Wakili
JF-Expert Member
- Jun 19, 2017
- 531
- 657
Habari wapendwa,
Mimi ni mwenyeji wa Kilimanjaro, wilaya ya Mwanga,tarafa ya Ugweno.
Napenda kuwafundisha pishi la kiburu na kiombo kwa kipare.
Pishi hili linahitaji ndizi mshale,maharage,magadi,mafuta na chumvi.
1. Kwanza unapika maharage hadi yaive na yanapokaribia kuiva unayatilia kijiko kimoja cha magadi ya maji.
2. Unamenya ndizi yako na kuitilia kwenye maharage yaive kwa pamoja.
3. Unapoa hakikisha ndizi zimelainika unaweka chumvi na kufunikia katika chungu chako na jani la mgomba.
4. Bada ya hapo unasonga chakula chako hadi kilainike na mwiko.
5. Kama unataka kutoa kiombo utakoroga na maji hadi kibalnce urojo hapo kitakua tayari.
6. Kama unataka kutoa kishumba utasonga bila kutilia maji hadi ndizi na maharage vilainike hapo kishumba chako kitakua tayari.
Asanteni.