Faida ya kula Mboga na Matunda mbalimbali kwa Afya yako

Faida ya kula Mboga na Matunda mbalimbali kwa Afya yako

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Matembele ni mboga maarufu sana, pia ni mboga yenye virutubisho sana,
Lakini matembele yana faida nyingi katika miili yetu.

FAIDA ZA MBOGA YA MATEMBELE KWA UFUPI

1: Matembele yana madini ya chuma. Madini haya ndiyo muhimu katika utengenezaji wa damu, kwa hiyo mtu anapotumia matembele anakuwa anaongeza kiwango cha damu mwilini. Watu wenye upungufu wa damu na kina mama wajawazito wanashauriwa kula matembele kwa wingi.

2: Matembele yana vitamini A ambayo husaidia kuimarisha macho na hivyo kumsaidia mtu kuona vizuri hasa hasa nyakati za usiku.

3: Matembele yana vitamini C Ambayo humlinda mtu asipate kiseyenye (scurvy). Vitamini C huimarisha ngozi na fizi, unapotumia matembele fizi zako na ngozi huimarika na huzuia kuvuja damu kutoka kwenye fizi.

4: Matembele yana protini ambayo husaidia katika kuimarisha misuli na kusaidia katika ukuaji wa mwili. Wape watoto matembele ili wakue vizuri.

5: Matembele yanasaidia kuongeza damu kwa wingi mwilini ikiwa utayachemsha na kula na maji yake kila siku

6: Matembele yanasaidia kuongeza nuru na kuboresha Afys ya macho

7: Matembe yanasafisha damu na kutoa mafuta machafu

8: Kamba lishe zilizo kwenye matembele ni chanzo cha kupata choo kikubwa vizuri
Kwani zinaboresha mfumo wa usagaji ( digestion)

MATAYARISHO
ILI UPATE FAIDA HIZI NI BORA UKAWA UNACHEMSHA MATEMBELE YENYEWE TUU UKAWEKA NYANYA NA VITUNGU NA CHUMVI KWA MBALI
UKATUMIA BAKULI KUBWA MOJA KILA SIKU

ANGALIZO
KWA MTU MWENYE VIDONDA VYA TUMBO HAYAMFAI AU GESI NYINGI
 

Fahamu umuhimu wa kula mboga mbichi (saladi)​



umuhimu wa kula mboga


KUNA watu wanapokwenda hotelini huagiza saladi tu. Salad ni mkusanyiko wa mboga za majani mabichi. Kinachotakiwa kujulikana ni kuwa ulaji wa mbogamboga zikiwa katika hali ya ubichi au zikiwa hazijapikwa una faida kubwa kiafya.

Hata hivyo, ulaji huo bila ya kuchukua tahadhari unaweza kusababisha magonjwa yanayoenea kutokana na kula vyakula vichafu visivyosafishwa vema. Katika maisha ya binadamu karibu kila jambo zuri linatakiwa kufanywa kwa tahadhari au kuchunga miiko yake, bila ya kufanya hivyo, faida ya jambo hilo haitapatikana na badala yake mtu anaweza kukumbwa na maradhi.

Ulaji wa mbogamboga zikiwa katika hali ya ubichi au zikiwa hazijapikwa una faida kubwa kiafya. Hata hivyo, ulaji huo bila ya kuchukua tahadhari utasababisha magonjwa yanayoenea kutokana na kula vyakula vichafu. Ni ukweli wa miaka mingi kuwa kupika au kutumia moto katika kuandaa vyakula kunaharibu virutubisho vya asili vinavyopatikana katika mbogamboga.

Mboga za majani kama mchicha, matembele, kisamvu, spinachi na kadhalika ambazo hazijakomaa na mbichi ni chanzo kikubwa cha vitamini na madini ya aina mbalimbali. Mboga hizo endapo zitakamuliwa na kutumiwa kama juisi, faida yake kiafya itakuwa kubwa hasa kwa wagonjwa.

Mbogamboga zinaondoa tindikali inayozalishwa wakati vyakula vingine vikisagwa tumboni kama vile nyama na jibini. Mboga za majani za kijani ni chanzo kikubwa cha carotene ambayo inabadilishwa mwilini na kuwa vitamini A. pia, ni chanzo kizuri cha vitamini C.

Vitamini A ina kazi kubwa ya kuimarisha macho ili yaone vizuri hasa wakati wa giza na ndiyo maana wapo wanaoshauri kula mchicha kwa wingi kama hawaoni vizuri hasa kama giza limeingia. Vitamini A. Mbogamboga pia, inasaidia pia ukuaji na ufanyaji kazi wa chembehai na kuimarisha kinga ya mwili.

