boniuso
JF-Expert Member
- Mar 13, 2013
- 786
- 1,043
FAHAMU SABABU ZA UPWEKE NA MADHARA YAKE
Hisia za upweke huwa zinakuja pale unapohisi kuna kitu huna ili uweze kuwa na furaha
Kitendo cha kutamani vitu kutoka nje yako ili uweze kuwa na furaha husababisha huzuni na hasira
Unaweza kutamani kuwa na mtu karibu,kuwa na kipato kadhaa,kazi fulani,kuwa sehemu tofauti ili uweze kuwa na furaha lakini vyote kwa ujumla unakosa na kujisikia upweke kupita kiasi
Zipo sababu za watu kuwa na upweke nazo ni
KUPITIA MAHUSIANO MABAYA
Kuna watu wamekuwa na marafiki ,mke au mume au mazingira ya kazi ambayo kwa kiasi kikubwa yamegubikwa na manyanyaso sana hivyo wamezoa manyanyaso mpaka hawana uwezo wa kuondoka na kwenda kwengineko
Kitendo cha kuvumilia maumivu makali ya matusi,dhihaka,kejeli, mafumbo, vijembe,lawama, kukosolewa, kuzomewa kwa muda mrefu hujenga hisia za kujichukia mwenyewe
Kitendo cha kujichukia mwenyewe huzidisha maumivu ndani kwa ndani kiasi cha kukuzuia kufurahia vile upo navyo badala yake unafikiria sana vile huna
Kuwa na mahusiano ya upande mmoja husababisha mtu mmoja kuwa na bidii sana ya kuhakikisha mahusiano yaanadumu huku mwengine hana habari wala hajali chochote
Kitendo cha kuishi na mtu hajali chochote kuhusu hisia zako hufanya mtu mwenye juhudi sana kuishi kwenye majuto,mawazo,hasira, kuchanganyikiwa, kupoteza matumaini ya kupendwa
Hisia za upweke huwa zinazidi hasa unapozoea kuona au kusikia maneno fulani kutoka kwa mwenzio
2. KUTEGEMEA 50/50 KUTOKA KWA WENGINE
Kama unaishi na mtu unampenda sana na yeye anakupenda sana hisia za upweke huwa zipo sanaa hasa nyakati ambazo unakuwa unamuhitaji sana mwenzio huku yeye akiwa na vipaumbele tofauti
Hisia za upweke huwa zinaongezeka kama umezoea kuona sms au kupigiwa simu kisha unaishi huoni sms wala kupokea simu,
Hisia za upweke huwa zinazidi kama umezoea kumwambia mwenzio maneno mazuri na yeye anakurudia maneno mazuri
Hisia za upweke huwa zinakuja kama kile kizuri unamfanyia mwenzio unatarajia akufanyie na wewe
Hisia za upweke huwa zinakuja kama unawajali sana wengine huku unataka wao wafanye kwako kwa 50/50
Haijalishi mtu unampenda sana na yeye anakupenda sana kiasi gani ikifika hatua kuwa furaha yako unategemea maneno ya umpendae lazima upate hisia za upweke
Furaha ya kweli haipo kwenye mahusiano yako, haipo kwenye pongezi, haipo kwenye maneno mazuri ya wengine, haipo kwenye kazi yako, haipo kwenye matokeo mazuri ya matarajio yako
Kitu chochote ambacho pesa inaweza kununua hakiwezi kukupa furaha ya kudumu.
Kama umeweka furaha yako kwenye kitu kimoja basi kitu hicho kutakutesa sana
Ukiweka furaha yako kwenye biashara, kazi, ndoa, watoto, pesa, simu, gari, nguo, muonekano wa sura yako na maumbile yako vyote hivyo huathiriwa na mabadiliko ya mazingira
Furaha yako haitakiwi kuegemea kwenye vitu vinavyoweza kukumbana na vikwazo kutoka nje.
Furaha ya kweli ipo kwenye kuelekeza fikra zako kwenye vitu tofauti tofauti kila unapoona sehemu ulitarajia furaha imekuwa tofauti
Wabunifu huwa wenye furaha sana kuliko watu wote kwa sababu wao huchukulia kila mpango au matarajio yenye kwenda tofauti kama fursa mpya ya kujifunza.
