Faida utakazopata ukila mbegu za Maboga

Yah ni kweli kwa matumizi inategemea na mtu na mtu kwasababu kipimo cha hizo MBEGU kwa siku unatakiwa utumie kiganja kimoja cha mkono
Kwahio hapo utaona vipimo vinatofautiana mtu na mtu
 
Wax huwa zinakaangwa pamoja na chumvi tanga tunaita binjira pale inapokuwa tayari kwa kuliwa
Mkuu upo tanga sehem gani kwasababu biashara hio niliianzia tanga kule magaoni tairi tatu mpk mikanjuni
 
Naona madaktari wamekuwa wengi siku hizi mitandaoni....walianza na vumbi la Kongo, wakaja na mbigiri (miba za kukaanga), na sasa mbegu za maboga. Kaba ya mwaka kwisha tutasoma mengi ya kushangaza.
Hpn mkuu Unajua ukifuatilia kwa makini utagundua hii ni elimu tu tunapeana kwasababu mbegu za Maboga zipo kila mahali sio sawa na vumbi la Kongo hujui linatengenezwaje hlf mbegu za Maboga ni kama karanga lkn kuna vitu kadhaa vimeongezeka ndani yake
Kula uinjoi maisha
 
Zinapikwaje?
Unaziosha vizuri..unazichuja maji then unazitia na chumvi vilevile zikiwa na maji! Baada ya hapo unaziweka kwenye sinia kubwa unazitandaza vizuri unazieka juani zikauke
Zikishakauka unazikaanga kwenye sufuria na moto mdogomdogo! Zikishaiva ziko tayari kuliwa
 
Nawaekea wanangu kwenye uji wao! Ni mtamu
 
Tulipokuwa watoto tunachemshiwa maboga na mamumunya tulikula sana hizi mbegu. Hayo madini had leo yamejaa mwilini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…