiazi halafu gandisha na kipande cha pili kiwe kama kiazi kizima.
  4. Fanya hivyo kwa viazi vyote vilivyobaki.
  5. Kwenye bakuli jingine koroga unga wa dengu , maji na chumvi kiasi uwe kama uji mwepesi.
  6. Kisha chovea kila kiazi kwenye unga huo halafu kaanga kwenye mafuta ukigeuza kama sambusa hadi kuiva.
  7. Vikisha wiva panga kwenye sahani tayari kwa kuliwa.
Soma Michango ya wadau

----
----

----
 
Dah ... this stuff is very delicious ... I like it ...

MadamX ... je nikichovya hivi viazi kwenye Maya kwa huu mchanganyiko nikavikaanga? will it be okay
 
mdizi, maya ndo nini?
 
Last edited by a moderator:
Madame X, what if baada ya kutoa maganda hivyo viazi nikiviponda na kuvichanganya na viungo kabla ya kuvichovya kwenye huo unga wa dengu.... Will it be Okay?
 
MadamX .... sorry .. I mean mayai

Mmmh, sidhani kama itawezeka kwasababu lengo la kutumia unga wa dengu ni kuvishikiza viazi viwili pamoja. Mayai hayana uwezo wa kugandisha bila kuachiana unless utachangana na unga ngano kidogo.
 
Aina ya 1...


Mahitaji
Viazi kg 1
Chumvi kiasi
Kitunguu saumu 1/2 teaspoon
Ndimu/limau 2
Pilipili
Unga wa ngano 1/2 cup
Yai 1...
Bizari 1/4 teaspoon (turmeric powder)

Namna ya kutaarisha
1)chemsha viazi vilivomenywa hadi viwive then bondabonda hadi viwe laini
2)weka chumvi,kitunguu saumu,ndimu na pilipili
3)changanya vizuri kisha tengeneza viduara vidogo vidogo

4)weka unga,bizari,yai na maji kiasi changanya vizuri uwe kama uji mzito mzito
5)weka mafuta katika karai
6)chukua viduara vya viazi ulivotengeza na upakae huo uji then kaanga kwenye mafuta..


Kachori tayari kwa kuliwa..
 

Attachments

  • 1385217754244.jpg
    55.4 KB · Views: 797
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…