Vitamini C ina kazi nyingi ikiwemo kuimarisha ufanyaji kazi wa chembehai, inaimarisha kinga, kuponya mafua na vidonda. Baadhi ya mbogamboga zina protini na wanga. Kwa mfano, maharage na kunde ni chanzo kikubwa cha madini ya chuma na protini.

Viazi mviringo na viazi vitamu ni chanzo kikubwa cha wanga mwilini. Siku hizi kuna kuongezeka kwa tabia ya watu kutumia mboga zikiwa mbichi kutokana na wengi kutambua umuhimu wake. Tunawahimiza watu watumie mboga mbichi kama vile saladi na kachumbari wakati wanapopata milo yao.

Wanaweza kuzitumia zikiwa zimekatwakatwa au kusagwa ili kupata juisi, lakini ni lazima kuzingatia usafi wakati wa kuandaa mboga hizo.

USHAURI​

Kwa ushahidi wa kutosha wa kisayansi, ulaji wa vyakula vibichi ambavyo havikuoshwa vizuri ni chanzo kikubwa cha magonjwa ya kuambukiza kama vile homa ya matumbo, kipindupindu, tumbo la kuhara, kuhara damu, kupata minyoo na amiba.

Kwa sababu hiyo, watu wanashauriwa kuosha vizuri mbogamboga kwa kutumia maji safi na salama. Pia, watu wale saladi na wanywe juisi ya mboga mbichi ili kupata virutubisho vingi zaidi. Mbogamboga kama matango, nyanya na karoti, zitumike kutengeneza juisi bila ya kuondoa maganda yake. Kwa sababu maganda yana madini na protini kwa wingi

UMAKINI​

Watu wawe makini kujua mahali zilipozalishwa mbogamboga wanazizonunua. Miaka michache iliyopita, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kiliwahi kufanya tafiti mbalimbali kuhusu ubora wa mbogamboga zinazozalishwa kandokando ya barabara zinazopita magari au katika bonde la Mto Msimbazi au mito mingine jijini Dar es Salaam. Tafiti hizo zilibaini kuwa baadhi ya mboga zilikuwa hazifai kuliwa na binadamu wala wanyama kutokana na kuwa na kemikali zinazodhuru afya hivyo ni muhimu kuwa makini
 
Hii mboga sio ya Kizungu, sidhani kama ni rahisi kupata jina lake la moja kwa moja
Nimejaribu ku-google......

Is it safe to eat sweet potato leaves?
Yes. Sweet potato plants are typically grown for their sweet tubers, but the leaves are great too. These edible leaves – scientifically called Ipomoea Batatas – contain high dietary fibre and can be absolutely delicious
 

Faida 20 Mwilini za Kula Bamia​



BAMIA.jpg
JAPOKUWA bamia huchukuliwa na wengi kuwa ni chakula rahisi kinachotumiwa zaidi na kundi la watu wenye uchumi wa chini na kati, ukweli kwamba aina hiyo ya mboga ina maajabu ya aina yake mwilini.



Walaji wa bamia hunufaika kwa kupata utitiri wa viinilishe vilivyomo kwenye zao hilo, ambavyo humpatia mlaji faida za kiafya takribani 20.

Mojawapo ya faida za ulaji wa bamia ni kuwasaidia wanawake kuepukana na changamoto za kiafya zinazojitokeza kwa baadhi yao ambao huwa na siku zisizotabirika za mizunguko yao ya kila mwezi.



Wapo wanawake wanaosumbuliwa na hedhi za mara kwa mara, ulaji wa bamia utawasaidia kuondokana na tatizo hili.

Faida nyingine ya ulaji wa bamia ni kuondoa vimelea vya sumu kwenye ngozi ya mwanadamu.



Ulaji wa bamia husaidia pia kukabili ugonjwa wa pumu. Huongeza kinga ya mwili na mtu akiwa na kinga ya mwili, hawezi kushambuliwa na maradhi mara kwa mara.

Faida nyingine ya ulaji wa bamia ni kupata virutubisho aina ya nyuzinyuzi ambavyo husaidia katika kusaga chakula tumboni.



Aidha bamia ni protini ambazo husaidia kujenga mwili.

Ulaji wa bamia husaidia pia kuimarisha afya ya nywele, kupambana na tatizo la uchovu wa mwili na pia msongo wa mawazo.

Kwa wale wenye tatizo la kupata choo kigumu, ulaji wa bamia husaidia kuondokana na tatizo hilo kwani husaidia kulainisha utumbo mkubwa (large intestines) kutokana na kazi yake ya kulainisha choo.



