Faida au hasara za misaada

Joined
Oct 12, 2012
Posts
23
Reaction score
2
Kuna faida za nchi kama Tanzania kupewa misaada ya kimaendeleo? Tafadhali kama unaona kwamba kuna faida au hasara weka maoni yako hapo. Asante
 
Wahenga walisema 'Amlipae mpiga nzumari ndio huchagua wimbo' Mara zote kuendisha taifa kwa kutegemea misaada sio jambo zuri kwani hata misaada yenyewe anayekupa ndiye atakayekuchagulia kipi cha kufanyaia na kipi sio cha kufanyia na mara zote waliopo juuu huwa hawataki kufikiwa na waliopo chini!!
Kwa upeo wangu mdogo huwa naona hakuna jambo zuri kama kujifunza kujitegemea aidha kwa mtu binafsi, familia na taifa kwa ujumla. Kielelezo kizuri ni pale mtu wako wa karibu akutafutie kazi na muwe mnafanya ofisi moja na awe bosi wako, hutopinga kitu chochote atakachokuambia kwa kumwonea aibu kwani yeye ndiye kakuweka pale na utasahau mpaka sifa ulizokuwa nazo.
Hivyo hakuna kitu kibaya kama kuendesha Nchi kwa kutegemea misaada.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…