Faida katika biashara, gharama za uzalishaji, idadi ya bidhaa

Faida katika biashara, gharama za uzalishaji, idadi ya bidhaa

LOVINTAH GYM

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2015
Posts
459
Reaction score
653
AVERAGE COST

Kama tunavyofahamu neno average ni wastani, na cost ni gharama.

Hivyo Average cost ni kuchukua jumla ya gharama zote fixed na variable cost (total cost) alafu ugawe kwa idadi ya vitu ulivyovizalisha (output).

Mfano:

Muuza mihogo ya kukaanga ametumia gharama ya 50,000 na amefanikiwa kukaanga mihogo 50.

Kwahiyo 50,000 ndio total cost yetu

50 ndio output yetu

sasa ili tuweze kupata average cost =50,000 gawanya kwa mihogo 50

Average cost yetu itakuwa ni 1000, kwahiyo inamaana umetumia shilling 1000 kufanikiwa kukaanga muhogo 1.

Kwahiyo muuza mihogo akiamua kuuza muhoga 1 kwa bei ya 1500

Profit (Faida) = (Price - Average cost) x Quantity

Faida = (bei yetu - wastani wa gharama) x idadi ya bidhaa

Faida = (1500 - 1000) x 50

Faida = 500 x 50

Faida =25,000

Kwahiyo muuza mihogo akifanikiwa kuuza mihogo yote 50 aliyokaanga kwa bei ya 1,500 na gharama 50,000 atafanikiwa kupata faida ya 25,000

Average-Cost.jpg

Mfano 2:

Muuza mkaa gharama alizotumia fixed cost na variable cost zote ametumia 700,000 kupata magunia 70 ya mkaa.

Kwahiyo Average cost ni kuchukua 700,000 kugawa magunia 70 aliyoyapata = 10,000

Kwahiyo kwa kila gunia moja la mkaa ametumia gharama ya shilling 10,000 ku produce.

Sasa muuza mkaa akiamua kuuza gunia 1 kwa bei ya 50,000

Profit = ( Price - Average cost) x quantity

Faida = (Bei - Watani wa gharama) x idadi ya bidhaa

Faida = (50,000 - 10,000) x magunia 70

Faida = 40,000 x magunia 70

Faida = 2, 800,000 kama akiweza kuuza magunia 70 yote

Karibuni sana kuchangia mada.

#Averagecost #totalcost #output #profit #business #economics #example #swahili
 
Back
Top Bottom