Bamia hutumika kwa kutibu vidonda vya tumbo, inasaidia kusawazisha asidi.

Fahamu kuwa bamia inaweza kukutoa katika hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari kwa sababu ya uwezo wake wa kusaidia kuyeyusha au kumeng’enya sukari.

Pia, huweka sawa mfumo wa sukari mwilini.



Bamia ni aina ya chakula chenye utajiri wa makapimlo ambayo ni muhimu sana katika mwili hasa katika usagaji wa chakula.

Mojawapo ya faida ambayo ni muhimu ni kusaidia kumeng’enya sukari mwili au kuweka sawa mfumo wa sukari mwilini na pia tatizo la kukosa choo ni tatizo la kawaida kwa wagonjwa wa Kisukari.



Bamia ikiliwa mara kwa mara inasaidia kurekebisha mfumo wa umeng’enya chakula na sukari mwilini.

Angalizo kwa wagonjwa wa kisukari, msiache dawa zenu na kuanza kutumia bamia kama dawa.

Majimaji yanayotoka katika bamia yana uwezo wa kuondoa lehemu katika mishipa ya damu kwenye mwili.



Tumia bamia mara kwa mara kama tunda mboga linalosaidia kumeng’enya sukari mwilini na kuimarisha kinga ya mwili wako.

Tukiachana na kisukari, bamia huongeza na huboresha kinga ya mwili hasa kwa watu ambao kinga yao ya mwili imeshuka kama vile watu wenye maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU).



Wataalamu lishe wanasema watu wengi wamekuwa wakila bamia kwa kuidharau ila huzuia magonjwa ya moyo kwa kuisaidia mishipa ya damu kufanya kazi vizuri.

Watu wenye matatizo ya vidonda vya tumbo, bamia huwasaidia kupunguza uwezekano wa kupata saratani ya tumbo na huongeza kiwango cha damu mwilini. Wengine wanatumia bamia kama dawa ya kuongeza kinga ya mwili kwa kutafuna zikiwa mbichi au kuzichemsha.



Faida nyingine ya ulaji wa bamia ni kuusaidia mwili kusafisha damu.

Ulaji wa bamia husaidia kutibu tatizo la upungufu wa damu. Bamia pia huondoa sumu mwilini na faida nyingine ni kuimarisha mifupa pamoja na mfumo wa uonaji kwa sababu ina chanzo kizuri cha vitamini A na Beta Carotene.



Bamia pia husaidia mwili kukabiliana na baadhi ya saratani. Utelezi wake huchuja uchafu unaoingia katika Kolestorali (cholesterol) na asidi ya nyongo inayoingia kutoka kwenye ini ambao usipodhibitiwa huenda ikasababisha matatizo ya kiafya.



Bamia ina Vitamin C ambayo inawafanya watoto wanaougua ugonjwa wa pumu kupumua vizuri wanapoitumia. Nusu kikombe cha bamia iliyopikwa, huwa na miligramu 13 ya vitamin C, ikiliwa husaidia sana.



Kwa wagonjwa wa kidondandugu (Cancer); wakitumia bamia husaidia kuweka utumbo kuwa na hali nzuri, hivyo kupunguza uwezakano wa kuugua ugonjwa huu wa kansa, hii hasa kwenye utumbo mkubwa.



Ulaji wa bamia pia husaidia mishipa midogo ya damu; kula kwa wingi kunasaidia kuimarisha mishipa hiyo midogo ya damu.

Watu wenye matatizo ya vidonda vya tumbo, bamia huwasaidia kupunguza uwezekano wa kupata saratani ya tumbo na huongeza kiwango cha damu mwilini
 
Nimejaribu ku-google......

Is it safe to eat sweet potato leaves?
Yes. Sweet potato plants are typically grown for their sweet tubers, but the leaves are great too. These edible leaves – scientifically called Ipomoea Batatas – contain high dietary fibre and can be absolutely delicious
Hongera
 
FAIDA YA TUNDA PARACHICHI (AVOCADO)
Ndani ya tunda hili kuna maji kiasi kidogo sana ukilinganisha na matunda mengine lakini kuna mafuta mengi na unaweza kuchanganya kula na tunda lingine kama vile apple, ndizi, chungwa au hata maziwa kwa kutengeneza juisi.