3. KUWAPA WATU WENGINE MAAMUZI YA KUKUPA FURAHA
Kama furaha yako huwa inategemea maamuzi ya wengine huwezi kuwa na furaha kama watafanya maamuzi tofauti na matarajio yako
Kama furaha yako inategemea watu wengine wanavyokutendea huwezi kuwa na furaha
Furaha haiwezi kutegemea vitu kutoka nje yako kwa sababu kuna sababu nyingi sana za kukuzuia usifanikiwe kuipata kama vile ahadi kuvunjwa, kazi umetuma maombi kuikosa, Ombi la msaada kukataliwa
Unaempenda anaweza kuondoka na kwenda kumpenda mwengine
Sura yako inaweza kupata dosari labda magonjwa ya ngozi au kuzeeka
Watu wanaokusifia wanaweza kukaa kimya ghafla
Watu unaowajali hisia zao na matarajio yao kwako yakiwa tofauti wataacha kuwa karibu yako
Anasema Dr. Viktor Franklin muhanga wa mauaji ya Auschwitz wakati wa Hitler kuwa "between stimulus and response there is a space of our choice to respond"
Kwamba baina ya mabadiliko au taarifa kutoka nje yetu kuna fursa ya sisi kuchagua maamuzi ya kufanya
Watu wanaweza kukuweka gerezani lakini hawawezi kuiweka akili yako gerezani
Watu wanaweza kukuweka kizuizini lakini hawawezi kukuzuia kufikiri
Dr. Viktor Franklin akiwa kwenye mateso ya Hitler alishuhudia mama yake mzazi,baba yake,mkewe,kaka yake wote walichomwa moto kwenye gesi
Alipitia mateso makali sana lakini alichukuliwa ile ni fursa kwake ya kujijenga kiakili
Aligundua kwamba binadamu anaweza kukutesa lakini hawezi kuitesa akili yako
Kama kuna mtu tabia yake huipendi na wewe huna furaha kwa sababu ya tabia zake wewe ndio mwenye makosa sio yeye kwa sababu hajakulazimisha ufikirie mabaya yake bali wewe
Bado uhuru wa kufikiri upo kwako hata ukiwa kwenye maumivu na mateso ndio sababu wapo hujiua kwa kupoteza kazi au kufumania wenza wao huku wapo waliokaa gerezani miaka 30 wakiwa na furaha na upendo kwa wengine mfano Nelson Mandela,Malcom X
4. KUISHI KWENYE MAISHA YA ZAMANI
Kuishi kwenye majuto ya makosa yako, kutamani siku za nyuma zirejee, kuendelea kuvumilia maumivu ya tabia za wengine
Kuogopa kukataliwa kama utaanzisha mahusiano mapya,hofu ya kukataliwa na wengine kwa sababu za mapungufu yako
Kuacha kujaribu vitu na fursa mpya kwa kuzoea zile za siku zote na kuogopa changamoto mpya
Kuishi na watu wenye kukuchukia huku haupo tayari kujitenga nao wala kukutukana na watu tofauti tofauti
Kuishi huku ukivuta kumbukumbu za miaka iliyopita kama vile ulipitia mateso, manyanyaso,ubaguzi,ajali, kumpoteza umpendaye,
Vitu vya kukusaidia
1. Jipende sana kuliko siku zilizopita hata kama huna pesa, kazi, cheo, umaarufu, muonekano mzuri au sura nzuri
Tajiri namba moja duniani sio mwenye furaha kuliko watu wote duniani
Tajiri namba moja duniani sio mwenye sura nzuri kuliko watu wote duniani
Tajiri namba moja duniani sio mwenye kupendwa sana kuliko watu wote duniani
Tajiri namba moja duniani sio mwenye akili sana kuliko watu wote duniani
Tajiri namba moja duniani sio mwenye mke mzuri kuliko watu wote duniani
Tajiri namba moja duniani sio mwenye afya nzuri kuliko watu wote duniani
Maana yake hata kama utakuwa na kitu kizuri ambacho watu watakipenda bado huwezi kuwa na kila kitu
2. Shukuru sana kwa hali unapitia
Kuichukia hali unapitia haiwezi kukusaidia chochote zaidi utaendelea kuteseka
3. Saidia watu kisha ondoa matarajio kwao kwa sababu unapoweka MATARAJIO kwa watu ndio unapovunjwa moyo
"Expect nothing accept everything,focus on what you can control and let go what you can't control"
Kupata kitabu cha
1. UTULIVU WA AKILI KIPINDI KIGUMU (Softcopy)
2. FIKRA ZAKO FURAHA YAKO (softcopy)
3. TIBA YA MSONGO WA MAWAZO (hardcopy & softcopy)
4. BADILI FIKRA ZAKO BADILI MAISHA YAKO (hardcopy & Softcopy)
5. MALEZI YA UBONGO KISAYANSI( hardcopy & softcopy)
6. TABIA ZA WATU WALIOFANIKIWA (Hardcopy & softcopy)
7.MISINGI 10 YA FURAHA SIKU ZOTE (hardcopy &softcopy)
+255766862579
+255622414991
Imeandikwa na Psychologist
Said Kasege
Temeke,Dar es salaam