Napenda zaidi madawa yake fulani ya asili..
hata siku moja sijawahi ona akimwambia mtu kanunue Asprin au Klorokwin..
yeye atachanganya vitunguu saumu sijui malimao, asali na nanilii lohhhh dawa tayari..
Nampa heshma yake kwa kweli..
:lol::lol::lol: Unanifurahisha naandika hapa kwenye keyboard huku ninacheka kwa maneno yako kusema ukweli Madawa ya kizungu yaani Asprin,
Klorokwin na Madawa mengineyo mingi
tu ni yana madhara kwa mwili wa binadamu kwa kizungu tunaweza kusema kuwa madawa ya kizungu ya Side effects sio kama hayatibu la hasha yanatibu kwa haraka na yanakupa madhara mengineyo katika mwili . ukitaka kutumia Madawa
ya kizungu lazima utumie pamoja na Dawa za
Vitamins ili kukinga hizo
Side effects lakini pia hata hizo Dawa za
Vitamins zina madhara ndani yake. Lakini ukitumia Madawa Asilia kwa mfano Asali,Mdalasini,Kitunguu Maji,kitunguu Saumu,Pilipili
hoho,Tangawizi na kadhalika hazina madhara kwa binadamu hata kidogo. Ila unatakiwa utumie kwa kipimo chake. Mimi nilikuwa na Rafiki yangu Babu Mmoja Mnyamwezi Mtu wa Tabaora mnamo Mwak 1980 kabla sijasafiri nje ya nchi, hapo Dar
nilimshangaa Mzee huyo wa kinyamwezi ana umri wa miaka 90 ana wake 3 na ana nguvu za kiume. Nikamuuliza eti Babu mbona una wake 3 unazo nguvu za kiume?alicheka sana huyo Babu alikuwa ni Mganga wa kienyeji,akanipa Siri ya
mafanikio yake kwanini ana nguvu za kiume akaniambia kuwa nyie vijana mnatumia sana
mafuta ya kupikia ,sindano za Hospitalini,Mchuzi wa nazi Sukari nyingi yaani vitu vya vyakula vya sukari nyingi na Bamia ya mrenda ndio maana mnakosa nguvu za
kiume,hivyo akaniusia usitumie vitu hivyo kwa wingi utakuwa na matatizo ya nguvu za kiume. Mimi tangu siku hiyo nikashika hiyo miiko yake huyo babu wa kinyamwezi akanifundisha madawa mengi tu. Nakuacha hapo kwa leo mkuu Afrodenzi.
Kwa hiyo MziziMkavu, mie pia nacheka kila wakati hata usingizini hadi meno yanapauka. Ina maana sihitaji gym eeh?
Asante manake nakomboa mapene na wakati.
Na mimi pia unanifurahisha sana nikiangalia hiyo Avatar yako sijuwi shemeji yangu yaani mpenzi wako au mume wako akikukasirikia si utamuuwa kwa hiyo silaha yako bibie King'asti? avatar yako inanivutia lakini pia inanitia woga kidogo hahahahahahahha:lol::lol::lol: