Kuna nyuzi za kutosha tu humu zinazo ongelea hayo masuala ya uwakala wa mitandao ya simu, na pia ile ya kibenki.
Kiufupi mawakala hupata faida kupitia commission inayopatikana kila mwanzo wa mwezi, na hiyo ni baada ya kuzungusha mtaji ulionao kwa mwezi mzima. Ukifanya miamala mingi ya kuweka na kutoa, na commission inakuwa kubwa zaidi ya yule alifanya miamala michache.
Kuongezeka kwa tozo, uwepo wa Matapeli, vibaka, na majambazi; ndiyo changamoto kubwa ya hii biashara.