Faida ya Kampuni ya Bia #Tanzania (TBL) katika nusu ya kwanza ya mwaka 2018 imeshuka kwa asilimia 16

Francis12

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2016
Posts
7,533
Reaction score
22,281
Faida ya Kampuni ya Bia #Tanzania (TBL) katika nusu ya kwanza ya mwaka 2018 imeshuka kwa asilimia 16 hadi TZS bilioni 64.5 kutoka TZS bilioni 77.13 katika kipindi kama hicho mwaka jana. Kushuka huko kumechangiwa na kuzuiwa kwa pombe za viroba, na mazingira magumu ya biashara.
 
Sioni ajabu , Tangu nizaliwe nilikuwa sijawahi kusikia Benki 5 mfururizo zinafungwa. Jana tumesikia na vyuo vikuu vinafungwa. Sasa jiulize hapa kuna cha ajabu kusikia na biashara zinashuka?
Mfano mzuri ni barabara ya Ubungo hadi kibaha wananchi walivunjiwa nyumba zao, ujue kawaida maduka hupangwa barabarani. sasa kama nyumba zilivunjwa ujuwe maduka yalivunjwa taklibani mengi. Sasa niambie hapo Uchumi wetu wa Tz si uko ICU?
Indicators nyingi za uchumi kushuka ni pamoja na kujaa michezo ya bahati na sibu kwenye taarifa za habari mpaka zinaboa.
 
Lazima faida ishuke we unampangia mtu kunywa/kuuza pombe saa kumi alafu mwisho saa Sita!what do you expect

Sisi tuna uzi wetu wa walevi na wanywaji mwenyekiti Mshana mimi katibu!issue hii tumeilalamikia sana pmja na wajumbe huko

Ova
 
Kumbe ndiyo maana wanahisa hatujapata gawio letuuuu!!!
 
Si ndio hao hao wanauza pombe na kuzawadia polisi vya kupima watu pombe na kuwakamata.. badala ya kuelimisha wateja wanaenda kusaidia.. watu wataendelea kuacha kunywa pombe hizo.. uoga wasikamatwe😁

Wanalo..
 
Siku hizi watu wanapiga togwa,mbege na wanzuki wanaenda kulala,hawataki shida na mtu kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…