Faida ya kutumia mbegu za ufuta

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363

Mbegu za ufuta

12 Health benefits of sesame seeds



1. Sesame seeds contain Vitamin B1,B2, B3 and E.

2. They have powerful antioxidants and help to fight cancer.


3. These oil seeds contain antioxidants sesamol and sesamolin

which protects the sesame oil from rancidity. Hence foods fried in

sesame oil have long shelf life.


4. Sesame seeds are oil seeds and contain monounsaturated and polyunsaturated fatty acids.


5. They also contain minerals like iron, calcium, magnesium and potassium.


6. These seeds supply required iron and minerals in lactating

mothers. Texts of ayurveda eulogize the galactogague properties of sesame seeds.


7. Texts of ayurveda recommend usage of roasted and powdered sesame seeds along with gur in conditions like painful menstruation.


8. Chewing of sesame seeds help to reduce toothache.


9. Consuming sesame seeds along with whole grains help to regularize bowel movement and relieve constipation.


10. They act as brain tonic.


11. Regular consumption of sesame seeds help to strengthen the bone and prevent osteoporosis. The minerals calcium and phosphorus present in these seeds, help to build strong bones.


12. Ayurveda acharyas recommend consuming of these seeds in diabetes to reduce frequency of micturition.

MWENYE KUTAKA KUNENEPA ABWIE ALE KILA SIKU UFUTA

MBICHI ATANENEPA MWILI WAKE





 
Mkuu Dr. MziziMkavu hakika nazikubali hizi punze na akina mama (food processors) wanazitengeneza ila tatizo wanaweka sukari nyingi. Natamani wangekuwa wanazitengeneza kwa kugandisha na asali. Ila mkuu nakuomba utoe somo upya kwa mafuta ya ubuyu maana TFDA wanazingua. Watu wako dilemma hasa wale ambao wameshatumia mafuta ya ubuyu na wakapata nafuu ya matatizo yao.
 
hii inafaa kuikaanga na kutwanga kwene kinu weka chumvi kwa mbali then songa ugali mkubwa hakika u will never regreat itakua mboga yako kuu na utatamani ureplace nafasi ya kula kuku kwene menu yako.
 
Mkuu Zogwale tungojee hao Mamlaka ya

Chakula na Dawa (TFDA) waje kusema kuwa hata huo Ufuta haufai kimatumizi hahahah. Nitacheka sana Kusema ukweli hawa viongozi wa

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) wanatuchanganya kuhusu hayo mafuta ya ubuyu mbona walikuwa hawajasema siku nyingi mpaka

hivi majuzi ndio wanasema hayo Mafuta ya Ubuyu yana madhara? Mimi ninashindwa kuelewa kabisa, siku zote walikuwa wapo wapi

wananchi wanatumia mafuta hayo ya Ubuyu mpaka majuzi ndio wanawakataza wananchi wasitumie mafuta ya Ubuyu kama ni dawa .?


TFDA inastahili lawama kwa mafuta ya ubuyu


MAONESHO ya 37 ya Kimataifa ya Biashara yamemalizika ambapo kampuni, taasisi, mashirika, wafanyabiashara na wajasiriamali walishiriki kuonesha bidhaa na kazi zao kwa wananchi na wageni kutoka ndani na nje ya nchi.

Katika maonesho hayo bidhaa zilioneshwa na waliokuwa na nafasi walizinunua ili mradi kila aliyeingia na kutoka alifurahia kwa nafasi yake.

Hata hivyo wakati wa maonesho hayo, iliibuka taarifa ya kuwa matumizi ya bidhaa zinazotokana na ubuyu yakiwamo mafuta, zina

athari mbaya kwa afya ya binadamu.


Taarifa hiyo ya kuogofya ilitolewa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ambayo nayo ilikuwa na banda lake katika

maonesho hayo maarufu kama Sabasaba.


Kauli hiyo ya TFDA imeonesha kuwashangaza na kuwashitua wengi, kwa sababu ni kweli bidhaa za ubuyu zimekuwa maarufu

hivi sasa zikitumiwa na makundi ya watu kwa ajili ya tiba mbadala.


Kwa mujibu wa wajasiriamali wanaofanya biashara ya kuuza bidhaa hizo, wanaeleza kuwa zimekuwa zikitumika kutibu vidonda

vya tumbo, uvimbe tumboni, ngozi na wagonjwa wa Ukimwi ambao CD4 zao zimeongezeka kwa kutumia bidhaa hizo.


Si hivyo tu, bidhaa hizo za ubuyu yakiwamo mafuta na unga, zimekuwa pia zikitumika kwa wanaotaka kupunguza vitambi na uzito

wa miili yao.


Juisi ya ubuyu imekuwa ikutumiwa kama njia ya kusafisha mwili na wengine wamekuwa wakikiri kuwa wanapotumia wanajisikia

mwili kupata nguvu.


