Faida ipo hivi:
YouTube inamikikiwa na google ambao wana tawi lao la kupachika matangazo kwenye video za wanaoweka video YouTube, yani ni kama vile namwambia diamond aweke kipande cha tangazo language kwa sekunde tano kwenye video yake kwa malipo, ndivyo ilivyo YouTube, utaingia mkataba na google kwamba kwa kila watazamaji kadhaa watakulipa kiasi Fulani ili uwaruhusu waweke matangazo yao kwa sekunde chache kwenye video yako. Mara nyingi kibongo bongo mtu unakuta dola 600 ( takribani milioni 1.4 ), hivyo kwa watu kama kina Millard ayo unaweza kuweka video zake kama 100 hivi, hizi video zote za mwezi zinaweza kupata views milioni 5 hivi kwa hio hapa uhakika wa milion 7 upo.
Game la YouTube kwa watangazaji kama kina miladi limekua humu siku hizi, nakumbuka zamani miaka ya 2013 hadi 2016 Millard alishika kisawa sawa YouTube kwasababu hakukuwa na wapinzani wengi, enzi zile video zake nyingi zikikuwa ni views laki 3 na kuendelea, yani hata ikitokea shilole kufanya birth day ni Millard tu ndio alikuwa ana upload, Aisee kile kipindi bwana mdogo alizichapa sana pesa, kwa videos kama 100 mwezi mzima views zake zote zilikua zinaweza kufikia milion 20 zilizoweza kutema kama shillingi milioni 30 hivi au hata zaidi, kuanzia mwaka 2017 simu Kali zilivyokwa bei chee watu wakaanza kufanya YouTube na kurekodi matukio kwa simu zao na ndio hadi Leo watu channel zao zonatrend YouTube kwa kutumia simu zao.
Kwa kweli kwa sasa hivi inabidi uwe mbunifu sana ili uweze kutoboa YouTube tofauti na hapo zamani ambapo vifaa ndio vilikuwa kitu muhimu.
Gharama Zia YouTube kwa Tanzania endapo utakua unaripoti matukio ya kila siku kama mwandishi wa habari itakubidi ulipie milioni 2 hivi, uende ofisi za tcra utajaza fomu.
Endapo unatumia YouTube kutoa burudani kama msanii au kutumia YouTube kuelimisha Jamii, hakuna gharama