Faida niliyopata kupitia mtandao wetu huu pendwa wa JamiiForums

Faida niliyopata kupitia mtandao wetu huu pendwa wa JamiiForums

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2020
Posts
7,799
Reaction score
14,215
Habari zenu wana JF wenzangu, ama baada ya salam ningependa sasa nijielekeze kwenye mada husika.

Ndugu wana JF wenzangu, leo ningependa niandike manufaa, au faida niliyopata kupitia mtandao wetu huu pendwa wa JF. Afu kama kuna mungine au wengine walionufaika na mtandao huu, basi walete ushuhuda wao hapa ili tuwapongeze waanzilishi na waendelezaji wa mtandao huu wenye member, wasomaji na wafuatiliaji wengi kuliko mtandao wowote hapa Afrika.

BINAFSI HIZI NDIO FAIDA NILIZOPATA KUPITIA JAMII FORUMS [emoji116]
1) Mtandao huu umenisaidia kupata marafiki wengi baadhi yao ni ndugu zangu, rafiki zangu na jamaa zangu wa kitambo (tuliokuwa tumepoteana), pia imenisaidia kupata marafiki wapya wenye vision na future mbalimbali.

2) Mtandao huu umenisaidia kujua mambo mengi kupitia thread mbalimbali za watu wenye maono. Pia nimekuwa nikipata taarifa nyingi kupitia mtandao huu, mfano habari za vifo vya marais wetu Benjamin Mkapa, John Magufuli na viongozi wengine waandamizi waliotangulia mbele ya haki.

3) Mtandao huu umekuwa ukiniliwaza katika nyakati ngumu mfano [emoji116]
a) Nikiwa na majonzi au huzuni> mtandao huu unanipa faraja na furaha.
b) Nikiwa na stress > mtandao huu huniondolea kabisa stress.

4) Mtandao huu umenisaidia kuona pale nilipokuwa sipaoni mfano [emoji116]
a) Kuna baadhi ya mambo nilikuwa siyafahamu, lkn nimeyafahamu humu JF kupitia thread na michango ya watu mbali mbali.
b) Kuna mambo nilikuwa nayasikia, lkn nimepata uhalisia wake kupitia thread mbali mbali hapa JF.

So kwangu mimi huu ndio mtandao bora kuliko mitandao yote ninayotumia, maana umeweza kugusa mambo yote yanayoihusu jamii kama vile michezo, siasa, mapenzi, historia, kazi nk.

Kwa sasa ningeshauri uongozi wa Jukwaa hili waweke na upande wa wale member wetu waliopoteana na ndugu zao, ili iwe rahisi kuwapata kupitia jukwaa hili.

Najua wengi wanatumia IDs fake, lakini member huyo mwenye ID fake anaweza kuandika jina halisi la ndugu yake aliyepotea, mwaka aliopotea kijijini au nyumbani kwao, picha au muonekano wake na baada ya hapo anaweza kuhusisha na PM yake.

Kwamba mhusika anayetafutwa akiwa humu au mtu anayemfahamu anaetafutwa akiwa humu basi aingie aingie PM kwa mtafutaji ili wangalie njia ya kuwasiliana katika mazingira halisi.

Ya kwangu ni hayo, kama kuna mungine anachochote cha kuchangia juu ya manufaa aliyoyapata kupitia mtandao huu wa Jamii Forum basi anakaribishwa kutueleza manufaa hayo ni yapi na yanamsaidiaje.

Asanteni sana moderators na wana JF wenzangu kwa kunisoma. WeekEnD NjEmA.
 
Jf ni zaidi ya UDUGU(IN Nyerere's voice)
sema wengi hatusemi mwakuwa mambo mengi na wabongo ni kawaida yetu kutokusifia!!
 
Jf ni zaidi ya UDUGU(IN Nyerere's voice)
sema wengi hatusemi mwakuwa mambo mengi na wabongo ni kawaida yetu kutokusifia!!
Uliyosema ni kweli kabisa, JF ni zaidi ya undugu. Wetu tumepata misaada mbali mbali ya kimawazo na hata kimaisha kupitia jukwaa hili.
 
Uliyosema ni kweli kabisa, JF ni zaidi ya undugu. Wetu tumepata misaada mbali mbali ya kimawazo na hata kimaisha kupitia jukwaa hili.
Kwa kawaida Kila kitu kinakuwa na pande mbili yaani strength and weakness mnapoanzisha nyuzi za kuonyesha uzuri wa JF siku nyingine sio mbaya kuandika na dark side ya mtandao huu.
 
Imenifanya nifikilie kuwa hakuna akitakacho mwanamke kwa mwanaume zaidi ya pesa. Niliingia kichwakichwa kwenye post za kina miss chaga na house girl kuwa pesa tu ndo inayotengeneza mapenzi kwa mwanaume. Nimekuwa nimtu nisiyejari mambo ya watu kama watu wa dar. Nimekuwa nikiona kila kitu nichakawaida hata kama nichaajabu mi sijari. Nimeonekana kama ninamajivuno kwa jamii kwa kutotaka kusikiliza pumba za jamii ninayoishi nayo hivyo inanichukulia nalinga hata mademu zangu nikiwa sina hela siwatafuti hivyo imenifanya niwe nalalamikiwa sana. Nimeanza kuwa na tabia za ki jf wakati jamii ninayoishi nayo iko huku nyashigwe hivyo ninaonekana waajabu huku

Kwa kifupi imenipa hasara na nimekuwa mlevi wa yenyewe
 
Kwa kawaida Kila kitu kinakuwa na pande mbili yaani strength and weakness mnapoanzisha nyuzi za kuonyesha uzuri wa JF siku nyingine sio mbaya kuandika na dark side ya mtandao huu.
Mkuu mimi kwa upande wang nimeona mazuri ndio mengi zaidi kuliko mabaya ndio maana nikayaandika.
Kwahiyo wewe kama umeyaona mabaya sio mbaya kuyaandika hapa au kuanzishia uzi wake na sisi tuchangie.
 
Back
Top Bottom