Kufungua blog ama website ni suala moja, sababu na faida ya kufungua ni suala jingine.
Swali lako ni sawa kama umefika UBT kisha wauliza nipande basi gani, litanifikisha wapi?
Maana yangu ni kwamba ni muhimu kujua mwisho wa safari yako kabla ya kwenda stendi, kabla ya kutaka faida, jiulize kwanini wafungua blog ama web, ni nini kusudio ama nia ya kufanya hivyo, ona mwisho wa safari mwanzoni.