WATEULE FAMILY
New Member
- Sep 5, 2022
- 4
- 6
UTANGULIZI
Sayansi Ni tawi la maarifa linalohusu nadharia, vipimo, uchunguzi wa hatua kwa hatua na uthibitishaji wa kuwepo au kutokuwepo kwa kitu au jambo katika hali halisi.
Tunaliona hili katika historia fupi ya sayansi.
Sayansi ilianza kama udadisi wa mtu mmoja mmoja lakini kadri maarifa yanavyo panuka
inakuwa vigumu kwa mtu mmoja kufanya mchango wa kujitenga.
Teknolojia Ni elimu inayohusu uhandisi, ufundi ujenzi, vifaa na mbinu za uzalishaji wa vifaa na huduma katika jamii. Tunaliangalia hili kwa uthibitisho wa kihistoria ya Teknolojia ya kwanza.
{Picha kutoka mtandaoni}
Kati ya mifano ya kwanza ya Teknolojia ya binadamu ni matumizi ya mawe kama vifaa Pamoja na matumizi ya moto.Tangu kupatikana kwa vifaa vya mawe wanahistoria wanahesabu kipindi hiki kama zama za mawe. Kuna mifano ya ncha za mawe kwa ajili ya mishale ya kuwinda tangu mwaka 64000kk lakini pinde za kwanza ambazo ni ubao zilipatikana tu tangu mwaka 800kk.
Kwa utangulizi huu mfupi zifuatazo ni faida nne zinazo chochea mabadiliko chanya katika jamii kwenye Nyanja ya Sayansi na Teknolojia;
Inakuza uhusiano na mawasiliano.
Sayansi na Teknolojia ni mojawapo ya njia kubwa katika ukuzaji wa uhusiano na mawasiliano katika Nyanja ya kijamii na kitaifa. Mfano, tunaona taifa letu la Tanzania namna ilivyokuza uhusiano na mawasiliano mazuli kwa mataifa makubwa duniani kwa lengo la kuwakalibisaha waje kuwekeza kulingana na ukuaji wao mkubwa wa Teknolojia katika Nyanja ya kiuchumi kwa ujenzi wa miundo mbinu bora kama vile, Mradi mkubwa wa UMEME BWAWA LA NYERERE, Mradi wa Reli ya kisasa Standard Gauge Railway (SGR) na Mradi wa Barabara za juu alimaalufu (FLYOVER).
Inakuza uzalishaji mkubwa wa malighafi.
Sayansi na Teknolojia imekuwa ni chanzo kikubwa cha uzalishaji wa malighafi kwa nchi na mtu mmoja. Tukiiangalia nchi ya Tanzania ni moja wapo wa wanufaikaji wa Teknolojia toka enzi za utawala wa kikoloni mnamo mwaka 1916 baada ya vita ya kwanza ya dunia na hadi kipindi cha mapinduzi ya viwanda mnamo mwaka 1881 toka kipindi hicho hata sasa tunaona katika Nyanja ya viwanda uzalishaji ni wa juu zaidi si kama zama za ukoloni kwani umekuwa wa mafanyikio makubwa kwa kutumia mitambo ya kisasa ya uzalishaji.
Inaimalisha njia za usafirishaji na miundo mbinu.
Sayansi na Teknolojia imekuwa ni moja wapo ya kichochezi cha uimarishaji wa miundo mbinu na njia za usafirishaji kwa ufikaji rahisi wa huduma kwa lengo la kuokoa muda na kuongeza mapato katika nchi na mtu mmoja. Mfano mzuri Tanzania ni nchi mojawapo apa Afrika kwa kunufaika na Sayansi na Teknolojia kwa kuimarisha miundo mbinu yake hasa katika njia za usafitishaji kama vile, ujenzi wa Reli ya kisasa Standard Gauge (SGR) na Barabara za juu pamoja na Madalaja makubwa.
Inakuza ufanisi wa utendaji kazi.
Kupitia Sayansi na Teknolojia imesaidia kuleta ufanisi mkubwa wa utendaji kazi kwa taifa na mtu binafsi Pamoja na jamii nzima kiujumla lengo kuu ni kukuza kipato pamoja na kukua kiuchumi. Ili tunaliona katika Nyanja tofautitofauti hapa nchi Tanzania kama vile, Nyanja ya Afya. Serikali imejitahidi kutoa fedha kwa ajili ya ununuzi wa mitambo ya kisasa ya matibabu mahospitalini hususani hospital kubwa za lufa hapa nchini kwa lengo la kuboresha huduma za afya zitolewazo. Mifano ya mitambo mikubwa ya matibabu ni kama ilivyo
onyeshwa katika picha.
{CT scan}
{Cathlab (Catheterization Laboratory)}
(Picha kutoka mtandaoni).
MAPENDEKEZO
Serikali inapaswa itoe uwezeshaji wa elimu ya Sayansi na Teknolojia ilikupata wataalamu wa kutosha kwenye idala ya Teknolojia ni Pamoja na kujenga vyuo vya kutosha ambavyo vitafundisha na kutoa wataalamu wenye ujuzi mkubwa kwa manufaa ya taifa letu na jamii kwa ujumla.
Tujifunze kwa nchi zilizoendelea kwenye Sayansi na Teknolojia kwani ni chachu kubwa ya maendeleo katika nchi yetu kwa kuona fursa nyingi za kutufanya tuweze kukua kiuchumi na kiteknolojia.
HITIMISHO
Ninapenda kumalizia kwa kuiomba serikali yetu na taasisi binafsi iwekeze katika maendeleo ya Sayansi na Teknolojia kwani ni mojawapo ya kichochezi kikubwa cha maendeleo katika nchi yetu ndani ya Nyanja ya kielimu, kibiashara, kiafya, kisiasa, kiutawala, kilimo na kiuchumi kwani itapelekea kumshinda adui yetu mkubwa umaskini.

Attachments
Upvote
7