Faida za kufungua kampuni

Basham

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2014
Posts
743
Reaction score
434
Imani iwe kwenu wana Jamvi.

Kama heading ilivo naomba kujuzwa faida ama hasara za kuendesha biashara kama kampuni maana nimefuatilia nimeona kuna utitiri wa kodi/gharama na uendeshaji kampuni. Mfano TRA TFDA TBS NEMC n.k kulingana na biashara unayoifanya.

Kila sehemu utakayo pita kuna gharama zake na ni za kila mwaka kubwa zaida ni 30% corporate tax ata the end of year.

Swali la msingi kulingana na gharama za uendeshaji kampuni. je kati ya kampuni na retail sales kwa wafanyabiashara wadogo ni ipi inalipa zaidi

Nawasilisha

Thanks in advance
 
Kumbuka microsoft,Apple,google inc.,facebook e.t.c zote hizi ni kampuni!!...Ukiwaza mambo ya gharama utabakia hapohapo!!.....business is all about taking risks!!.....Take risk now!!
Thanks mkuu lakini inawezekana sera za nchi zao zipo vizuri kwa nchi yetu kodi zipo juu sanaa unajikuta unafanyia kodi unapitwa mapato na machinga. All in all nitapambana tuu kitaeleweka
 
Hizo ulizotaja hazihusiani na kampuni bali biashara utakayofanya bila kujali ni mfumo upi unatumia kumiliki hiyo biashara. Kampuni hasara yake inategemea ni kampuni ipi kati ya Private na Public. Private ina faida dhidi ya public kwa biashara ndogo kwani haina paper work nyingi na pia haina followups kama za public. Hasara ya kampuni dhidi ya sole propriator ni gharama za ukaguzi na kusajili. Faida yake dhidi ya sole propriator ni kwamba kodi hulipwa kutoka kwenye faida kwa 30% wakati solepropriator unakadiriwa kwa hiyo hata kama umepata hasara mwaka huo kodi ni ya lazima. Faida nyingine ya kampuni ni ulinzi wa mali za wamiliki - wenye hiza tofauti na biashara binafsi ikidaiwa, mali za mmiliki kama nyumba itauzwa tu ili kulipa deni. Kampuni ina faida zingine lukuki tofauti na biashara binafsi
 
Kwa kuongezea kama biashara haitamiliki asset kubwa au kuingia kwenye biashara ya mikataba, sole propriator ni option nzuri japo ya mpito kwani biashara ikfanywa chini ya kampuni iko salama zaidi kuliko hii ya mtu mmoja
 
ushauri huu apa, kama biashara yako inategemea tenda kutoka katika makampuni menginne anzisha kampuni. Ila kama huitaji tenda kutoka kwenye makampuni n bora ufanye retail
 
Mikopo
Legal identity
Limited shareholders liability
Indefinite life
Transferability of ownership etc
 
Thanks mkuu umeeleza vemaa sanaa. I get the point
 
Kama unafikiri kuanzisha biashara ni muhim kujiua biashara ni system na Kuna watu muhim utahitaji kuwa nao.. Na Watu muhim ni mwanasharia, accountant. Pia lazima ujue kuwa kila business Zina sheria zake na zinatofautiana viwango vya kodi.. Business is the system.
 
Thanks
 
ushauri huu apa, kama biashara yako inategemea tenda kutoka katika makampuni menginne anzisha kampuni. Ila kama huitaji tenda kutoka kwenye makampuni n bora ufanye retail
Hapo mwisho,, kwani kampuni haiwezi kufanya retail?
 
Hapo mwisho,, kwani kampuni haiwezi kufanya retail?
Kwa kampuni ili uifaidike vizuri ukiwa na kitu cha kuproduce(Production) ndo inakua poa zaidi.
 
FAIDA ZA KAMPUNI:
1.Kodi inatozwa kwenye faida utakayopata.
2.Makadirio ya kodi utafanya mwenyewe.
3.Inatambulika kisheria(legal entity).
4.Kama una hasara hutakiwi kulipa kodi.
5.Ni rahisi kukopesheka kama biashara iko vizuri.
6.Baada ya December kukamilika utaandaa mahesabu ya mwaka ( kuna gharama hapa ya mhasibu na mkaguzi-auditor),uzuri gharama hii utaitambua kama matumizi ya kampuni.

NOTE: Kama unamalengo makubwa nakuomba uwaze kuwa na kampuni hata kama utashindwa kwa sasa ila baadae jitahidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…