Fahamu zaidi kuhusu Boat Bar

Fahamu zaidi kuhusu Boat Bar

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2018
Posts
5,489
Reaction score
14,091
Boat Bar ni Boti Kubwa ambayo Ina miundombinu ya watu kupata vinywaji na chakula wakiwa ndani ya boti. Boti hii ni kwaajili ya utalii,starehe na sehemu ya kufanyia vikao.

images (12).jpeg

Boat Bar inaweza ikafanya safari fupi kando ya pwani wakati raia wakiendelea kujivinjari, pia inaweza ikatia nanga kando ya ufukwe.

download (2).jpeg

Boti hii uwekewa nakshi za fenicha,sehemu nzuri za kupumzika,sehemu ya music wa live band na vyumba vichache vya mapumziko.

images (9).jpeg

Kwa Ukanda wa Dar es Salaam boti kama hii inaweza kufanya kitalii pembezoni mwa bahari. Zanzibar pia inaweza kufanya kazi za kitalii Kwa kuwazungusha raia pwani ya bahari.

download (3).jpeg

Faida ya boti hii ni Kampuni au waendesha huduma Kuwa Zaidi ya Mmoja na kuleta Nafasi na fursa kibao za Ajira. Mosi ni Kampuni yenye boti, pili Kuna Kampuni ya kutoa huduma ya vinywaji,chakula,burudani,wakatisha tiketi na watoa Usafiri wa Taxi/Bajaj/Bodaboda.

download (1).jpeg

Mifumo ya usalama katika boat Bar pembeni boti huwekwa Kingo za kuzuia mtu asianguke(Guard Rail),pia mfumo wa stabilizer ufungwa vifaa vya kisasa Kwa ajili ya stability (Humphree stabilizer) ambayo hubalance chombo wakati wa mawimbi na kufanya abiria Kuwa na utulivu(Comfortable) wakati wa Hali mbaya ya bahari.Moja ya jaribio ni abiria akiweka glass au chupa ya soda kwenye meza kinywaji hakiwezi kuanguka.

Boat Bar hufanya kazi kwa mfumo wa booking au membership card au entrance fee ambazo humuwezesha mtu kuingia na kupata huduma.

Kwa wenzetu Uganda kipindi Cha nyuma walikuwa Wana Boti ndogo Mv Earth Wise katika Bandari ya Port Bell ilikuwa ikikodiwa na kufanya safari za utalii ndani ya Ziwa Victoria.
 
Kuna jamaa zetu wakilewa wanaanza kutafuta njia ya kwenda kwao sasa sijui itakuaje?😅😅😅😅
 
Huyo Mjomba ye anataka aone Ile kitu yenye utelezi tu story za mtungi hatakagi kabisa [emoji1][emoji1][emoji1]
Utelezi hapo ndio nyumbani kwake, atakutana na watoto wanaota jua kwenye deck ya meli kama wapo Ibiza au Coppa Cabana
 
Kuna jamaa zetu wakilewa wanaanza kutafuta njia ya kwenda kwao sasa sijui itakuaje?😅😅😅😅
Watatulizwa sehemu Salama na customer care ya kimataifa, hii inakuwa na ratiba kila Baada ya masaa 2 au 3 inakuja nchi kavu na kuondoka kurudi baharini
 
Back
Top Bottom