TINDIKALI
Licha ya kuwa na mafuta parachichi lina tindikali (acid) mbalimbali ikiwemo inayojulikana kama amino ambayo husaidia sana kukinga na kutibu maradhi katika mwili wa binadamu. Tunda hili pia lina protini ya kiwango cha juu.
Pia kuna tindikali inayoitwa oleic acid kwenye parachichi ambayo husaidia kukinga magonjwa ya moyo, kiharusi na kansa.

VITAMINI “E” NA B6
Imeelezwa na wataalamu kuwa tunda hili lina kiwango kikubwa cha vitamini E kuliko ile inayopatikana kutoka kwenye mazao ya wanyama.Parachichi lina vitamini hiyo nyingi kuliko inayopatikana katika mayai ambayo yanasifika kwa kuwa na vitamini e, hivyo hii inathibitisha kuwa lina faida kubwa mwilini.
Licha ya vitamini E pia ndani ya parachichi kuna vitamini B6 na kuna madini ya chuma (Iron) kwa wingi na madini ya potassium, pamoja na vitamin B6 na E mlaji anaweza kuletawa nafuu sana kama alikuwa na matatizo ya stress, matatizo ya uzazi kama ugumba na jogoo kutopanda mtungi Nguvu za kiume pia tunda hili linasaidia (impotence) .

FAIDA ZA PARACHICHI
Licha ya binadamu kufaidika na virutubisho vya tunda hili kuna faida nyingi za parachichi kama vile majani ya mti wake pamoja na magamba, baadhi ya watu hutumia kutibu maradhi ya kuharisha.
Majani na magamba hayo hutibu pia tatizo la gesi tumboni, kutuliza kikohozi pamoja na matatizo ya ini na kusafisha njia ya mkojo.
Hata hivyo, kwa mujibu wa wataalamu wa dawa za mitishamba, dawa hii haifai kutumiwa na wanawake ambao wana mimba kwani wakitumia inaweza kusababisha kuharibika kwa ujauzito.

HEDHI
Hata hivyo, wataalamu wa tiba mbadala wanasema dawa hiyo inaweza kuwasaidia sana wanawake ambao wameshindwa kuona siku zao kwa wakati, na wakitumia vyema wanaweza kuanza kuona siku zao.
Aidha, tunda hili linasaidia uyeyushaji wa chakula tumboni hasa kwa wale wenye matatizo ya vidonda vya tumbo, kwani parachichi lina nyuzinyuzi “fiber” ambayo ni muhimu kukinga kuta za utumbo. Watu wenye maradhi ya anaemia, diabetes, matatizo ya mfumo wa neva, matatizo ya mishipa ya moyo hasa wa artery wanashauriwa kula tunda hili mara nyingi.

Lakini pia tunda hili limethibitishwa na wataalamu kuwa linapunguza kwa kiwango kikubwa cholesterol kutoka kwenye damu hasa kwa watu wanene.
Tunda hili husaidia kulainisha ngozi na kuondoa mikunjo, hung`arisha na kulainisha nywele na kuzisaidia kukua pia kuziimarisha na kuzuia kukatikakatika.

Parachichi unaweza kulila kwa kulimenya au kwa kulisaga na kutengeneza juisi na kama nilivyoeleza hapo juu unaweza kuchanganya na matunda mengine kama tulivyoyataja na hutaharibu virutubisho vilivyomo badala yake utaongeza ubora wa juisi yako.
Watoto wadogo pia unaweza kuwapa tunda hili na wakafaidika na haya tuliyoyaandika.

Parachichi pia huweza kutumika kama siagi kwa kupaka kwenye mkate au kuchanganya na wali.
Haya wale wanaopenda ngozi zao za mwilini zisijikunje hata wakiwa watu wazima wadumu kula tunda hili kila siku katika maisha yao basi ngozi za mwili wao hazitajikunja hata usoni watakuwa kila siku vijana hata wakiwa wazee...
 
🌿🍀ZIJUE FAIDA ZA MMEA UITWAO UWATU KTK AFYA YA MWANADAMU🌳🌲
Mbegu za uwatu au kwa lugha ya kigeni Fenugreek, ni moja kati ya tiba-mbadala ambazo huweza kutumika katika kurekebisha hedhi za wanawake.
Mbegu hizi zinapatikana maeneo mengi hapa duniani na Tanzania.
Mbegu hizi pia hutumika katika kutibu matatizo mbalimbali ya kiafya katika nchi mbalimbali kama vile Misri, Ugiriki, Italia na Asia ya kusini. Mbegu hizi pia hutumika kama kiungo katika mapishi .
Mbegu za uwatu zimegundulika kuwa na virutubisho kama vile protini, vitamini, vitamin C, na madini ya potassium.
Kwakuwa mbegu hizi kuwa na tabia yakinishi za hormoni za Ostrogeni (estrogen-like properties), mbegu za uwatu zinasaidia katika kurekebisha 'moody' katika kipindi cha ukomo wa hedhi (meno-pause).
Mbegu hizi pia hutumika katika matibabu ya asthma, mfumo wa upumuaji, kurekebisha mmeng'enyo wa chakula, kuongeza nguvu za kiume, na matibabu ya ngozi.
Mbegu hizi pia hutumika katika matatizo ya uzazi, matatizo ya homoni, matibabu ya kisukari na kupunguza maumivu wakati wa hedhi

