Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Spinach ni mboga yenye faida nyingi kwa afya ya binadamu. Baadhi ya virutubusho vinavyopatikana kwenye mboga hii husaidia mwili kusafirisha vizuri hewa ya Oxygen, kutoa kinga dhidi ya magonjwa, kuongeza uzalishwaji wa damu pamoja na kuboresha afya ya macho, ngozi, nywele na mifupa.
Pamoja na uwepo wa faida lukuki zitokanazo na mboga hii, watu wenye changamoto ya ugonjwa wa figo huwa hawashauriwi kuitumia kwa kiasi kikubwa kwa kuwa huwa na wingi wa chumvi za Oxalate ambazo husababisha kutengenezwa kwa mawe kwenye ogani (organ) hizo.
Aidha, watu wenye tatizo la kuganda kwa damu kwenye mishipa hushauriwa kupata kwanza ushauri wa daktari kwani mboga hii huwa na kiasi kingi cha vitamini K ambayo huathiri utendaji kazi wa dawa zao, pamoja na kuongeza ukubwa wa tatizo hivyo kuhatarisha zaidi afya.
Chanzo: Medical News Today