Faida gani ntapata kufungua website au blog?

Faida gani ntapata kufungua website au blog?

Zembeta

Member
Joined
Dec 15, 2012
Posts
31
Reaction score
2
Habari gan wana jf leo nimekuja na swali langu la faida gani ntaipata kufungua website au blog nawaomba mnipe ufafanuzi kwa wale wenye uelewa na mambo ya blog na web site.

Asanteni.
 
Kufungua blog ama website ni suala moja, sababu na faida ya kufungua ni suala jingine.
Swali lako ni sawa kama umefika UBT kisha wauliza nipande basi gani, litanifikisha wapi?
Maana yangu ni kwamba ni muhimu kujua mwisho wa safari yako kabla ya kwenda stendi, kabla ya kutaka faida, jiulize kwanini wafungua blog ama web, ni nini kusudio ama nia ya kufanya hivyo, ona mwisho wa safari mwanzoni.
 
1. Kupitia blog unaweza kutoa habari unazotaka zifike kwa jamii.
2. Unaweza kupata habari unazohitaji kutoka kwa wasomaji wanaochangia.
4.Unaweza kufanya biashara ya matangazo kwa blog.
5. Blog yako ikipata wasomaji wengi unaweza kuiuza kwa pesa nyingi.
6.Unaweza kutoa ajira kwa ndugu, jamaa, marafiki na wanajamii wengine.
7. Kupitia blog utafahamika na kufamiana na watu wengi wanaoweza kuwa na manufaa kwako kwa namna moja au nyingine.
8. Kama unafanya kama hobbie utaenjoy...
 
Nimefungua blog mkuu lakini inanichanganya jinsi ya kuweka matangazo je unaweza kunifahamisha mkuu..?
 
Back
Top Bottom