UWATU HUTUMIKA KATIKA KUPUNGUZA KIWANGO CHA CHOLESTEROL KWENYE DAMU
Uchunguzi unaonyesha kwamba iwapo mtu atatumia gramu 56 kila siku za mbegu za uwatu itasaidia kiwango cha cholesterol kwa asilimia 14 ndani ya miezi sita na atapunguza uwezekano wa kupata matatizo ya moyo kwa asilimia 25.
Mbegu hizi siyo lazima zitumiwe peke yake zinaweza kutumiwa au zikachanganywa na chakula kama vile achali n.k. vile vile zinaweza zikatumiwa kwa njia ya vidonge.

MATIBABU YA KISUKARI NA KIWANGO CHA SUKARI KWENYE DAMU
Mbegu za uwatu zimegundulika katika kusaidia kutibu kisukari (diabetes type 2) na kusaidia katika kurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu. Inashauriwa mtu atumia gramu 500 mara mbili kwa siku kila siku ili kupata matokeo mazuri.

KUTIBU MATATIZO YA NGOZI
Uchunguzi unaonyesha kwamba mbegu za uwatu husaidia katika matibabu ya matatizo ya ngozi. inashauriwa kwamba mtu atumie kijiko kimoja cha mbegu za uwatu na kusaga kuwa poda/ unga na kuchanganya na maji ya uvuguvugu na kupaka kwa kitambaa sehemu yenye jeraha au ilyoathiriwa.

MATIBABU YA KIUNGULIA
Mbegu za uwatu zinakiwango kikubwa cha uteute ambao husaidi katika kupunguza kiungulia kutokana na kuzuia asidi iliyopo tumboni isikutane na kuta za tumbo na utumbo.
Inashauriwa mtu kuchanganya kijiko kimoja cha chai simply cha mbege za uwatu kwenye chakula. Njia nyingine ni kunywa kijiko kimoja cha chai cha mbegu hizi na sprinkle 1 na maji au juisi.

MATIBABU YA HOMA
Mbegu za uwatu hutumika katika kupunguza homa iwapo zitatumika pamoja na maji ya limao au asali.
Ili kutibu homa inatakiwa mtu kutumia kijiko kimoja cha uwatu mara tatu kwa siku pamoja na chai (green tea), pamoja na kijiko kimoja cha asali na juisi ya limao.

KUONGEZA UKUBWA WA MAZIWA/MATITI
Mbegu za uwatu hutumiwa pamoja na bidhaa zingine katika kusaidia kurekebisha kiwango cha homoni katika mwili na hivyo kuongeza ukubwa wa maziwa au matiti. Ili kupata matokeo mazuri inatakiwa kufanya mbegu za uwatu kuwa sehemu ya mlo wako. Inashauriwa mtu atumie gramu 3 za uwatu kwa siku
 

UFUTA UNAVYOTIBU KISUKARI, SARATANI !​



KASHATA2.jpg


UFUTA au kitaalamu Sesamum indicum, hustawi na hulimwa zaidi mikoa ya Kusini mwa Tanzania ya Lindi, Mtwara na sehemu ya mkoa wa Ruvuma, Tunduru.



Hata hivyo, tafiti mbalimbali za ndani na nje ya nchi, zinaonesha kuwa ulaji wake ni kinga na tiba ya magonjwa katika mwili wa binadamu.



Baadhi ya magonjwa hayo ni kisukari, shambulio la moyo, kuimarisha mmeng’enyo wa chakula, huondoa lehemu, huboresha ngozi, huondoa na kukinga saratani na kuongeza damu. Pia ufuta huzuia mwili kuharibiwa na mionzi na mionzi ya jua, hulinda ini dhidi ya madhara ya pombe, hung’arisha ngozi na kuimarisha afya ya macho.
kashata.jpg


Faida nyingine kuwa ni kuzuia maradhi ya kinywa. Pia huimarisha mfumo wa upumuaji, lishe kwa watoto wadogo na kuimarisha afya ya nywele na hivyo kuzuia tatizo la nywele kunyonyoka na kuota nywele kwa wale wenye uhaba au kutoota nywele.



