Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Broccoli inafanana na cornflower isipokuwa ina rangi ya kijani. Inapatikana soko la Kisutu, Mwenge
FAIDA ZA BROCCOLI MWILINI
1. Mfumo wa Neva: Inasaidia kufanya mfumo mzima wa neva kufanya kazi inavyotakiwa na kufanya ubongo kufanya kazi yake vizuri kwa kuwa ina madini ijulikanayo kama potasiamu (potassium), na kisha misuli kuwa na nguvu.
2. Msukumo wa damu: Brokoli ina potasiamu na madini chokaa kwa wingi inayosaidia msukumo wa damu kuwa sawa.
3. Inapambana na sumu :Ina Vitamic C ambayo husaidia kupambana na sumu mwilini
4. Inalinda na kujenga mifupa: Vitamini K pamoja na Madini chokaa vinasaidia kujenga na kulinda mifupa.
5. Kuathirika na jua: Inasaidia kuondoa sumu ya kwenye ngozi pamoja na kurejesha uhalisia wa ngozi
6. Kinga dhidi ya maradhi: Ina zinki na seleniamu ambazo zinasaidia kuifanya kinga ya mwili kuwa imara.
NAMNA YA KUTENGENEZA/KUTAYARISHA
1. Unaweza kuchemsha peke yake ukazila zenyewe pamoja na supu yake (unaicha na maji maji)
2. Unaweza kuchanganya na carrots, gilgilani, cabbage ukazi steam kidogo