Faida gani za kiuchumi naweza kuzipata kwa kujichora tattoo mwili mzima?

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2015
Posts
6,661
Reaction score
21,656
Wakuu mko poa?
Jamaa yangu mmoja kafungua hizi ofisi za kuchora watu tattoo na juzi alinikaribisha ofisini kwake kuona mambo yanavyoenda,katika maongezi yetu nilimuomba kidogo anikopeshe hela lkn kitu cha kushangaza aliniambia sasa hivi biashara ni mbaya kuliko navyoweza kufikiri lkn akaniambia kitu pekee anachoweza kunisaidia kwa sasa ni kunichora hizo tattoo bure,hata kama nitahitaji kuchora mwili mzima.
Kama ilivyo ada,JF home of GT, je naweza pata faida gani za kiuchumi nikijichora tattoo mwili mzima, yaani nawezaje kubadilisha tattoo kuwa cash?
 
kama unafanya biashara jiandike tangazo la biashara zako, mfano ka una uza mbao unajiandika tangazo la kuuza mbao utanufaika kiuchumi.
 
shughuli utakumbana nayo wakati unataka kufuta hizo tatoo.

maana wino ni kama unaingia ndani ya ngozi
 
Tatuu muda mwingine sio za kujichora harikadharika inaweza kukuletea misukosuko ya kimaisha kutokana na Picha unayojichora na maana yake au bila kujua maana yake..
 
Kibongo bongo zaidi ni Fursa za Kimapato Kupungua......Bado watu wenye'' tattoo'' wanachukuliwa kwa mtazamo hasi..
 
hakuna faida yoyotye,lada kama kuna mtu amekwambia ili upatea au akupe lada mill.10 hivi uchore tattoo ila napo bado ni njaa ilopitiliza,haina faida mkuu mana hilo sio duka kwamba unatmbea nalo au leseni ni mapambo tu na kuudhi mwili sema tu hauongeiiii.
 
Unaweza ukapata bahati ya kufananishwa na wiz au lil wayne
 
Anataka kutumia mwili wako kama matangazo ya yeye kujipatia fedha, maana watu wakikuona umependeza lazima wakuulize umechora wapi nawe utawa Direct kwa aliyekuchora na yeye kujipatia fedha
 
Utafaidikaje kwa kujichora tattoos?

Ipo njia, si unajua hakuna kinachoshindikana?

Mwambie akuchore tattoo nzuri/yakijanja. Labda tatto zinazohusu mambo yaliyojificha ya kiafrika?

Unajichora vitu kama vile sign ya Ankh (truth and life) au unachagua alama nzuri ya Adinkah. Ukimaliza haya anzisha kurasa yako kwenye instagram unajipiga picha zenye ubora una-share na ulimwengu. Hii itasaidia wanaopenda wakuulize wapi wataweza kuchora. Wewe utapatana na huyo jamaa yako je anaweza kukulipa kwa kila mteja wa tattoo utakayemleta kwake.

Its all about being smart upstairs and understand how to influence people and make some dough.
 
Utapata faida ya kujiweka kwenye hatari(risk) ya kupata kansa ya ngozi (skin cancer)..ni hayo tu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…