Kwa msingi huu, naungana na hoja ya wajasiriamali kuhoji kwamba TFDA siku zote ilikuwa wapi, mpaka sasa ndipo inakuja

kutangaza, kwamba mafuta ya ubuyu yana athari kwa afya.


Najiuliza kwa sababu bidhaa hii haiuzwi kwa siri, wanaofanya biashara ya mafuta hayo na zingine za ubuyu wamekuwa

wakitangaza na kuuza kwa uhuru sehemu mbalimbali, hivyo hata TFDA walikuwa wakisikia.


Cha kujiuliza ni kwa nini wamesubiri hadi leo ndipo wanatangazia umma, wakati watu wameshatumia kwa muda mrefu,

inashangaza sana kuona mamlaka husika imekaa kimya siku zote wakati Watanzania na watumiaji wengine wanatumia bidhaa

ambayo kumbe ina madhara kwa afya zao.


Mtazamo wangu ni kuwa mamlaka husika imeshindwa kuwajibika na tunaweza kusema kama bidhaa hiyo ina athari basi

Mamlaka hiyo imehusika kuathiri afya za Watanzania.


Haya si matukio ya kwanza, zimekuwepo bidhaa zisizofaa kama dawa, vipodozi, sabuni, mafuta na vingine kama hivyo vikiuzwa

madukani na baadaye kusikia mamlaka husika zikiibuka kuzuia au kupiga marufuku.


Kuna kila sababu ya TFDA kujipanga vema na kuhakikisha inafanya kazi yake ipasavyo, ili bidhaa zisizofaa kwa afya za watu

zizuiwe sawia zinapogundulika.


Naamini TFDA ina wataalamu wenye uwezo wa kungamua bidhaa zenye madhara kwa wananchi, hivyo wawajibike na kufanya

kazi yao kwa weledi, hii tabia ya zimamoto kwa Mamlaka muhimu kama hii haipendezi.


Lakini pia uwepo utaratibu wa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu bidhaa zinazooneka kuwa hazifai kwa afya zao ili hata

wanapokutana nazo, wasikubali kushawishiwa na kuzinunua.



Hata kwa hili la ubuyu, tunaomba TDFA itoe maelezo ya kitaalamu na kwa kina ili wananchi waweze kujiridhisha na kuacha

kuyatumia, maana mara nyingine maneno bila vithibitisho vya kisayansi, watu wanakuwa wagumu kukubaliana na hali halisi.


http://www.habarileo.co.tz/index.php/wazo-langu/13944-tfda-inastahili-lawama-kwa-mafuta-ya-ubuyu
 

Mkuu Dr. MziziMkavu nimeshangaa sana. Bidhaa za ubuyu zimekuwepo tangu tuzaliwe watoto wanakula ubuyu hasa wa uswahilini. Na ukiafanya ka utafiti kadogo watoto wa uswahilini wanaokula ubuyu na ukwaju wana immune kubwa sana na ndio maana magonjwa kwao hutayasikia (nazungumzia infections kama za UTI, sijui kooo, na mengine). Yatokanayo na uchafu yanaweza kuwa ni hatari kwa uswahilini (kuhara na kipindupindu). Cha pili haya mafuta ya ubuyu wakazi wa Dodoma wameanza kuyatumia sana kabla ya kufika hata sokoni. Pia wamekuwa wakisaga mbegu zake na kuweka kwenye mboga kama kiungo. Sasa kwa health statistics ni mikoa gani inaongoza kwa cancer? Je Dodoma ni mojawapo? Kama kuna mwekezaji anaitaka hii biashara ya ubuyu aweke wazi na si kuleta longolongo. Nina rafiki yangu ni VVU na majuzi hapa aliugua typhoid na CD4 zilishuka hadi 300. Nikachukua hatua ya kumnunulia mafuta ya ubuyu kunywa kwa dose na kujipaka maana alibabuka ngozi pia. Unga wa ubuyu akawa anakoroga juice asubuhi na jioni. Kwa sasa ni mzima na CD4 zimepanda maana yale magonjwa yalimwandama CD4 ziliposhuka hayapo tena. Ngozi imenawiri kwa kujipaka mafuta ya ubuyu. Hakika sijui kama ukimwambia mtu kama huyu kuwa ubuyu haufai kama atakuelewa. Serikali ijipange upya ije na strong evidences.
 

Nimewaelewa vizuri TFDA, Wametoa maelezo mazuri sana. Wamekiri pia kuwa, Mafuta ya Ubuyu yanafaa sana lakini ni vizuri "yakajujwa" kwa umakini na utaalaam ili kupunguza tindikali yenye sumu inayafikia hadi asilimia kumi na ibaki walau chini ya asilimia 0. Mchakato wa aina hii hufanyika pia katika mafuta ya pamba. Ni masuala ya kitaalam zaidi tuyaache kwa wenye mamlaka kwa manufaa yetu sote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…