Hiyo ni kutokana na aina mbalimbali za virutubisho vilivyomo katika mbegu za ufuta kama vile, protini, mafuta, madini kadhaa kama ya kopa, kalishiamu (calcium), chuma, zinki, fosforasi, manganizi, magineziamu na thiamine.



KISUKARI:

Ufuta huzuia na kutibu ugonjwa huo kutokana na mbegu zake kuwa na madini ya magneziamu ambayo yakiwa mwilini huzuia visababishi vya sukari kama vile tatizo la insulini na kongosho kutofanya kazi ipasavyo. Pia mafuta ya ufuta huimarisha kuta za plasma na hatimaye kuwa na uwezo zaidi wa kuweka sawa kiwango cha sukari kwenye damu.

KASHATA4.jpg


KUKOSA CHOO, SARATANI

Mtu mwenye matatizo ya kukosa choo au choo kigumu, anapaswa kula kwa wingi ufuta kutokana na virutubisho hivyo kurahisisha mmeng’enyo wa chakula na kufanya hali hizo kutoweka na kuondokana na tatizo la ugonjwa wa bawasiri.



Kuhusu ugonjwa wa Saratani, mbegu za ufuta zina misombo (compounds) kama vile asidi aina ya phytic madini ya maginesiamu na phytosterols ambayo kwa pamoja huukinga mwili na kuondoa sumusumu zinazosababisha saratani. Ufuta pia ni tiba ya matatizo yanayokabili kinywa.



Kwa miaka mingi sasa watu wa kabila la Ayurveda huko barani Asia, wamekuwa wakitumia mafuta ya ufuta kama tiba na kinga ya matatizo ya kinywa ikijumuisha meno, fizi na kingo za mdomo au kinywa.
KASHATA3.jpg


SHINIKIZO LA DAMU (PRESHA), MATATIZO YA UZAZI, KUONDOA KITAMBI

Ufuta hutibu pia matatizo ya moyo na shinikizo la juu la damu (presha ya kupanda) ambapo mara baada ya kula ufuta hushuka na kuwa la wastani kwa muda mfupi ikiwa matumizi yake yatazingatiwa.



Ufuta huweza kuimarisha moyo na kuulinda usishambuliwe na magonjwa ikiwa ni pamoja na kushusha ‘presha’ ya juu kutokana na virutubisho hivyo.
FIX4-1.jpg


MATATIZO YA FIGO, KIBOFU…

Ufuta ni tiba muhimu katika tiba ya figo ikiwemo kuondoa mawe kwenye figo na matatizo ya kibofu. Pia una uwezo wa kutibu kipindupindu na kuzuia kuhara, kuweka sawa homoni zinazosababisha mzunguko wa hedhi kwa mwanamke kwenda sawa.



Huongeza nguvu kwenye mifupa na kuimarisha misuli mwilini kutokana na kirutubisho cha Kalishiamu kilichomo. Huzuia na kutibu maumivu ya tumbo ya ghafla.



Ufuta pia ni tiba nzuri kwa matatizo ya mfumo wa upumuaji kwani virutubisho vilivyomo huyakinga mapafu dhidi ya hewa chafu na magonjwa yanayoambata na kusababisha mfumo wa hewa kutokuwa mzuri.
INI3.jpg


MATATIZO YA INI NA MACHO

Mtaalamu mwingine wa tiba lishe, Dk. Josh Axe wa nchini Marekani anasema kupitia kitabu chake cha Eat Dirt kuwa ufuta hulinda ini dhidi ya magonjwa.



Hiyo ni pamoja na kulifanya ini kuwa na uwezo wa kufanya kazi ipasavyo na kuliepusha na magonjwa hasa ikiwa limeathiriwa na pombe kwani ufuta huondoa sumu zilizomo zinazotokana na matumizi ya pombe.
 
UMUHIMU WA NDIZI KWA AFYA
YAKO:
1614399402456.png

Naam. Baada ya kusoma makala hii hutaiangalia ndizi tena kwa mtaazamo uleule uliozoea

• Ndizi imejumuisha aina tatu za sukari ya asili ambazo ni glukosi, sukrosi na fruktosi.

• Ndizi hutoa nishati muhimu, ya kudumu na ya kutumika wakati wowote mwilini.

• Utafiti umethibitisha kwamba ndizi mbili tu zinatosha kuzalisha nishati ya kuufanya mwili ufanye kazi ngumu kwa dakika tisini. Hakuna shaka ndizi ndiyo kipenzi namba moja kwa wanariadha wanaoongoza duniani.

