Faida za Komamanga

Faida za Komamanga

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Komamanga ni mojawapo ya matunda yaliyodumu duniani kwa karne nyingi sana, kisayansi huitwa Punica granatum.

5E4B87F7-584A-4A11-A9E1-8F633713EA95.jpeg


Virutubisho
Huwa na muunganiko mkubwa wa kemikali za phenolics, flavonoids, ellagitannins, na proanthocyanidin, pamoja na madini ya potassium, calcium, phosphorus, magnesium na sodium.

Huwa pia na viondoa sumu, aina mbalimbali za sukari pamoja na kiasi cha kutosha cha aina mbalimbali za asidi.

Kwa mujibu wa USDA, maji, nishati, protini, zinc,vitamini C, folate, copper na selenium hupatikana pia kwenye tunda hili.

Faida zake
Baadhi ya faida ya tunda hili ni-
  • Kinga ya changamoto za tezi dume hasa kwenye kuzuia saratani na uvimbe
  • Huongeza uzalishwaji wa vichocheo vya kiume, maarufu zaidi kama testosterone ambayo huhusika katika kuratibu kazi zote zinazohusu tabia za kiume
  • Husaidia kuzuia, pamoja na kupunguza utengenezwaji wa mawe kwenye figo.
  • Huulinda moyo pamoja na mishipa ya damu
  • Hurejesha uhai wa misuli, pamoja na kupunguza uchovu kwa watu wanaofanya mazoezi magumu.
  • Hudhibiti miamsho inayosababisha kutengenezwa kwa aina mbalimbali za uvimbe na mizio (allergy) mwilini
  • Huongeza msisimko wa vimeng’enya vya insulin katika kudhibiti ongezeko la kiwango cha sukari mwilini. Ni tunda zuri linaloweza kutumiwa na watu wenye ugonjwa wa kisukari.
Chanzo: Afyainfo
 
Back
Top Bottom