Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Miongoni mwa mboga za majani ninazopenda ni pamoja na tembele, leo ngoja niwashirikishe jinsi ya kuyapika matembele.
Pishi hili ni kwa wale wenye Maisha ya kawaida kabisa ambao tunapika bila vipimo (tunakadiria lakini msosi unakuwa mtamu balaa).
Mahitaji:
Pishi hili ni kwa wale wenye Maisha ya kawaida kabisa ambao tunapika bila vipimo (tunakadiria lakini msosi unakuwa mtamu balaa).
Mahitaji:
- Matembele mafungu mawili ( hapa inategemea na mahitaji)
- Nyanya tatu
- Kitunguu cha wastani kimoja
- Kariti moja( sio lazima sana)
- Hoho( ukipenda sio lazima sana)
- Mafuta kiasi
- Chumvi kiasi
- Chukua matembele yako yachambue vizuri kutoa vinyuzi kwenye mikia yake kwa kuvunja mkia wake na kuvuta kile kivyuzi kwa kuwa huwa yanakua magumu kama usipotoa.
- Waweza kuyaweka juani yanyauke kidogo kama ukipenda sio lazima sana(mimi hupendelea yaliyonyauka)
- Yasafishe vizuri matembele yako, kisha andaa viungo vyako kwa kuanza upishi.
- Weka mafuta kiasi cha vijiko viwili kwenye sufuria na weka jikoni( hapa inategemea na wingi wa mboga uliyonayo)
- Mafuta yakipata moto weka vitunguu na kanga mpaka view kahawia.
- Weka nyanya zako ulizokatakata na kanga kisha weka karoti kanga kisha weka hoho kama unayo kaanga mpaka mchanganyiko uwe sawa.
- Weka chumvi na uendelee kukaanga mpaka mchanganyiko uwe sawa na uive ila usitumie muda mrefu ili usije kukauka.
- Weka matembele yako geuza geuza na kisha ufunike.
- Tumia dakika tano mpaka saba kisha funua na geuza kisha onja chumvi na kama iko sawa epua ili mboga isiive sana kutunza vitamini vyake.