• Lakini nishati siyo pekee ambacho ndizi yaweza kutupatia nguvu ili kuilinda afya yetu. Pia inaweza kutusaidia kukabiliana au kutulinda dhidi ya magonjwa sita. Hizi ndizo zinazofanya ndizi kuwa muhimu katika mchanganyiko wa milo yetu ya kila siku.



MIONGONI MWA FAIDA ZA KULA NDIZI:

KULETA RAHA
: Kutokana na utafiti uliowahi kufanyika, watu wenye matatizo au ukosefu wa raha maishani, wamejiona wakirudia furaha waliyokuwa nayo awali baada ya kula ndizi. Hii ni kwa sababu ndizi ina aina ya protini ijulikanayo kitaalam kama tryptophan ambayo mwili wetu huibadilisha na kuwa serotonin, ambayo hukufanya ujisikie mwenye furaha.

VITAMINI B6 iliyopo kwenye ndizi husaidia kurekebisha glukosi iliyopo kwenye damu na hivyo kuboresha hali ya mwili na kukufanya ujisikie vizuri.

ANEMIA: Ndizi pia ina kiasi kingi cha madini ya chuma ambayo husaidia kuchochea uzalishaji wa chembechembe nyekundu za damu, hivyo husaidia mwili kujikinga dhidi ya maradhi mbalimbali, kama anemia.



Tafiti za Sehemu mbalimbali zimethibitisha uwezo wa ndizi kukabiliana na matatizo mbalimbali ya kiafya.

SHINIKIZO LA DAMU: Tunda hili lina kiasi kikubwa cha madini ya potasi na kiasi kidogo cha chumvi na kuifanya kuwa bora katika kudhibiti maradhi ya shinikizo la damu. Hii imethibitishwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani.

UWEZO WA KIAKILI: Ushahidi unaonyesha kwamba takribani wanafunzi 200 huko Marekani walisaidiwa kufaulu mitihani yao kwa kula ndizi wakati wa kufungua kinywa na mlo wa mchana. Hii ina maana kwamba huongeza uwezo wao kiakili. Kichocheo kikubwa cha kupata akili ni madini aina ya potasi yaliyomo.

KUVIMBIWA: Kambakamba za protini zilizomo kwenye ndizi zinasaidia kuzabua tindikali (antiacid). Hivyo kama mtu ana tatizo la kiungulila ajaribu kutumia ndizi ili kupata nafuu. Aidha ndizi husaidia kurejesha hali ya utendaji kazi wa kawaida wa tumboni. Ikiwemo kudhibiti kuvimbiwa bila kutumia kemikali.

KUHARISHA: Kula ndizi mbivu tatu kubwa na huzuia aina nyingi za miharisho na msokoto wa tumbo.

MAUMIVU YA KICHWA: Moja ya njia nyepesi na ya haraka ya kukabiliana na maumivu ya kichwa ni kwa kula ndizi iliyosagwa na kuchanganywa na maziwa. Hii husaidia kusawazisha sukari ya ziada kwenye damu.

Wataalam wamethibitisha kwamba kiafya ndizi ni tunda bora zaidi ya mengine .

Kusaidia mwili kuwa katika hali nzuri wakati wote. Wakati ikifanya hivyo vilevile hurudisha kiwango cha maji kinachohitajika mwilini.

HOMA NA UCHOVU WA ASUBUHI: Ulaji wa mara kwa mara wa ndizi husaidia kuongeza sukari mwilini, hivyo kuondoa hali ya homahoma na uchovu.

KUUMWA NA MBU: Kabla kutumia krimu kusugua sehemu yenye maumivu ya kuumwa na mbu, jaribu kutumia ndizi mbivu. Utashangazwa na matokeo yake.

KUONGEZEKA UZITO: Uchunguzi uliofanya katika Chuo cha Mambo ya Saikolojia nchini Australia, ulibaini kwamba shinikizo la kazi huchochea watu wengi kula vyakula kama chokoleti na mikaango mbalimbali. Ulitafiti kwenye wagonjwa 500 waliolazwa hospitalini, ulionyesha kwamba wengi wana vitambi na kutokana na kazi zenye shinikizo kubwa. Uchunguzi ukahitimisha kwamba watu wajihadhari na vyakula vinavyochochea mifadhaiko ya akili. Hivyo ikapendekezwa kula zaidi vyakula vya wanga. Ambavyo hupunguza kiwango cha sukari mwilini.

