Fahamu sifa za mwanaume asiye na pesa

Craig

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2013
Posts
1,512
Reaction score
2,712
1. Viatu huisha upande mmoja
2. Kushabikia YANGA
3. Hunywea maji kwenye jagi hata kama kuna glass au kikombe
4. Kupenda kuvaa suruali zenye rangi ya kung'aa.
5. Kufungua soda kwa meno
6. Kuvaa socks hadi magotini hata kama hayupo mazoezini
7. Anapenda sana kuangalia movie zilizotafsiriwa
8. Kufuta jasho kwa vidole
9. Kupiga miayo hadi machozi yanamtoka.
10. Kuingilia ugomvi hata wa watoto wadogo
11. Kumchukia kila mwanamke anayemiliki gari
12.Kumiliki smartphone iliyopasuka kioo.
13.Akitengewa chakula lazima amalizie kunywa mpaka na mchuzi kwenye kibakuli.
14.Kila mwanamke anayemchangamkia kwake anajua ashapata zari la kupendwa.
15.Wanapenda sana kutafuna vitumbua asubuhi asubuhi bila chai.
16.Akiingia kuoga bafuni, anahakikisha anasugua mpaka ndala akiamini usafi huficha umasikini.
17.Akipanda dala dala lazima ashike nauli mkononi ili isije kudondoka.
18.Wanapendaga sana kukaa siti za dirishani kwenye safari yoyote.
19.Ukiangalia mashati yake mengi utakuta kola za mashati zimeanza kuchanika.
 
mimi nikipiga miayo[sina uhakika na spelling] natoka machozi lakini mbona nina pesa. Haina maana hauna kabisa, hapa ina maana unazo za kubangaiza. Nakupa muda ufanye utafiti.
 
Mtoa mada unaongelea asilimia 90% ya wanaume wote tz!!

Wenye pesa wachache sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…