Faida ya mboga za majani kwa afya

Faida ya mboga za majani kwa afya

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Hakuna aina moja ya mboga za majani inayotosha kukupatia virutubisho vyote muhimu ili uweze kuimarisha afya yako.

Ni muhimu kutokutumia aina moja ya mboga kila siku kwa kuwa haiwezi kukupatia virutubisho vyote unavyohitaji, bali jitahidi kuchanganya au kubadili mara kwa mara ili uweze kunufaika vizuri.

Mboga za majani huwa na faida zifuatazo kwa afya-
  • Huwa na nyuzinyuzi zinazosaidia kuboresha mfumo wa chakula, kurahisisha choo na kutoa kinga dhidi ya saratani ya utumbo mkubwa
  • Aina nyingi za mboga za majani huwa na madini ya potassium ambayo husaidia kudhibiti shinikizo kubwa la damu na magonjwa ya moyo
  • Huwa na kipimo kidogo cha sukari (Low Glycemic Index) hivyo hufaa sana kwa watu wenye tatizo la ugonjwa wa kisukari
  • Kama ilivyo kwa makundi mengine ya chakula, mboga za majani hubeba virutubisho muhimu kwa afya yako kama vile vitamini A, vitamini C, asidi ya foliki, madini mbalimbali na viondoa sumu. Vyote hivi huhitajika mwilini ili kujenga afya.
Chanzo: WebMD
 
Uzi wako mzuri Ila utakosa wadau kwani watu WANAPOENDA upuuzi zaidi ya vitu vyenye msingi
 
Tule Mboga Mboga Kuliko Nyama Na Viungo Tele
 
Mboga za majani zote ni nzuri kwa afya zetu, Ila ukienda hospitali wanasifia Sana spinach.
 
Ila Mbona wanasema hazifai kwa wanaume?!
Yawezekana, Kuna Uzi nimesoma mda si mrefu, pia wamesema sio nzuri kwa watu wenye tatizo la Figo mpaka ushauri wa daktari.
 
Back
Top Bottom