VIDONDA VYA TUMBO: Ndizi hutumika kama mlo kwa wagonjwa wenye matatizo haya kwa sababu ya ulaini wake. Ndizi mbichi za kupika ndizo zifaazo hapa. Hizi husaidia kupunguza tindikali ya ziada tumboni, pia kusambaa kwenye kuta za tumbo na hupunguza maumivu.

UDHIBITI WA JOTO LA MWILI: Tamaduni nyingi zinakubali kwamba ndizi ni kipoozi cha joto la mwili ambalo husababisha na hali mbalimbali zisizo za kawaida mwilini. Mathalani huko Thailand akina mama waja wazito hutumia ndizi kuhakikisha watoto wanaowazaa wanakuwa katika hali nzuri na ya ubaridi.

UVUTAJI TUMBAKU: Ndizi huwasaidia watu wanaojaribu kuacha kuvuta tumbaku. Vitamini B6 na B12, potassium na maginesiam ipatikanayo kwenye tunda hili husaidia kuondoa athari ya sumu iitwayo nikotini.

UCHOVU: Madini ya potasi yaliyo kwenye ndizi husaidia kutuliza mapigo ya moyo na kuwa ya kawaida. Hupeleka hewa safi kwenye ubongo na kurudisha kiwango cha maji kinachohitajika mwilini. Wakati tukiwa wachovu kiwango cha utendaji kazi wa mifumo mbalimbali ya mwili huongezeka na hivyo hupunguza kiasi cha potasi mwilini, upungufu huu hufidiwa kwa kula ndizi mara kwa mara.

HITIMISHO: Hivyo ndizi ni dawa ya kuponya maradhi mbalimbali. Aidha zina utajiri mkubwa wa protini mara nne zaidi, mara mbili zaidi ya wanga, mara tatu zaidi ya madini ya fasifarasi, mara tano zaidi ya vitamini A na madini ya chuma, ukilinganisha na aina zingine za vyakula. Pengine ni wakati muafaka kuzingatia msemo “kula ndizi kila siku kuepuka kuonana na daktari”
 

Maziwa Mgando Yana Manufaa Mwilini​

1614399763342.png
MTINDI unaorodheshwa kuwa miongoni mwa vyakula bora kwa sababu una virutubisho vingi vya aina mbalimbali ambavyo vina faida nyingi katika mwili wa binadamu.

Mtindi ni chanzo kizuri cha ‘Calcium’, ‘Phosphorus’, ‘Riboflavin (vitamin B2), ‘Iodine’, ‘vitamin B12’, ‘Pantothenic acid (vitamin B5) ‘Zinc’, ‘Potassium’ na ‘Molybdenum’.
Mbali ya virutubisho hivyo, ndani ya mtindi kuna ‘bakteria hai’ ambao ni muhimu kiafya katika mwili.
Kinga kwa wanawake
Mtindi una uwezo mkubwa wa kutoa kinga dhidi ya maradhi ya kuambukiza ukeni (vaginal infections). Wanawake wenye magonjwa ya kuambukiza sehemu za siri, wanapaswa kutumia mtindi kiasi cha pakiti moja kila siku kwa muda wa miezi sita. Maambukizi waliyokuwa nayo wanawake hao kabla yatatoweka.
Huondoa lehemu mbaya mwilini
Katika hatua nyingine, mtindi umeonekana kuwa na uwezo wa kupunguza kiwango cha lehemu mbaya mwilini, na wakati huo huo kupandisha kiwango cha lehemu nzuri mwilini. Hii inamaanisha kuwa, ikiwa mtindi unaondoa lehemu mbaya, mtumiaji anajiepusha pia na hatari ya kukumbwa na tatizo la shinikizo la damu.
Kusaidia mmeng’enyo wa chakula
Kama unapata shida ya kupata choo, basi mtindi unaweza kukusaidia kwa namna moja ama nyingine. Viritubisho vilivyomo kwenye maziwa (probiotics) husaidia sana kupunguza kukosa choo pia huzuia kuharisha.
Kupunguza uzani
Mtindi una kiwango kikubwa cha protini na protini ni muhimu sana katika kudhibiti hamu kubwa ya kula kwas ababu wakati mwingi utakuwa huhisi njaa.
Mtindi pia ni kinywaji kizuri sana kutumia mara tu baada ya kufanya mazoezi. Kuna watu wengi huwa wanatumia protini shake kama kinywaji baada ya mazoezi na ukweli ni kwamba hizi shake nyingi ni bei ghali sana kwa hiyo mtindi unaweza kuwa suluhisho lako kwani una uwiano mzuri wa protini na wanga.
 
Back
Top Bottom