Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Salaam Wakuu, karibu tupate somo la lugha tujikumbushie shule kidogo. Najua wengi wetu kwa namna moja au nyingine katika harakati za kusoma mshawahi kusikia neno kirai na kishazi. Katika kujifunza lugha hususani katika masuala yanayohusu aina za maneno na sentensi Virai na Vishazi havikwepeki.
Kwakuwa mada hii ni pana nimeona katika andiko hili nieleze kwanza kuhusu Virai na aina zake halafu andiko linalofuta tutatazama vishazi. Twende pamoja hapa chini:
Maana ya Kirai
Kirai ni dhana ambayo imefafanuliwa na wataalamu wengi lakini katika andiko hili nitatumia ufafanuzi wa Massamba na Wenzake (2009). Wao katika andiko lao wanaeleza kuwa Kirai ni kipashio cha kimuundo chenye neno moja au zaidi lakini ambacho hakina uhusiano wa kiima kiarifu
Muundo wa Kirai
Wataalamu wengi wanakubaliana kwamba kirai ni kipashio cha mimuundo ambacho kinaundwa na sehemu kuu mbili ambazo ni: (i) neno kuu; na (ii) kijalizo
Neno kuu ni nini?
Akitumia mfano wa ndoano, O’Grady (1996: 185) anaeleza kuwa vishazi hujengwa katika kiunzi chenye viwango viwili kama inavyoonyeshwa katika kielelezo hiki hapa chini (msimbo K ukisimama badala ya kirai):
KN KT KV KE KH ← kiwango cha kirai
׀ ׀ ׀ ׀ ׀
N T V E H ← kiwango cha neno
Anaendelea kusema kuwa kila kiwango cha muundo wa kirai kinaweza kufikiriwa kama ndoano fulani ambapo vipashio vya aina aina vinaweza kupachikwa. Kiwango cha chini kabisa ni kwa ajili ya neno ambalo kwalo kirai ndio hujengwa – N kwa upande wa KN, T kwa upande wa KT, V kwa upande wa KV, E kwa upande wa KE na H kwa upande wa KH. Kipashio hiki ndicho huitwa neno kuu. Kwa hiyo, kutokana na maelezo ya O’Grady, tunaweza kusema kuwa Neno kuu ni neno linalotawala kirai chote. Neno kuu linachukuliwa kuwa linatawala kirai kwa kuwa linaweza kutokea peke yake katika kirai kama mifano ifuatayo invyoonyesha:
1) KN 2) KT
N T
(Anapenda) vitabu
(viumbe hai wote) hula
(Watoto wamefanya) mtihani
(Simu yako) inaita
3) KV 4) KE
V E
(Huu ni mchezo) mgumu
(Wewe unapika) vizuri
Hata hivyo, katika sarufi ya Kiswahili, neno kuu la kirai kihusishi, kama inavyoonekana katika mfano wa 5 hapa chini, haliwezi kujitosheleza likiwa peke yake bila kijalizo chake.
5) KH
(Watakuja chuoni) kwa
(Watakuja chuoni) kwa gari
Kwa hiyo, ingawa ni kweli kwamba neno kuu huweza kuwa peke yake katika kirai, muundo wa kirai kihusishi hutofautiana na miundo ya virai vingine kwa sababu neno kuu la kirai kihusishi halijitoshelezi kimuundo bila kijalizo chake.
Kijalizo
Kijalizo ni kile kipashio kinachojalizia/kamilisha neno kuu. Kwa mfano, katika mfano wa 5 hapo juu, nomino gari ni kijalizo cha kihusishi kwa. Kijalizo kinaweza kuwa neno moja au kifungu cha maneno mawili au zaidi. Katika kirai, neno kuu hutangulia na kijalizo chake hufuatia.
Kutokana na muundo huu wa kirai, tunaweza kuzikataa fasili zote za kirai zinazodai kuwa kirai ni kifungu cha maneno mawili au zaidi kwa kuwa imedhihiri kuwa kirai kinaweza kuundwa na neno kuu peke yake. Hivyo, kirai kinaweza kufasiliwa kuwa ni neno au kifungu cha maneno kinachotawaliwa na neno-kuu moja.
Aina za Virai
Kwa kawaida, katika uainishaji wa virai, kategoria ya neno kuu ndiyo hutumiwa kutambulisha aina ya kirai kinachohusika. Kwa hiyo, kama ambavyo tuliona katika mifano 1 – 5 hapo juu, tuna aina zifuatazo za virai.
1) Virai nomino (KN)
2) Virai vitenzi (wengine huviita virai tenzi) (KT)
3) Virai vivumishi (wengine huviita virai vumishi) (KV)
4) Virai vielezi (wengine huviita virai elezi) (KE)
5) Virai vihusishi (wengine huviita virai husishi) (KH)
Hata hivyo, wapo wataalamu ambao hawaungi mkono idadi hii ya virai. Wao wanaona vipo pugufu. Kwa mfano, Mdee (2007) anatambua kuwapo kwa aina tatu za virai: vikundi nomino, vikundi vitenzi na vikundi vielezi lakini anapoviainisha anaona kuna aina mbili tu za virai: kikundi nomino na kikundi kielezi. Nkwera (1989) naye anatambua kuwapo kwa aina tatu tu za virai: virai vya nomino, virai vya vivumishi na virai vya vielezi. Si lengo letu kuhoji usahihi au upotofu wa mtazamo wa Mdee na Nkwera. Tunachoweza kusema tu hapa ni kwamba mtazamo wao kwa sasa unakosa mashiko kwa kuwa utafiti umethibitisha kuwapo kwa virai vingi zaidi ya hivyo vinavyotajwa na watu hawa.
