Faida ya kukimbia asubuhi na masuala ya kuzingatia

Faida ya kukimbia asubuhi na masuala ya kuzingatia

Dr Rutagwerera Sr

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2011
Posts
5,809
Reaction score
11,462
Watu wengi tumekua tukikimbia barabarani nyakati za asubuhi. Hizi hapa faida na masuala ya kuzingatia:

1. Unapata faida ya jua la asubuhi ambalo wengi tunalikosa tukiwa katika pilika za kawaida.

2. Muhimu kuhakikisha unafanya warm-up ya kutosha kwa sababu asubuhi mwili unakua hauna mijongeo ya kutosha ya kuuchangamsha mwili tofauti na jioni.

3. Kunywa maji ya vuguvugu kabla ya kwenda kukimbia. Usiende kukimbia ukiwa hujapata walau glasi 1-2 za maji ya vuguvugu. Muhimu kwa afya ya moyo na hydration.

4. Ukimbiapo barabarani muhimu kubana pumzi kwa sekunde chache ili kuepusha kuvuta hewa chafu za moshi wa magari. Na hilo hata kwa watembeaji wa miguu ni muhimu. Hili unafanya kila unapoona gari inatema hewa chafu au vumbi kutimka.

5. Kukimbia upande sahihi wa barabara ni jambo la kuzingatia.

NB: Kutematema mate wakati wa kukimbia ni dalili ya kutofahamu namna ya sahihi ya kupumua. Wanamichezo wengi wana tatizo hilo hata wachezaji wa soka.
 
Back
Top Bottom