Aidha, wapo wataalamu wengine ambao wana idadi hii ya aina tano za virai lakini hawajumuishi aina zingine tulizozitaja hapo juu. Mathalan, Massamba na wenzake wana virai viunganishi lakini hawana virai vihusishi.
Tutajaribu kuvipitia kwa ufupi virai tulivyovibainisha hapo juu aina moja baada ya nyingine.
1) Kirai nomino
Neno kuu la kirai nomino ni nomino. Vijalizo vyake vinaweza kuwa vikumushi mbalimbali kama vile vivumishi (mwalimu mgeni, ugonjwa hatari), au virai vivumishi (mwanamke mwenye maziwa makubwa sana), virai viunganishi (mama na mwana, mume na mke), virai vihusishi (mpishi wa shule, safari ya ndege, suala la kijinsia), sentensi (mwalimu aliyetufundisha mwakajana), na muunganiko wa vikumushi kama vivumishi, vionyeshi na sentensi (mtoto wako yule mzuri uliyemtuma kukuleta kuni jana).
Kidhima, kirai nomino kinaweza kuwa kiima, yambwa, yambiwa, kijalizo cha kirai kihusishi na kinaweza kukaa mahali pengine popote ambapo nomino inakaa.
Kwa mfano
Walimu wakuu waliwapa wanafunzi wao wote vyeti vyao kwa siku moja.
Kiima yambiwa yambwa kijalizo cha KH.
2) Kirai kitenzi
Neno kuu la kirai kitenzi ni kitenzi. Vijalizo vyake vinaweza kuwa kitenzi (ilikuwa inanyesha) kirai nomino (anapika ndizi, utawapenda watu wote), kirai kihusishi (anacheza kwa magongo ya miti, atasafiri kwa ndege), kirai kielezi (usisogee huko, wanacheza vizuri mno) na sentensi (anafundisha alivyotufundisha mwaka jana).
Kidhima, kirai kitenzi kinaweza kuwa kiarifu.
3) Kirai kivumishi
Neno kuu la kirai kivumishi ni kivumishi. Vijalizo vyake vinaweza kuwa vikumushi vyake mbalimbali kama vile vivumishi (mrefu mweusi, mweusi mtanashatitanshati), virai vielezi (mzuri mno, mwembana sana), virai nomino (mwenye kipara kipana), virai vihusishi (mlimbwende wa Tanzania, mtoro wa mwaka), na sentensi (mtundu anayewahangaisha polisi).
Kidhima, kirai kivumishi kinaweza kuwa kikumushi cha kirai nomino (mtoto mdogo mjanja), kiima cha sentensi (wadogo wote wamesonga mbele).
4) Kirai kielezi
Kirai kielezi ni kirai ambacho neno lake kuu ni kielezi. Vijalizo vyake vinaweza kuwa vielezi vingine (vizuri sana, kwa mfano katika: umesoma vizuri sana, ughaibuni milele, kwa mfano katika nakwambia wewe hutafika ughaibuni milele), virai vihusishi (usiku wa manane, ofisini kwa mwalimu wangu), vivumishi (shuleni kwetu).
Kidhima kirai kielezi kinaweza kuwa kikumushi cha kirai kitenzi (anatembea kibatabata, wameimba kishamba mno), kiima cha sentensi (nyumbani kwao kuna wageni, kibatabata ni mwendo wanaotembea walimbwende majukwaani).
5) Kirai kihusishi
Kirai kihusishi ni kikundi ambacho neno lake kuu ni kihusishi. Vijalizo vyake vinaweza kuwa kikundi nomino (katika kituo cha mabasi, ya udongo mwekundu), kishazi cha kitenzi jina (kwakutia saini mkataba, kwa kupokea zawadi nono, ya kutoa nakala ya kitabu hiki), kishazi/sentensi rejeshi ((amepewa kipigo) kwa alichokifanya usiku wa kuamkia leo) na katika miundo mingine, ambayo watu wengi nilipowasaili walidai si Kiswahili safi, kikundi kihusishi kinaweza kuundwa na kihusishi na kishazi cha kwamba (neno la Bwana linasema ya kwamba Hagai alimzaa Yonamu).
Kidhima kihusishi kinaweza kuwa kikumushi cha nomino (mganda ya miti, mtumbwi wa makuti makavu), kikumushi cha kitenzi (Osama amekufa kwa aibu kubwa), au kiima cha sentensi (yaani kinaweza kufanya kazi kama kiwakilishi (Kwa mkuu wa shule kumewekwa matangazo mengi).